Happy's Pentecoste day wapendwa.

54bf82bce05cf246f42f5a2fc1fad0a0.jpg
5884c222c72425dafcc92dfad17e4aee.jpg
 
Aaabeeeh....😁😁😁😁

Ila hiyo video imetoa/imenipa taswira namna mke aliyeamua kuolewa na mwanaume haswa aliyekamilika idara zote.

Hii kichwa yangu sijui huwa inatoaga wapi tafsiri, sijui bangee nnazokorogea kwenye chai...!!!??🤔🤔

Anyways acha niendelee kidogo... huyo bibi harusi ametoa namna mke aliyekubali kuolewa aenende kwa mume wake kwa mustakabali mzima wa akili ya mume wako kuwa nawewe..... (maana asili ya mwanaume ni kuwa na wengi, wanaopinga na wapinge kivyao).

Bibi harusi ameonekana tangu mwanzo wa video anacheza non stop kwa furaha, tuweke kituo; mke unatakiwa ukiwa mbele ya mumeo muda wote uwe na furaha na mumeo akuone wewe ndo chanzo cha furaha yake, amani yake, burudiko lake na hapa ndo maana haswa ya mwanamke kuitwa kiburudisho cha mwanaume.... hakuna anayeburudoshwa na mwenye gubu..... kazi kwenu kunyoq au kusuka.... tuendelee....

Mwanaume ana mambo mengi kikubwa wewe ndo amekuoa ni mkewe, akili yake ya chini ikimtuma kwenda nje, usimkague, usimfate fate kufumania aka kutaka kujua yuko wapi yuko na nani anafanya nini...

La muhimu tuu akiheshimu, asiende huko na huko halafu hafuti ushahidi hadi unajua. Mwanaume mshenzi ni yule anafanyq ubaladhuli wake huko makusudi akuudhi huyo ukiweza hata usiolewe nae ni mshenzi wa tabia na ukiwa ndani tayari ujumlishe na kutoa maamuzi ni yako...

Hapo bwanahqrusi alipoenda pembeni wamshikie simu yake, bibi harusi aliona na akasindikiza kwa macho kuhamaki kulikoni, alipotambua namuamini mume wangu akaendelea na dansi lake kwa furaha, mume alirejea na akaendelea kucheza nae.

Hakumuuliza ulikuwa wapi kwa nani ulikuwa unafanyq nini, kalale hukohuko.....!
Bali alimsikiliza akapungiza beats na wakacheza wote hadi mume akablow mwenyewe na kutunzwa juu.


Well msitilie maanani sana alfulela ulela za Kasinde, tuendelee na vituko mitandaoni mambo ya ukungwi tuwaachie makungwi.

Ila kucheza style ya huu wimbo imenishinda kabisa aisee, yaani kila nikijaribu mabega na magoti vinaishia kutetemeka badala ya kucheza kuendana na beats.... sijui ndo uzee...

Alamsiki.
Katika ubora kwako kasie!
Nimetamani mno wakina dada wangesoma comment hii!
 
Back
Top Bottom