Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

Hosea 4:6
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe,usiwe kuhani kwangu mimi;kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako,mimi nami nitawasahau watoto wako.

Mathayo Mtakatifu 24:3 Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa ?Nayo ni nini dalili ya kuja kwako,na ya mwisho wa dunia?
4.Yesu akajibu ,akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye. 5 Kwasababu wengi watakuja kwa jina langu ,wakisema, Mimi ni Kristo ;nao watadanganya wengi.6 Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita;angalieni,msitishwe;maana hayo hayana budi kutukia;lakini ule mwisho bado.

7.Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme;kutakuwa na njaa, matetemeko ya nchi mahali na mahali.

8.Hayo yote ndio mwanzo wa utungu.

9.Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua;nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.

10.Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana na kuchukiana.

11.Na manabii wengi wa uongo watatokea na kuwadanganya wengi.

12.Na kwasababu ya kuongezeka maasi ,upendo wa wengi utapoa.

13.Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho ,ndiye atakayeokoka.

14.Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote;hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.

23.Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama ,Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki.

24.Kwa maana watatokea makristo wa uongo ,na manabii wa uongo ,nao watatoa ishara kubwa na maajabu;wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.

25.Tazama nimekwisha kuwaonya mbele.

26.Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke;yumo nyumbani, msisadiki.

27.Kwa maana kama vile umeme utokavyo Mashariki ukaonekana hata Magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu .

28.Kwa kuwa popote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai.

Mkuu wangu; haya tunayoyaona hayana budi kutokea ili kutimiza unabii, na yatakuja mengi sana ya kustaajabisha na kushangaza kuliko ambayo tumeshayaona cha msingi ni kuwa makini na matukio yote yanayohusiana na mambo ya imani hasa za kiroho.

(Mara fungeni mfe ili mwende mbinguni, mara yupo kutokea India anatembea juu ya maji n.k ,tetesi za vita, matetemeko ndio hizi hizi ishara)
Asante Mtumishi

Tulishaonywa.

Kila mtu na ashike sana alichonacho.

Mungu na Atusaidie 🙏🏿🙏🏿🙏🏿
 
FB_IMG_1685972878805.jpg
 
Back
Top Bottom