Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

71073a8747c355ea95594bbb057a57f2.jpg
 
HUYU HAPA MWANAUME WA MIAKA 71 ALIYEAMUA KUJITENGA NA WANAWAKE BAADA YA KUBALEHE.

Anaitwa Calixte Nzamwita( 71), Mwanaume ambaye aliamua kukaa peke yake kwenye nyumba yake ndogo kwasababu aliamini kuwa hatakiwi kuzungumza na wanawake. Akiwa na umri wa miaka 71 hivi sasa hadithi yake ni kuhusu kuwa peke yake, inasemekana kuwa mzee huyo alifanya uamuzi huo akiwa na umri wa miaka 16 pekee na hajawahi kuruhusu mwanamke yeyote kuingia nyumbani kwake.

Anaamini kwamba hapaswi kuzungumza na wanawake na hii ni kwasababu yeye ni masikini, Kisayansi huu ni uoga ukiokithiri, mwanaume huyo alinukuliwa akisema

"Ninajifungia humu ndani na nina uzio kuzunguka nyumba yangu ili kuhakikisha wanawake hawatanikaribia, sitaki wanawake karibu nami kwasababu wananitia hofu"- alisema

Moja kati ya wanawake ambao humhudumia Calixte Nzamwita alisema humsaidia kwa chakula licha ya kutotaka ukaribu nae, mwanamke huyo alisema tangu amfahamu mwanaume huyo ni mda mrefu kidogo na amekuwa akijifungia ndani muda wote kwasababu anaogopa kuchangamana na wanawake

"Cha ajabu ni kwamba japo anaogopa wanawake sisi ndio tunamsaidia kupata chakula na baadhi ya vitu anavyohitaji na ukijaribu kumsaidia hataki umkaribie wala kuongea nae badala yake tunampa tu. Vitu huvitupa ndani ya nyumba yake tunakuja kuvichukua baadae kama sahani aliyotumia kula chakula lakini bado tunajitahidi kumsaidia"- alisema

Credit; Afrimax
FB_IMG_1692712529239.jpg
 
Back
Top Bottom