Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

Junia
MSOSI..jpg
 
MASOOD KIPANYA KAZINDUA GARI MAPROFESA PALE SUA WANASAGA UNGA WA KULISHA MAPANYA.

Na Thadei Ole Mushi.

1. Pale SUA ukifika hapo utakuta Maprofesa wapo Busy kweli kufundisha Panya kunusa Mabomu utadhani Tanzania ipo vitani.

Unajua kwa nn wapo busy? sababu ni moja tu Mradi wa panya pale SUA unaojulikana kama APOPO kuna Unafadhiliwa na Chuo kikuu cha Belgium kinaitwa Antwerp. Yaani hawa panya wamewakeep busy vya kutosha Maprofesa wetu. Maprofesa wetu wanafuatilia Magawa ameacha watoto wangapi duniani Maprofesa wetu wanafua na kuitunza Medal ya Magawa isichafuke hizi ndio shughuli zao kwa sasa. Na ndivyo wazungu wanavyotumia miradi yao kuwafubaza akili wasomi wetu.

Kwa nini nasema haya?

Nimepiga Simu kwa watu wenye Viwanda vya kukamua mafuta Singida, Babati na maeneo mengine kuwauliza bei ya mafuta ni shilingi ngapi. Majibu yao yalikuwa kama ifuatavyo:-

Kiwandani

Lita ishirini wanauza kwa 105,000
Lita tano wanauza kwa shilingi 25,000.

Rejareja huku mtaani.

Lita 20 inauzwa Sh 120,000
Lita tano inauzwa kwa Sh 30,000

Kwa maana hiyo ni wastani wa shilingi Elfu Sita Mlalahoi apate Lita moja ya mafuta ya Kula.

Maajabu.

Asilimia 20 tu ardhi ya Tanzania ndio ambayo inatumika kwa kilimo nchini.Eneo kubwa lenye rutuba zaidi ya asilimia 46 ya eneo lote la Afrika mashariki kabla ya Congo kujiunga juzi Lipo Tanzania.Tanzania ina hekta milioni 44 za ardhi ya kilimo, na 5% tu ndiyo inayolimwa.Tuna mvua za kutosha kwa mwaka mzima, tumezungukwa na maji kila pembe ya nchi hii.

Tuna Maji kila Pembe ya Nchi hii tena Maziwa makubwa na Mito ya Maana. Tuna chuo Kikubwa kabisa nchini cha Agriculture na sasa wameanza kufundisha Ualimu pale.

Lakini hatuna Alizeti ya kutosha kuzalisha mafuta ya kupunguza Tatizo lililopo.

Mwaka jana pekee Tanzania iliagiza mafuta ya Kula nje ya nchi ya zaidi ya Bilion 222. Huku ardhi yetu ikiwa inaruhusu mazao ya mchikichi,Pamba na Alizeti kulimika yaani ukiyalima mazao hayo lazima uvune kwa kuwa ardhi yetu inayakubali.

Pamoja na hayo yote Tuna uwezo wa kulisha Mafuta nchini kwa Asilimia 40 tu. Asilimia 60 tunagiza toka nje ya nchi.

2. Jana Masood Kipanya Kazindua Gari iliyotengenezwa na Kampuni yake inayoitwa Kaypee Motor. Tena ka advance zaidi ni gari linalotumia Umeme. Wakati akiwa anafanya hivyo alikuwa anafuatiliwa kwenye TV na Maprofesa waliosomea Engeneering na wanafunzi wao wakiwa wamevaa maovaroli huku kwenye Karakana zao kukiwa hakuna hata Toroli la kusukuma kwa mikono.

Any way Kipanya yeye Elimu yake ni ya Form Four tu. .... amenikumbusha Elon Musk.

Elon Musk ni Mtu maarufu Sana Duniani na Tajiri mkubwa Sana. Anamiliki kampuni la SpaceX ambalo huunda vifaa vya kuhama Orbit Moja kwenda nyingine au kwa Lugha rahisi huunda engine za Rocket zinazoweza kwenda anga za juu na kutua katika Sayari nyingine (aerospace). Kampuni Hili linamiliki technolojia ya hali ya Juu Sana.

Kwenye Ukurasa wake wa tweeter mwaka jana aliandika hivi:-

I don't have an aerospace degree. I've read a lot of books and talk to a lot of smart people and have a great team.

Kwa tafsiri ameandika kuwa hana degree ya kutengeneza hizo aerospace Bali kinachomsaidia ni Kuwa anasoma vitabu vingi na kuongea na watu Smart na kuwa na Timu nzuri. Msikilize Kipanya alipokuwa anazungumzia timu ya wataalamu aliowachagua kwenye project yake ya gari.

Wasomi tujitafakari....hii ni pamoja na mimi japkuwa nimeishia tu Darasa la Saba B.

Ole Mushi.
071702602
IMG-20220403-WA0246.jpg
 
Back
Top Bottom