Semina ya wanandoa
Kulikuwa na semina ya wanawake kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika ndoa zao...
Mwalimu aliwauliza ni wangapi wanawapenda waume zao.
Wote wakanyoosha mikono kama ishara ya kuwa wanawapenda waume zao.
Mwalimu akauliza tena, “Ni lini mara ya mwisho ulimwambia mumeo “
Nakupenda Mpenzi”?
Majibu yalikuwa kama ifuatavyo:
Baadhi walisema Asubuhi ya leo,
Wengine jana,
Wengine wiki iliyopita
Wengine mwezi uliopita
Na wengine wakasema hawakumbuki!
Mwalimu aliwapa kazi kila mwanasemina achukue simu yake na kumtumia mume wake meseji yenye neno “NAKUPENDA MPENZI”
Baada ya meseji kwenda aliwaamuru kubadilishana simu kila mmoja na jirani yake.
Kila mwanasemina aliambiwa kusoma meseji za majibu kwenye simu aliyoshika
Simu ya 1 – “Samahani, nani mwenzangu”!
Simu ya 2 – “Samahani, wrong number”!
Simu ya 3 – “Wee, Si nimekuambia usinitumie messages kwenye namba hii”! Usirudie. Wife anashikaga hii simu.
Simu ya 4 – “Mmmhh.. makubwa! Leo mvua itanyesha”!
Simu ya 5 – “Nikija tutaongea zaidi”!
Simu ya 6 – “……Imethibitishwa: Umepokea Tsh300,000 kutoka kwa ……”!
Simu ya 7 – “Me too”!
Simu ya 6 – “Duuh! Inaelekea huu ujumbe ulikuwa unamtumia hawara yako, leo nikija utanikoma”!