Viwanja na nyumba zisizopimwa hii imekaaje

Simba Mkali

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
620
239
Nilimsikia Mh. Lukuvi akisema kwamba viwanja ambavyo havijapimwa na nyumba zilizopo sehemua mbayo haijapimwa vyote vinatakiwa kulipiwa kodi. Unachotakiwa kama unamiliki nyumba (au kiwanja) hapa Tanzania hususan sehemu ambayo haijapimwa uende Manispaa na karatasi yako ya manunuzi ya kiwanja ili ukadiriwe kulipa kodi na mwisho mwezi wa sita... Jamani nataka kujua hili utekelezaji wake umekaaje? Au kuna tamko mpya
 
Mm nasubiri nikamatwe!!
Maasifa ardhi wake wamejaa tu maofisini kwenda SITE kupima hakuna!!
Siwezi kulipa hata Plot No sina, square meter sijui.., umeme kwangu hakuna, maji hakuna, sewerage system hakuna!!

Yy kwenye ardhi yangu kafanya VALUE ADDITION IPI?
 
Nijuavyo hiyo kauli ya Lukuvi haitekelezeki ikizingatiwa kuwa wenyekujua mauziano halali ya ardhi ni viongoz wa vijiji na mitaa...sasa hao maafsa ardhi hawawez kukurupuka bila waraka unaowaelekeza cha kufanya.mimi kwangu naona kama mwendelezo wa matamko tu.
 
Tukumbuke hapa tz kila jambo ni fursa kwa baadhi ya watu hebu fikiria 1 unaenda kulipia nyumba ilyopo mtaa----kitalu----block---2unaenda kulipia kiwanja ndo kabisaaa sijui hata wewe mlipaji utasema unalipia nini? Tuwe makini kwa hili tz ni ya wajanja ukiliwa usilie hapo kutakua na sintofahamu nyuma ya mlango sishawishi watu wasilipe maana hawakawii kusema ni uchochezi hayo ni maoni tu
 
Back
Top Bottom