Vituko vya gairo : Akimbia na funguo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vituko vya gairo : Akimbia na funguo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kwame Nkrumah, Oct 7, 2011.

 1. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  • David Jairo aondoka na funguo za ofisi
  • Wengine wahoji miaka 20 ni ya dharura gani?
  • Vigogo wahaha Symbion ipewe mkataba wa miaka 20


  HUKU Bunge likichunguza madai ya kuwapo fedha zilizogawiwa kwa Wabunge kutoka Wizara ya Nishati na Madini, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayehusishwa na sakata hilo, David Jairo, ameifunga ofisi aliyokuwa akitumia na anayekaimu nafasi yake anatumia moja ya ofisi za makamishina, imefahamka.
  Habari zilizothibitishwa na maofisa wa Wizara ya Nishati na Madini, zimeeleza kwamba ofisi hiyo kwa sasa haitumiwi na Kaimu Katibu Mkuu, Eliakim Chacha Maswi kwa maelezo kwamba bado ina vitu vya Jairo.
  Maswi anatumia ofisi za aliyekuwa Kamishna wa Madini Dk. Peter Kafumu, ambaye sasa ni Mbunge wa Igunga aliyeshinda uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo, Jumapili iliyopita.
  Raia Mwema lilipofika katika ofisi za Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Jengo la Tanesco, mtaa wa Samora, Dar es Salaam ghorofa ya tano lilimkuta katibu muhtasi, huku ikionekana kwamba ofisi za Katibu Mkuu zimefungwa na katibu huyo akaelekeza kwamba Kaimu Katibu Mkuu anapatikana ghorofa ya nne.

  Mwandishi wa Raia Mwema alipofika ghorofa ya nne kwa Kaimu Katibu Mkuu Maswi, alimkuta akiwa katika ofisi za ‘Kafumu’, lakini akakataa kuzungumzia sababu za yeye kufanyia kazi katika ofisi hizo akidai haoni tatizo lolote kwa vile anapata ushirikiano wote anaohitaji katika utendaji wake wa kazi za kila siku tokea apangiwe kazi katika wizara hiyo.
  “Mimi sina la kusema kwa kuwa nimepangiwa hapa na nilipofika nimepewa hii ofisi ambayo kama unavyoiona inanitosha na naendelea na kazi zangu kama kawaida,” alisema Maswi kwa ufupi.
  Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara ya Nishati na Madini, Theresia Mghanga aliliambia Raia Mwema wiki hii kwamba, katika ofisi za Katibu Mkuu kuna vitu vya Jairo ambavyo hakuna mtu anayeweza kuvivuruga kwa maelezo kwamba kwa sasa Jairo yuko likizo na bado ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo.
  Mghanga alipoulizwa kwanini ofisi za Katibu Mkuu zimefungwa na Kaimu Katibu Mkuu anatumia ofisi nyingine, alisema; “Kwani ulielekezwa wapi na walinzi? Kama walikuelekeza ghorofa ya tano walikosea. Kaimu yuko ghorofa ya nne, ndipo anapopatikana. Kule (Kwa Katibu Mkuu) kuna vitu vya watu ambavyo vimekaa vibaya na mwenyewe yuko likizo.”
  Alipoelezwa kwamba hiyo ni ofisi ya umma na inatakiwa kutumiwa na yeyote na kwamba kuna taarifa kwamba Jairo ameondoka na funguo, alisema; “nani kakwambia…. Kwanza hayo mambo yana faida gani? Sisi tuna utaratibu wetu wa kufanya kazi.”
  Mtumishi mmoja wa Wizara ya Nishati na Madini, ambaye amekuwapo katika wizara hiyo kwa zaidi ya miaka 15, ameliambia Raia Mwema wiki hii kwamba ilipata kutokea katika ofisi za wizara hiyo za zamani zilizokuwa Mtaa wa Mkwepu, ofisa mmoja kugomea kutoa funguo za ofisi kabla ya uongozi wa juu wa wizara kuamuru kuvunjwa kwa mlango.
  “Nakumbuka tulipokuwa Mkwepu kuna ofisa aligoma kutoa ufunguo wa ofisi na nina wasiwasi alikuwa ni Jairo wakati huo, kabla ya aliyekuwa Katibu Mkuu, Patrick Rutabanzibwa kuamuru mlango uvunjwe na kitasa kibadilishwe ili ofisa anayehamia aweze kufanya kazi. Nadhani kama kweli mtu hayupo aachie ofisi za Serikali,” alisema mtumishi huyo ambaye ni wa ngazi ya chini.  Raia Mwema
   
 2. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Rekebisha title basi. Gairo ni mji mdogo katikati ya Dodoma na Morogoro.
   
 3. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Serikali ya kishkaji, inaongozwa kishkaji.
   
 4. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,509
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Serikali legelege na fisadi haiwezi kusaidia wananchi wake kuondoa kero za maendeleo
   
 5. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Red and bolded: nyani halioni kundule, mweeee!
   
 6. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kuna vitu vyake au kuna mafaili kavundika?
  kama kulikuwa na faili kwenye hiyo ofisi linapaswa kushughulikiwa litamsubiri Jairo akifurahi na kutoa ufunguo
  harafu baadaye tunatafuta sababu kwa nini hatuna umeme
   
 7. Binti Magufuli

  Binti Magufuli JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 7,458
  Likes Received: 758
  Trophy Points: 280

  katika development discourse tuna kero za umasikini lakini hakuna kero za maendeleo
   
Loading...