Dunia Sasa hivi imekuwa ngumu Sana.
Kiasi kwamba watu wanajali maiti zaidi kuliko aliyepo hai.



Kuna jamaa tulikuwa tunamtibu hapa alivunjika.
Ametibiwa amepaona lakini ndugu walikuwa hawaji kumuona Wala kulipa madeni.
Pigiwa simu hawaji.
Deni limeongezeka mpka kulipika ni shida.
Jamaa akamuambia daktari, wapigie simu ndugu zangu waambie nimekufa.
Waje wachukue maiti.
Simu ikapigwa.
Ndugu wamepokea.
He, amekufa!!?





Basi tunakuja baba!!
Baada ya siku 2 wamekuja na jeneza na gari wamekodi.
Kwenda wodini wakapewa faili.
Kalipieni madeni tuwape kibali mkachukue mwili wa marehemu.
Wakaenda uhasibu wakalipa madeni.
Wamerudi wodini na risiti wakamkuta jamaa amekaa kwenye benchi anawasubiri.!!
Wakaangua kilio Tena.







Jamaa likawaambia, si mlitaka nifie huku huku.
Nimefufuka Sasa.
Twendeni nyumbani Sasa tukamalizane huko huko.!!!








