Napenda kutuma salamu kwa babu yangu,anaitwa mzee simba.
Salamu imfikie popote pale alipo,,,,,napenda kumwambia Kuwa nimemkumbuka sana,
Aje atutengenezee juisi ya ulezi kuchanganya na parachichi
Umenikumbusha mbali sana mjukuu. Enzi zetu ukiwa umeulamba hivi halafu uwe na baisikeli ya Phoenix uliyoinunua baada ya kuuza pamba nakwambia demu hachomoi. Hata yule aliyekula sh. kumi yangu nilikuwa nimeulamba hivi hivi. Yaani mpaka leo sijui nilikwama wapi yaani dah!
Asante kwa kumbukumbu nzuri mjukuu. Kila kitabu na zama zake. Enzi zenu hizi ni vijinsi vya kubana na mlegezo..