Mimi nadhani ni mgonjwa wa akili. Labda ndiyo masharti aliyopewa na hao waliompa hizo nguvu anazotumia kulaghai watu.
Kabla serikali haijamshtukia mara ya kwanza alikuwa na wafuasi wengi. Akipita lazima wafuasi wake wajipange huku na huku wakimsujudia na inasemekana alikuwa/ana uwezo wa kutenda miujiza (kuponya wagonjwa na kufungulia wenye matatizo). Watu wanasafiri kutoka huko walikotoka na kwenda kukaa kwake. Ndiyo maana kwenye hii kesi ya mwisho serikali ilimshikilia kwa kosa la human trafficking.
Jamii yetu hii ina matatizo makubwa na ukijifanya unatenda vimiujiza basi utapata wafuasi kweli kweli.
View attachment 2554731View attachment 2554732