babu na mjukuu
JF-Expert Member
- Jun 23, 2016
- 3,949
- 6,751
Watu wengine wana roho mbaya!!!
VANNY: Mambo debo?
DEBORAH: p..
VANNY: Mzima mrembo wangu wa nguvu?
DEBORAH: mzm..
VANNY: Dah ujue nimekumiss sana wewe?
DEBORAH: Okey..
VANNY: Mh mbona unanijibu shortcut mamii au nakuboa?
DEBORAH: Nop..
VANNY: Sasa kwanini unakuwa hivyo au upo na shemela nakusumbua?
DEBORAH: Mh..
VANNY: Kwani si unajua unachat na nani lakini?
DEBORAH: Yes..
VANNY: Ujue sipendi kabisa unavyofanya debo au hauko sawa leo?
DEBORAH: No..
VANNY: Bas sawa me nilitaka tu nikujulie hali pia nikuambie nimepata habari zako, nasikia ulifumaniwa na mume wa mtu guest ukala kichapo heavy na wakakutembeza mtaani uchi uchi Dah pole sana best.
DEBORAH: Weeeh koma kama ulivyokoma umepata wapi hizo habari za uongo, nani aliyekuambia?
VANNY: Mh..
DEBORAH: Si nakuuliza wewe nani kakuambia umbea umbea wenu mi sipendi.
VANNY: Okey..
DEBORAH: Mbona nakupigia cm haupokei una maana gani ujue ushanichanganya?
VANNY: Yes..
DEBORAH: Pokea cm we mbwa nakuja kwako sasa hivi usinitanie.
VANNY: No..
DEBORAH: Au ni wewe vanny ndio umenizushia mbona unanijibu mkato mkato hivi una maana gani?
VANNY: Bye..








Hahahahahaha.......
Hata mimi nimecheka sana mkuuNimecheka sana dah