Vituko vya migambo wa jiji la Arusha

EMMANUEL JASIRI

Senior Member
Feb 2, 2015
127
62
Siku moja Kaka mmoja wa kimasai ,katika harakati zake za kutembeza mikanda ili kuiuza,

Alikutana na mteja, akawa akimwonyesha hiyo mikanda bila kuweka chini bidhaa zake,

Akaja mgambo akamkamata,

Kijana akahoji kosa lake ni nini?

Mgambo aka endelea kung'ang'ania zile bidhaa bila maelezo maalum

Mpaka walipo tokea wasamaria wema na kumtetea yule kijana,maana alikuwa anatembeza tu,ndipo mgambo aka achia.

Kuna mtindo wa migambo wa hapa Arusha,wanawakamata machinga wanao tembeza bidhaa

Kama sija sahau,

Agizo ni kuwatoa machinga barabarani waliko panga bidhaa,

Lakini huku Arusha hata baadhi ya wamachinga ambao wanazitembeza bidhaa zao wanakamatwa,

Nakumbuka wanawake wawili walikamatwa na migambo,wakiwa wamebeba kichwani soksi na kuwa za ndani kwa ajili ya kuziuza,

Swali ninalojiuliza ni,

Ikiwa watu wameondoa biashara barabarani ,inakuwaje wakamatwe wakati wamezibeba kichwani?

Lakini pia mara kadhaa,

Baadhi ya Migambo wa Arusha wamekuwa wakikamata baadhi ya spika za vijana wa matangazo ya tigo,vodacom,airtel;halotel n.k

Wakisha kamata ,wana bembelezwa na kupewa chochote na kuwarudishia vijana hawa spika hizo.
sijui kama pia wametumwa kuifanya hii kazi ya kukamata spika au wao ndio wamejiongeza kufanya hivyo.

Ninaomba mamlaka husika fanyeni uchunguzi wenu na njia sahihi ili kuyafanya mazingira ya Arusha kuwa safi,

Bila kuwa bughudhi wananchi wenzetu.
 
Migambo ni Lasaba na Form 4 failure sasa mtu aliefeli lasaba ambae kashindwa kumuelewa mwalim 1+1=2 unafkr uku mtaani ataelewa Raia kwamba hii ni SAWA na hii SIO SAWA?? Wao wanachojua ni logic ya Ubabe tu ili wakikaa kambini wawe wanasimuliana ubabe walioufanya kitaani
 
Hawana huruma kabisa waliwavunjia Vijana wa watu mtaani cd zao na speaker computer,laptop wakabeba ilinisikitisha sana wale Vijana ndio walikua wamemaliza chuo wakaamua wajiajir
 
Siku moja Kaka mmoja wa kimasai ,katika harakati zake za kutembeza mikanda ili kuiuza,

Alikutana na mteja, akawa akimwonyesha hiyo mikanda bila kuweka chini bidhaa zake,

Akaja mgambo akamkamata,

Kijana akahoji kosa lake ni nini?

Mgambo aka endelea kung'ang'ania zile bidhaa bila maelezo maalum

Mpaka walipo tokea wasamaria wema na kumtetea yule kijana,maana alikuwa anatembeza tu,ndipo mgambo aka achia.

Kuna mtindo wa migambo wa hapa Arusha,wanawakamata machinga wanao tembeza bidhaa

Kama sija sahau,

Agizo ni kuwatoa machinga barabarani waliko panga bidhaa,

Lakini huku Arusha hata baadhi ya wamachinga ambao wanazitembeza bidhaa zao wanakamatwa,

Nakumbuka wanawake wawili walikamatwa na migambo,wakiwa wamebeba kichwani soksi na kuwa za ndani kwa ajili ya kuziuza,

Swali ninalojiuliza ni,

Ikiwa watu wameondoa biashara barabarani ,inakuwaje wakamatwe wakati wamezibeba kichwani?

Lakini pia mara kadhaa,

Baadhi ya Migambo wa Arusha wamekuwa wakikamata baadhi ya spika za vijana wa matangazo ya tigo,vodacom,airtel;halotel n.k

Wakisha kamata ,wana bembelezwa na kupewa chochote na kuwarudishia vijana hawa spika hizo.
sijui kama pia wametumwa kuifanya hii kazi ya kukamata spika au wao ndio wamejiongeza kufanya hivyo.

Ninaomba mamlaka husika fanyeni uchunguzi wenu na njia sahihi ili kuyafanya mazingira ya Arusha kuwa safi,

Bila kuwa bughudhi wananchi wenzetu.
Inatakiwa wawekewe mtego aadabishwe mmoja kwa kipigo cha haja, ila ionekane amepigwa na watu wenye hasira kali, bila kuacha kizibiti
 
Back
Top Bottom