Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

Screenshot_20220731-213154.png
 

Wadada​

Ticha katangaza test , Akatoa Masharti; Ukiandika jibu hamna kufuta au kukata.

1). Taja vyakula vi3 ambavyo ukienda hotelini umelipiwa utapenda kula (marks 1)

WAVULANA wakajaza
: wali, ugali, mihogo.
WADADA wakajaza: burger, pizza, egg chop.

2). Eleza jinsi ya kupika kila chakula ulichotaja hapo juu. (marks 99)
wacha wadada waanze kuhangaika kukata na kufuta majibu ya mwanzo😊🤔
 

K​

Zuzu kaniuliza, “Anko, unajua vitu vinavyoanzia na K ni vitamu sana.”
Nikashtuka, “Astaghafilulah we mtoto! Niondolee uchuro wako hapa!”

Zuzu akatabasamu. Akaendelea kuongea kabla sijafanikiwa kumzuia.. “Kweli kabisa anko. Vitu vinavyoanza na K ni vitamu sana kwa mfano kuku, kalimati, keki, kabab, katleti, kashata, kisheti, karanga, korosho na karoti.”
Nikashusha pumzi. “Ahaa! Kumbe ndo hivyo, ni kweli!”

Zuzu akanitupia swali. “Kwani we anko ulidhani nini?”
 

Askari​

Askari wametumwa nyumba iliyokuwa kuna ugomvi wakafika wakatakiwa kuripoti kwa njia ya Radio Call juu ya kinachojiri:
ASKARI: Mkuu tumekuta mama mwenye nyumba kampiga mumewe chuma cha kichwa na kumuumiza vibaya sanaa

AFANDE: Kha! kisa mkasa mpk akafanya hivyo?!!!
ASKARI: Mama mwenye nyumba alikua anapiga deki mumewe akaingia ndani na viatu kabla sakafu haijakauka.
AFANDE: Sasa mmesha mkamata huyo mwanamke?
ASKARI: Bado mkuu.
AFANDE: Kha! sasa mnangoja nini?!
ASKARI: Si tunangoja kwanza sakafu ikauke?!!!
 
ALIYETANGAZA KUWA NI SHOGA ATANGAZA KUOLEWA.

Mwaka jana zilienea taarifa za kusikitisha zilizowaacha watu vinywa wazi, ni baada ya mwanamuziki wa kundi la Sauti SOUL Chimanno kutoka Kenya kujitangaza kuwa yeye ni shoga,
Watu wengi walionyesha kukeleka na kundi la sauti soul lilipoteza mashabiki wengi sana.
Ni miezi kadhaa imepita na sasa Chimano ametangaza kuwa tayari ana mume wake ambaye yupo Ujerumani na wanampango wa kufunga ndoa hivi karibuni.
Screenshot_20220801-051758.jpg
 
Back
Top Bottom