Vituko mitandaoni. Tupia chako

Huyo dogo aliyekabwa hapo alitegesha kitu kama msumari chin ya tairi ili gari likianza kuondoka tairi lipate pancha
Hii nilifanya nikiwa darasa la tano kwa trekta lilokuwa linasomba mchanga na kupita kwetu.Kibaya zaidi mimi nilikaa pempeni ya barabara hapo kushuhudia kitendo kinavotendeka.Alaulah!!!!!Lilikuwa ni kosa la jinai ambalo sitalisahau maishani,make nilipokea kipigo toka kwa mshua na dereva wa trekta kwa umoja wao walikuwa wanapiga mashambulizi ya mwizi. Na zaidi wakati wa purukushani saa ya dingi aina ya Disko ikapasuka kioo ndo niliona cha mtema kuni sasa nina 41yrs na sijawahi kusahau ze ujinga huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…