Vituko mitandaoni. Tupia chako

Ila nyie CCM na mkiti wenu @SuluhuSamia mmetudharau na mmeonyesha KIBURI!
Kesi imepelekwa mahakamani kuwa mmekiuka sheria - sasa mmekimbiza bungeni muswada kubadili sheria

MABADILIKO
Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Mali na Rasilimali Asilia, Sura ya 449 - Mmefuta ibara ndogo ya 2 na kupendekeza
MASHARTI YA SHERIA ISITUMIKE iwapo
a. Itahusu usafirishaji wa rasili mali zilizochimbwa nje ya Tanzania
MY TAKE: mnataka kuwapa DPW LOGISTICS pia upendeleo wa usafirishaji kwenda DRC huko kuleta madini na mengine
b. Uendelezaji, uendeshaji au uandaaji wa mipango ya kuendeleza maliasili na rasilimali kwa lengo la kuboresha utendaji wa bahari, kavu na kavu Bandari za ziwa katika Jamhuri ya Muungano
MY TAKE: hiyo maliasili ina maana mtawapa na mikataba ya kuchimba gesi, mafuta, madini na watazisafirisha wanakotaka kwa kutumia bandari zetu bila sisi kuwa na usemi

Mmefanya mabadiliko haya kwa Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusu Utajiri na Maliasilia za Nchi (Mapitio ya
Mikataba na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi) pia

HUU NI USALITI WA NCHI! Ni hivyo tu in short!
Alafu mnajiita wazalendo?
Tusipowasimamisha TUMEKWISHA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
DALALI @zittokabwe amekuwa DALALI wa DP WORLD..

Ukiuza kiwanja chako mnunuzi atakuwa hajanunua kwa kuwa hawezi kubeba na kuhamisha kiwanja? Kwamba, atapeleka wapi kiwanja? Hii ni akili timamu?

Nasikitika kuona DALALI ana wafuasi wanamuita “mheshimiwa kiongozi wa chama”.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…