Bado maji hayafiki mabwawani jamani? Mmekata umeme kuanzia usiku saa 10!


View attachment 2877469
TANESCO imesema mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini hususani katika ukanda wa Pwani na ukanda wa Ziwa Victoria, mtiririko wa maji yake hauelekei viliko vyanzo vya uzalishaji wa umeme vya Mtera, Kihanzi na Kidatu.
Mkurugenzi wa TANESCO, Eng. Gissima Nyamo-Hanga amesema mvua hizo zimeleta athari katika miundombinu ya shirika katika baadhi ya maeneo, hivyo kuongeza changamoto katika upatikanaji wa umeme.