ISAYA 10:1-2
¹ Ole wao wawekao amri zisizo za haki, na waandishi waandikao maneno ya ushupavu;
² ili kumpotosha mhitaji asipate haki yake, na kuwanyang'anya maskini wa watu wangu haki yao; ili wajane wawe mateka yao, na kuwafanya yatima waliofiwa na baba zao kuwa mawindo yao!
HILO NDILO NENO LA MUNGU