"Mkome kama mlivyokoma kunyonya maziwa ya mama zenu"- RC Chalamila
"Mliowafukuza watumishi wangu mkome kama mlivyokoma kunyonya maziwa ya mama zenu, msije mkanichokonoa nikafunga soko hili, haiwezekani Watumishi wa Serikali wanakuja hapa Mpumbavu mmoja anasimama kuzuia watu nyie mna akili sawa? unamtishia DC wewe una adabu wewe?"
"DC anakuja hapa na watu wake kinajiinua kijitu kimoja kwa maslahi yake unaanza kumzuia DC, nitakufyatua na utasahaulika, nimeambiwa kuna watu wanataka kunizomea, zomeeni halafu mtaona nimekujaje na kuanzia leo nimevunja uongizi wa soko hili"- RC Chalamila alipotembelea soko la Mabibo mapema leo jijini Dar es salaam.