Vivuko vya Azam pale feri Dar es salaam kuna dalili za Ufisadi

Kama uwepo wao/dili hilo linatatua shida za watu, sioni tatizo.
 
Vivuko vyetu vinakalishwa sana tena makusudi huku Abiria wakipakiwa kwenye vile vya Azam. Sijui Azam wanalipwa kwa idadi ya trips wanazofanya?
Mkuu 'Missile', mara kwa mara huwa napenda sana aina ya mijadala unayoiibua hapa JF.

Kwa mfano hii ya leo, ni mfano mzuri sana kwa mtu anayependa kutetea hoja yake ya kwamba serikali haiwezi kufanya biashara. Ijitoe kabisa katika sehemu yoyote ile, hata kama ni eneo la huduma mhimu kwa wananchi.

Hapa Azm shaona fursa ya faida, na anatumia kila aina ya mbinu kuonyesha kwamba serikali haiwezi kufanya biashara; hata kama ni kwa njia za uhujumu wa kazi inazozifanya serikali.

Sasa mimi ningefurahi akajitokeza mtu kama Roat hivi, au Mo, na wao wakasema wanaitaka kazi hiyo ya kuwahudumia wanaKigamboni.
Nadhani hilo lingekuwa ni jambo jema sana.
 
Na tiketi zao za kuchapisha
 
Very true
 
Wanalipwa kila trip Suma anaandika kikijaa full anaandika 250+ anaandika departing time na arriving time
Btw na mimi nilijua sheikh azam katoa msaada mpaka nlipokuja kujua kumbe wanahesabu na wao
Ni aina mpya ya kuwalaza akili waTanzania.

Subiri yatakayotokea TPA, baada ya TICTS; hivyo hivyo na sehemu nyingi mbalimbali nchini; hata kwenye siasa ni hivyo hivyo. Using new approach in doing the looting while achieving the same results.
 
Niliwaambia watu wapumbavu walio jazana jf na kwenye chama cha mabuzi wakapinga na kutukana
 
Niliwaambia watu wapumbavu walio jazana jf na kwenye chama cha mabuzi wakapinga na kutukana

Hata mimi ninashangaa watu humu JF wanaotetea mambo ya upigaji na ufisadi serikalini.

Azam amepewa hii tenda kinyemela, kimyakimya na kuna dalili za 10% za wakubwa katika hii huduma wanayotoa.

Ukifika pale Feri na Kigamboni, utaiona hujuma ya wazi ambayo vivuko vya serikali vinafanyiwa ili Vivuko vya Azam vipige kazi.

Yaani, Vivuko vya serikali vinakalishwa muda mrefu bila kuondoka, ili vya Azam vipige trip nyinginyingi maana abiria wanahaulishwa kwenye vivuko vya AZAM.

Kwa kuwa wenye magari hawana namna isipokuwa kuvuka kwa kutumia vivuko vya serikali basi wanapotezewa muda sana maana vivuko vya serikali vinakalishwa mno.

Pale feri kipindi kuna vivuko vya serikali peke yake hakukuwa na kuchelewa kuvuka, ulikuwa ukifika unakaa dakika chache tu za kusubiri. Kulikuwa na vivuko vikubwa viwili, vya Mv Kigamboni na MV Magogoni. Na vyote vilikuwa vinapiga kazi simulteneously, Kila kimoja kikienda upande mmoja kinakuta abiria wa kutosha wameshakusanyika, hakikai sana. Lakini leo vinasubirishwa ili Azam abebe abiria waliokusanyika huku vyenyewe vikikaa sana.

Hapa cha kujiuliza Azam analipwa sh ngapi kila tripu?

Tenda ilitangazwa lini?

Au wanamlipa kinyemela mzee Bakhressa aliwapa nini?

Kwa sasa uhitaji wa vivuko vya AZAM unatokana na nini wakati vivuko vya serikali vipo na vinafanya kazi vizuri?
 
Hajui huyu...
Huu ndio ujinga unaotumiwa vizuri sana na hawa wahujumu wa nchi.
Hapa mjinga kama wewe huoni hujuma inayofanywa kwa maksudi kabisa juu ya hivyo vyombo vya serikali ili vionekane haviwezi kufanya kazi kwa ufanisi..., halafu mtu mjinga kama wewe na huyo mwenzako mnashangilia nchi yenu kuhujumiwa!

Kuna kitu gani cha kipekee sana kinachofanywa na hivyo viboti vya Azam, ambacho serikali haiwezi kukifanya?
Watu wanahujumu juhudi za nchi, halafu wapumbavu fulani hapa wanashangilia!
Hovyo kabisa.
 
Sawa
 
Umegundua leo!nchi hii kila Kona ni upigaji tu
 
Mv magogoni na vyezake haviko salama mtakuja zama mkakumbuka mwaka 1985 baada ya kivuko kuzama na kuua woooote
 
Panda kile kivuko unachoona kiko salama.kwani ni lazima kupanda ya Azamu
 
Hujaelewa nini? Amesema kuwa kuna hujuma ya kufifisha vivuko vya umma na kuachia Azam achume kilaini. Hili jambo linaweza kuwa na ukweli ndani yake kwani hii serikali ya sasa kila mtu anashindana kupiga deal.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…