VITUKO:Mkurugenzi wa Kishapu aangua kilio barazani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VITUKO:Mkurugenzi wa Kishapu aangua kilio barazani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ochu, Jan 29, 2009.

 1. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wlaya ya Kishapu, Elly Mlaki, ameangua kilio ndani ya kikao cha Baraza la madiwani wa halmashauri hiyo, baada ya kushindwa kujibu swali la mmoja wa madiwani.

  Tukio hilo lilitokea jana mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo ambamo kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Brigedia Jenerali Dokta Yohana Balele, kilifanyikia.

  Hatua ya Mkurugenzi huyo kuangua kilio, Ilikuja baada ya Diwani wa Magalata, Albert Kapongo, kumuliza swali lililohusu jinsi ofisi yake ilivyotumia Sh 120 milioni, kununulia lori la Idara ya Elimu.

  Hata hivyo mkurugenzi huyo, hakutoa maelezo ya kina kuhusu swali hilo, jambo lililomsukuma Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,kuingilia kati na kutaka ufafanuzi wa kina juu ya swali hilo.

  "Ndugu mkurugenzi naomba kupata ufafanuzi wa matumizi ya Sh120 milioni zilizotumika kununulia lori la Idara ya Elimu,"alisema.

  Akijibu swali hilo mkurugenzi huyo alidai kuwa lori hilo halijanunuliwa na kwamba fedha hizo zimetumika kwa shughuli mbalimbali ikiwemo mandalizi ya ziara mbalimbali za viongozi wa kitaifa.

  "Nataka utoe ufafanuzi wa jinsi fedha hizo zilivyotumika," ling'aka Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, hatua iliyomlazimisha mkurugenzi huyo kuendelea kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu fedha hizo.

  Alidai Sh 2 milioni katika kuwa fedha hizo zilitumika kununulia kapeti la rais na Sh 5 milioni, zilitumika kuwalipa walimu tarajali.

  Hata hivyo mkuu wa mkoa alizidi kumbana zaidi mkurugenzi kuhusu fedha ambazo kimsingi, hakizikupaswa kutumika kwa shughuli nyingine.

  "Hizo fedha zingine zilizobaki zikowapi,"aliuliza mkuu wa mkoa.

  Kufuatia kubanwa kwa maswali hayo, mkurugenzi huyo aliaanza taratibu kutoa kwikwi na baadaye kuangua kilio hadharani kwa sauti kubwa na kuwafanya madiwani kushikwa na butwaa.

  Hali hiyo ilipoendelea mkuu wa mkoa alimwomba mwenyekiti wa halmashauri hiyo kuahirisha kikao hicho kwa vile haikuwa rahisi tena kuendelea nacho wakati kuna kilio cha mkurugenzi.

  Kikao hicho kimepangwa kufanyika tena leo.
   
 2. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #2
  Jan 29, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Kama bosi wao PM alivyolialia leo. Utamaduni mpya huu....
   
 3. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huyu kichwani alikuwa anafikiri Yona, Mramba, Liumba...... Akajua sasa inafuata zamu yake kwenda kumsalimu Pilato.
   
 4. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  tehe tehe tehe bongo Bwana... Sasa ndo taifa linaanza kukua, huko nyuma tulirushwa umri. You can't fool any body that we are more than 40yrs old. Hii ni hali ya Taifa linaloanza kutambaa... ama kweli tupo nyuma!
   
 5. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2009
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Nafikiri kinachomliza huyu bwana ni kitendo cha RC na Baraza zima kumtaka ajibu juu ya matumizi ya pesa ambayo nina hakika zimetumika ndivyo sivyo kwa amri ya wakuu wake na sasa anaona mzigo unamdondokea peke yake bila huruma.
   
 6. G

  Ghwakukajha Senior Member

  #6
  Jan 29, 2009
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kama ni sababu hiyo,nadhani alisahau kuwa "there is no PATNER in a CRIME"
   
 7. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Duh! Ebwana ee! Hii kali. Bongo kuna mambo. Lakini bonge la trick hilo mtu wangu.
   
 8. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,147
  Likes Received: 1,242
  Trophy Points: 280

  Tehe! Ina maana ni uchungu, hasira, kuwa quoted vibaya au nini? Ukimwona mtu mzima aliyeshikilia mpini (yaani) dola halafu analia mbele ya walishikilia makali (Wauaji wa Albino) hapa pana utata kidogo.

  Any way niliona nikashtuka kidogo kwa muheshimiwa PM kumwaga chozi

  Kule Kishapu huyu Mkurugenzi halii tu kwa vile kakosa maelezo ila kwa sababu asilimia 75 wametafuna wakubwa na 15 yeye na treasurer wake. Pagumu hapa...ni lazima aende Mhumbu.
   
 9. L

  Lorah JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mi nahisi mkurugenzi amelia kwasababu anajua kuwa mkuu wa mkoa nae alikuwepo, aliona hivyo vimemo halafu anamkunjia ndita, halafu mhhh labda walikuwa wameshayaongea wakayamaliza masikini......
   
 10. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2009
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  There is no partner in a crime.... kwi kwi kwi, mbona Kisutu wanapandishwa wawili wawili!!
   
 11. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
   
 12. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #12
  Jan 30, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Mkuu wewe ni kiongozi tena unayekubalika, sasa utufundishe sisi wananchi wanyonge kuheshimu hisia za viongozi wengine wanoalia katika kusema machungu yao, sasa wewe kiuongozi ukisema hivi, sisi wananchi tutasema nini mkuu?

  - Wewe ni mtu mkubwa sana mkuu, jaribu kuelewa urefu wa maneno yako kwa sisi jamiii, siasa sio ugomvi wala kejeli, utu wa mtu na hasa kiongozi huonyeshwa kwa maneno kwanza baadaye ni kwa vitendo. Tutofautiane kwa hoja, lakini sio kwa kejeli taifa liko njia panda sana hili!
   
 13. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #13
  Jan 30, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kama ni kweli hii posting ni ya kwako Mh Zitto, basi ninyi viongozi ni vivuli wa hawa waliopo sasa.
  Safari yetu ya kupata serikali na viongozi mbadala is far from reality.
   
 14. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #14
  Jan 30, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...Shinyanga huko habari zake mnh, ...kila siku kuna kituko kipya toka mkoa huo...
   
 15. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #15
  Jan 30, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi mtu akiwa kiongozi asiongee vile anavyojisikia hata akiwa kwenye leisure time awe mtu wa kujifanyishafanyisha tu na kuongea kinafiki?Kwahiyo nyinyi mnataka mtu akishakuwa kiongozi basi asikohoe wala kufanya utani,saa zote awe anaongea mambo mazitomazito tu...
  Muacheni Zitto aonyeshe hisia zake za kibinadamu.Siyo bungeni hapa!!
   
 16. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #16
  Jan 30, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Huna haja ya kumtetea, kama alikuwa anafanya utani basi atarudi hapa kusema hivyo, lakini hadi sasa hatuwezi kum'bashiria mawazo yake na itabaki kuwa kama tulivyotundika.
   
 17. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #17
  Jan 30, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Hii si kwa Zitto tu ni kwa viongozi wote.Mnapojadili kauli zao hasa zile ambazo siyo rasmi basi muwe mnaangalia na upande wa pili kuwa wao ni binadamu kama wewe.Sasa mtu unakutana nae restaurant akaongea ka joke tu basi isiwe nongwa kwavile yeye ni kiongozi.
   
Loading...