Mimi nliyokuwa chekechea nlikuwaga nnasukwa nywele , watu wananisifia nimependeza, nlivyotaka kuingia la kwanza ikabidi ninyolewe kwa sababu shule niliyoingia darasa la kwanza ilikuwa ikikataza kusuka.
Nakumbuka wenzangu walikuwa kila wakiniona wananicheka so nikawa Nina hasira Sana, nikapanga kulipiza kisasi kwa mtoto mwenye nywele yeyote nifanye njama ya kumuharibu nywele zake.
Sasa siku moja akaja mgeni , alikuja na katoto ka kike kadogodogo Ila hakajui kuongea vizuri kamebanwa nywele zake vizuri kichwani kamewekewa vidolidoli watu wanamsifia.
Wivu ukaniingia nikaamua kwenda kwa mangi nikanunua big G nikaitafuna vizuri afu nikakadanganya katoto twende tukacheze, tulipokuwa tukicheza nilikasokomeza Ile big G kwenye nywele zake, zikajifungafunga, mama yake Yule mtoto alisikitika sana. Ikabidi wampunyue pale kichwani penye big G. Mm nikasema Yan hata sijui hii big G kaitoa wapi.
Na hawakujua km Ni mm.
Sent from my Infinix X655C using
JamiiForums mobile app