Mwanaume kupatwa...
Marafiki wawili
(Jose na Ben) walikuwa wanatembea mtaani akatokea mwanamke akarusha busu kwa mmojawapo kupitia dirishani katika jengo la ghorofa tatu.
Wakaanza kujadiliana kama ifuatavyo:
Ben: Muone yule mrembo amenirushia busu
Jose: tafadhali achana na huyo mwanamke, usimjali..
(baadae yule mwanamke akamuashiria aende)
Ben: yule mwanamke ameniita!
Jose: Rafiki yangu, usiende tafadhali
Ben: Kwa nini unaniambia nisiende wakati mrembo kama yule ananiita? Huu wivu sasa.
Jose: Ben, Nakwambia, tafadhali usiende
(Ben alienda. Ghafla wakiwa wanataka kuanza mambo, wakasikia mlio wa gari getini)..
Lady: (akiangalia kupitia dirishani)
Oooh dear! Yule ni mume wangu karudi!!
Ben: Mama yangu nafwaaa!
Tufanyeje sasa?
Lady: Usiwe na khofu, jifanye we Dobi na anza kupiga pasi hizo nguo hapo
(akimuonyesha lundo kubwa sana la nguo)
(Ben alitumia masaa matano kukamilisha kazi ya kunyoosha zile nguo kwa sababu yule mume hakutoka tena siku ile)
(Siku iliyofuatia Ben alikwenda kwa Rafiki yake)
Ben: Kaka, unaweza kuamini Jana nimepiga pasi nguo kwa masaa matano pale kwa yule mrembo??!!!
Jose: Lakini nilikwambia usiende ukakaidi..
Amini usiamini, nguo zote hizo ulizonyoosha,
Nilizifua Mimi Juzi🙄
When an experienced person speaks, you better listen!