Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

322011609_733368061228059_7894741302856135852_n.jpg
 
NI MAMA AU NI MAMA YAKO?

Salum alimtumia meseji mke wake; “Samahani mke wangu sitaweza kuja kukuchukua, nipo Hospitalini hapa Mama amelazwa kapungukiwa damu ndiyo nahangaikia watu wa kumuongezea”

Mkewe akajibu; Kwahiyo Mama yako ndiyo umemuona wa muhimu sana kuliko mimi, yaani mimi nipande Bajaji kisa Mama yako anaumwa, si umuache uje unichukue, unakaa huko kwani wewe Daktari!

Gari yangu mwenyewe kisha unisumbue sababu ya Mama yako! Umesikia gari ya wagonjwa hiyo, ungetaka kumhudumia Mama yako si ungenunua ya kwako!”

Salum alimuuliza’; Kwahiyo ni muache Mama hapa nije kukuchukua?” Mkewe alimjibu, ndiyo kwani ukimuacha atakufa! Si ushasema yuko hospitalini! Si kuna madaktari huko!

Nitaendaje kwenye sherehe peke yangu kama vile sina mume!” Salum alikata simu na baada ya kama nusu saa hivi alikua nyumbani tayari kumchukua mkewe, kwahasira mke alipanda kwenye gari, walienda mpaka kwenye sherehe.

Sherehe ilianza, huku mke akinywa kwa hasira hakutaka hata kuongea na mumewe.

Salum alikaa kimya akiwa na mawazo mengi kila mara akishikilia simu yake. Katika kipindi chote hicho mkewe hakumuuliza hata hali ya Mama.

Sherehe iliisha wote wakaingia kwenye gari kurudi nyumbani. Walilala mpaka asubuhi mkewe akiwa hajamuulizia chochote.

Asubuhi wakati wanaamka simu ya mwanamke ikatoa mlio Wa Meseji, ujumbe ulitumwa kutoka kwa Mdogo wake Wa tumbo moja ukasomeka hivi:

"Dada! mama amelazwa hospitali tangu Jana, tulimuona tu shemeji we we ulikua wapi?"

Ghafla uso ukabadilika akamgeukia Mume wake na kumuuliza "kumbe anaeumwa ni mama yangu! Mbona hukuniambia??

Salumu akajibu:

"Jamani jana si nilikuambia anaumwa hali mbaya kalazwa hospitalini?”
*“Uliniambia lakini hukuniambia kama ni Mama yangu”

"Jamani mke wangu sisi ni mwili mmoja, sasa niliposema Mama nilikua na haja gani ya kusema Mama yangu au wako, kwamaana ninavyojua Mama yangu Mama yako na Mama yako ni Mama Yangu.

Huku akilia. “Sasa ndiyo ukamuacha Mama hospitalini, kwani kapatwa na nini? Yaani unanaicha na sherehekea kumbe Mama yangu anaumwa!”

"Alipata ajali ya gari jana, akapoteza damu nyingi, sasa hospitalini kulikua hakuna damu ndiyo nikawa natafuta watu wa kumuongezea, sema uliposema niache kuhangaika naye ndiyo nikaacha sasa sijui hali yake inaendeleaje maana alizidiwa sana".

Huku akilia mkewe aliingia kwenye gari kwa kasi akimtaka mumewe aendeshe gari kwa haraka, Salum aliendesha gari taratibu akipitia ofisini kwao kusaini, mkewe alilalamika kwamba wanachelewa.

Kwa namna alivyokuwa amechanganyikiwa mkewe alishindwa hata kuendesha gari hivyo ilibidi amsubiri mumewe waondoke wote. Njia nzima mkewe alikua akilia.

Mkewe alijua Mama yake alishakufa kwa kukosa damu kwani kwa hali aliyoelezewa alijua kuwa hawezi pona. Alifika na kuwakuta ndugu zake wako nje, aliwasalimia na kuwauliza hali ya Mama walimuambia aingie kumuona.

Alizidi kuchanganyikiwa akijua Mama yake kashafariki.

Alifika na kumkuta Mama yake mzima, alimsalimia na kumuomba msamaha kwa kuchelewa kuja kumuona akisema alikua hajui, Mama yake alimuuliza kwa mshangao.

“Ulikua hujui wakati Mumeo jana alikuwa hapa, Baba wa watu kahangaika sana mpaka kupata watu wa kuniongezea damu, kasumbuka sana jana, mwanangu hapa umepata mume. Asingekua mumeo ningeshakufa kwani madakitari walisema ningekosa damu ningekufa…”

Mke wa Salum alishindwa cha kujibu, hakujua kuwa kumbe Salum hakuacha kutafuta damu alihakikisha Mama yuko salama ndiyo akaondoka.

"Sikumwambia Mama, Jana alikua anajisikia vibaya, nadhani presha ilikua inamsumbua, nikasema nisimwambie kwani angeweza kuchanganyikiwa. Asubuhi ndiyo nikamuambia baada ya kuona yuko vizuri”

"Naendela vizuri mwanangu, ahsante sana kwa kuhangaika na mimi jana, nilikua hoi sana". Mama yake aliongea huku akitabasamu. Mkewe alinyanyuka, huku akitoa machozi alimkumbatia mumewe na kumwambia: "nisamehe mume wangu sasa ndiyo nimejua maana ya ndoa"

Salum alimkumbatia mkewe kwa nguvu na kumwambia.

"Usijali mke wangu nakupenda sana nilitaka tu ujifunze kuwa mali sio kila kitu, najua umenizidi kipato lakini pesa
zinatafutwa na kamwe hela haiwezi kuzidi thamani ya UTU"

JIFUNZE KISHA Funza wengine
 
Back
Top Bottom