Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

Unakumbuka Sheria za mpira za utotoni?​

1.Mwenye mpira Lazima acheze hata kama hajui mpira
2.Dogo mnene Lazima awe golikipa
3.Mwenye mpira ataamua nani acheze na nani asicheze
4.kama haujashiriki kufuma mpira unaweza usipate namba
5.Ukichaguliwa mwishon ujue uwezo wako ni mdogo kuliko wote
6.Mwenye mpira akikasirika mpira umeisha, maana anauchukua na kusepa kimyakimya..
7.Inaruhusiwa kubadili golikipa kama ikitokea penat na baada ya hapo ataendelea kudaka yule yule
8.Mechi itaisha pale giza linapoingia
9.wale ambao wamekosa namba kazi yao ni kufuata mpira ukitoka nje
10.mtaalam wa soka huwa hakoc namba hata siku moja!
Ukiikumbuka unatabasam😁
 

Mume anaenda kazini...​

Jamaa kaamka asubuhi sana Jumamosi, mvua inarindima vikali, kang’ang’ania kuwa anaenda ofisini.
Kawasha gari yake, kufika njiani hali ikawa mbaya kaamua kurudi.

Kafika home kavua nguo kaingia tena kitandani, kamnong’oneza mkewe aliyekuwa usingizini;-
Mume: “Yaani hali ya hewa huko nje ni mbaya sana”
Mke: Si ndiyo nimemshangaa huyu mpumbavu eti kaenda kazini…🙄
 

Faini ya kukojoa..​

Polisi alimdaka jamaa anakojoa pembezoni mwa ukuta.
Polisi: Wewe unajua kusoma?
Jamaa: Ndiyo
Polisi: Hicho kibao kimeandikwaje?
Jamaa: Usikojoe wala usitupe taka hapa.. Faini 5K
Polisi: Kwa hiyo umetenda kosa makusudi?
Jamaa: Sasa nimebanwa nifanyaje?
Polisi: Faini yake elfu tano.
Jamaa akatoa noti ya elfu 10.
Polisi: Sasa chenji tunaipataje?
Jamaa: Tafuta chenji unipe changu.
Polisi: Hakuna chenji.. basi kojoa tena😁
 
IMG-20220914-WA0154.jpg


Sent from my LM-V500N using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom