Vituko mtaani kwetu!

Jaguar

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2011
Posts
3,440
Reaction score
1,029
(1)Nikiwa matembezi mtaani hapa iringa,nimekutana na bibi kizee mmoja kalewa ulanzi chakareee anatembea kwa kujishikilia ukutani huku akiimba wimbo wa Dogo Aslay;(Tena inaniumaaa sana....ooh,nikitoka naenda kumwambia mama...ooh,naenda kuseema kwa mama,kusema kwa mama) x nyingi.Sasa sijui ni kipi kilimsibu bibi kizee huyu umri wa bi kidude mpaka atishie kwenda kusema kwa mamake.
 
Reactions: Edo
Huyo bb kiboko bt ilbd umfatilie anakoenda pengine ungemwona huyo mama yake....
 
Huyo bb kiboko bt ilbd umfatilie anakoenda pengine ungemwona huyo mama yake....
Mh!kwa umri wake kama ni kumfuata mama yake ni lazima angeelekea makaburini.
 
Hahahahaaaa kweli ngoma imembamba bibi
 
Mh! hiyo lazima ni Pande za INDIUKA kuelekea Ipogoro hahahah mkuu i just love IRINGA hasa msimu huu wa KITETE aka ulanzi. miaka hiyoo nikiwa pande za mitaa ya Nyamhanga kule karibu na Secondary ya Cagliero daaaah tulikuwa tunaoga kwenye VITINDI mwana hahahahahaha. siku nyingine tunaufuata mtogwa njia panda ya TOSA
 
Kimsingi bibi alikuwa anajiburudisha na kisekondari pombe nizo zilimtuka kama ulivi wa madaraka ulivyomtu Magufuli kuropoka asiyeweza kulipa mia2 aogelee
 
Mh!kwa umri wake kama ni kumfuata mama yake ni lazima angeelekea makaburini.
hahahhahahaahah, ungeenda tu mpaka uko hafu unamwambia nakusubilie hapa nje uje na mama yako eeh.
 
Basi nikiwa nalitazama soko letu pale Tunduma likiteketea,mara namwona teja anakuja upande wangu mbio.Mkononi alikuwa na dozen moja ya vijiko alivyoiba,nikamsikia akimwambia teja mwenzie;mwanangu huu mwaka wetu,lazima tutoke,napeleka hivi vijiko gheto na nitarudi kwa ajili ya sahani za plastiki.Yaani vitu kibao vya thamani vilikuwepo kama Tv,decks,solar panels,radios n.k,lakini teja akaamua kuiba vijiko na sahani.
 
ngómbe hazeeki maini mkubwa!!!! SURA INAWEZA IKAWA CHAKAVU LAKINI BADO BURUDANI IPOOOOO
 
Songíto;3107402 said:
ngómbe hazeeki maini mkubwa!!!! SURA INAWEZA IKAWA CHAKAVU LAKINI BADO BURUDANI IPOOOOO
Mh! Burudani gani tena hiyo?
 
Bila shaka ni maeneo ya MTWIVILA kwa Mwalukosi mkuu, au Mitaa ya IDUNDA teh teh teh l Love Iringa jamani.
 

Duu.. Mateja noma
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…