Vituko na vimbwanga kwenye vikao vya ndoa

Vituko na vimbwanga kwenye vikao vya ndoa

Chief Wingia

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2013
Posts
2,863
Reaction score
5,095
Habari zenu wakuu

Aisee ipo hivi kuna jirani hapa mtaani ana kijana wake anatarajia kuoa mwaka huu hivyo nikapewa mwaliko wa kikao cha kwanza cha harusi ambayo ilikuwa ni weekend.

Ila tokea nilipopata mwaliko nikawa nawaza why kikao kikafanyike mahala pagharama hivi wakati kuna sehemu za kawaida tu au hata nyumbani kwa huyu jirani tungefanya kikao.

Aaah! Ila nikapuuza na wala sikumuhoji muhusika zaidi ya kuitikia wito na siku ilipofika nikaenda kwenye kikao hivyo tuliowahi tukakaa kidogo kusubiri watu wengine then kikao kikaanza.

Nilianza kuona utofauti walipotaja budget ya ndoa ni 30.4M na kisha ahadi ya muoaji ni 1M na ahadi ya wazazi wa muoaji ni 2M, kimoyomoyo nikajisemea hivi hawa kenge jangwa ni timamu kweli wanategemea 27.4M watazipata kwa kuchangiwa.

Pledges zilipoanza kila mtu akatoa ahadi yake pale hadi tunafunga kikao ahadi ni 10M kwahiyo kuna loss ya 20.4M na ukumbuke kuna walioahidi ila hawatakupa mchango.

Nawasilisha.
 
Ni ujinga kutaka kuoa hapaf ukategemea michango angejipanga mwenyewe tu kama hawezi gharama simpo angeoa bila tarumbeta yaani kama ni mwislam ni shekhe mashahidi wa pande zote mbili na watu wawili watatu simpoo ukitoka hapo tayari mu mke na mume halali wa ndoa!!
 
Habari zenu wakuu
Aisee ipo hivi kuna jirani hapa mtaani anakijana wake anatarajia kuoa mwaka huu hivyo nikapewa mwaliko wa kikao cha kwanza cha harusi ambayo ilikua ni weekend.

Ila tokea nilipopata mwaliko nikawa nawaza why kikao kikafanyike mahala pagharama hivi wakati kuna sehemu za kawaida tu au hata nyumbani kwa huyu jirani tungefanya kikao.

Aaah..! Ila nikapuuza na wala sikumuhoji muhusika zaidi ya kuitikia wito na siku ilipofika nikaenda kwenye kikao hivyo tulio wahi tukakaa kidogo kusubiri watu wengine then kikao kikaanza.

Nilianza kuona utofauti walipotaja budget ya ndoa ni 30.4M na kisha ahadi ya muoaji ni 1M na ahadi ya wazazi wa muoaji ni 2M, kimoyomoyo nikajisemea hivi hawa kenge jangwa ni timamu kweli wanategemea 27.4M watazipata kwa kuchangiwa.

Pledges zilipo anza kila mtu akatoa ahadi yake pale hadi tunafunga kikao ahadi ni 10M kwahiyo kuna loss ya 20.4M na ukumbuke kuna walioahidi ila hawatakupa mchango.

Nawasilisha.
Mpaka tutakapoondokana na dhana ya kudhani kuwa ndoa ni public issue bali ni suala binafsi na la kimila zaidi, ndipo wengi watafunguka na kuachana na tabia ya kujitangaza wanapooa au kuolewa au kuozesha.
 
Ni ujinga kutaka kuoa hapaf ukategemea michango angejipanga mwenyewe tu kama hawezi gharama simpo angeoa bila tarumbeta yan kama ni mwislam ni shekhe mashahidi wa pande zote mbili na watu wawili watatu simpoo ukitoka hapo tayar mu mke na mume halali wa ndoa!!
Hii nzuri sana, nikitaka kioa naenda zangu zenji huko na wazazi wa binti na wangu na mashahidi kama wanavoonekana hapa pichani😀
 
Attachments

  • Screenshot_20230130-153724.png
    Screenshot_20230130-153724.png
    168.6 KB · Views: 19
Harusi zimekuwa biashara kubwa! Kadri gharama zinapokuwa kubwa ndivyo harusi inavyoonekana imefana! Mamc hulipwa mamilioni, watu wa kamera huja na gharama zao za hatari, mapambo, ukumbi, vinywaji, Bado mavazi! Kila kitu ni gharama!

Lakini vyote hivyo unaweza kuvipata kwa gharama ndogo tu ila zama hivi watu hawataki vya bei ndogo! Huenda kwenye bei kubwa hata kama huduma ni mbovu!
 
Kwny familia/ukoo wetu(upande wa mzee)
huu upuuzi wa michango ilishaukataa.

Wa kiume akioa
Ukoo mzima unagharamia mahali na harusi in simple way, Watu mnaalikwa kula,kunywa na kutoa zawad zenu na kuondoka

Wa kike akiolewa
Familia inagharamia send-off, kitchen party na zawadi
Watu wanakuja kula,kunywa,kutoa zawadi na kutawanyika

Sema ndo hivyo,
Tunaohenyeka na michango Ni sisi wanafamilia/ukoo kila Mara michango maana ukoo wetu Ni mkubwa na huwez kukwepa

Ila majirani,marafiki,Watu baki wanatoa wanavojiskia maana mwngn ukimpelekea kadi aje kula na kuondoka bure hawezi/anahisi km umemdharau
 
Kwa hiyo 1M ya kijana na 2M za wazazi zingetosha kabisa kufunga ndoa na maisha Kuendelea bila kusumbua watu. Mimi binafsi nishaacha kuchangia harusi kitambo sana kabla ya mapolisi hawajaacha kuvaa kaptula.
Hata ya wanafamilia wako uchangi?
 
Ningeomba niongee na Muweka hazina faragha wakichanga tukiamshe na mumewangu aisee😂😂😂
 
Ningeomba niongee na Muweka hazina faragha wakichanga tukiamshe na mumewangu aisee😂😂😂

Wanawake wenye akili hizo hamtongozwi na wanaume wa aina hizo.

Nyinyi mnapambana na kina sisi waunga unga maisha tu. Ambao hata harusi ya milioni 1 bado tunaipinga
 
Ni ujinga kutaka kuoa hapaf ukategemea michango angejipanga mwenyewe tu kama hawezi gharama simpo angeoa bila tarumbeta yaani kama ni mwislam ni shekhe mashahidi wa pande zote mbili na watu wawili watatu simpoo ukitoka hapo tayari mu mke na mume halali wa ndoa!!
Sisi Wakristo tuna mlolongo sana kwenye ndoa ila
Waislam wako simple mkuu nakumbuka kuna classmates wasuni chuoni hapo SUA walioana wakiwa chuoni na hadi leo wako pamoja.
 
Back
Top Bottom