Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

6f6a885ab4fef0d11914c7fc6ac37920.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbusho muhimu: ZINGATIA

Kwa mnaosafiri Kwa ajili ya Mapumziko ya Mwisho wa Mwaka, ni jambo jema,uwe peke yako au na familia yako
Jiandae ki saikolojia

1.Hakikisha gari iko vizuri
2.Safiri mchana tu
3.Waza kufika salama na si saa ngapi
4.Epuka mafuta ya vichochoroni
5.Kama kwenu mbali yaani km 700 na zaidi basi safari yako unaweza kuikata vipande viwili
6.Ukiwa na wasi wasi na uwezo wako tafuta mtu ukifika mpe posho kidogo na nauli arudi
7.Kuwa makini sana unapoanza safari na unapokaribia kufika
8.Usipende kusimama porini usipopajua bila sababu au kuchimba dawa
9.Usiku ukipishana na gari punguza mwendo huku ukiibia kushoto kwako kidogo
10.Epuka kushindana na gari/mtu ambaye hata hujui anatoka na anakwenda wapi hata kama gari lake ni sawa na la kwako
11.Kama vipi andaa chakula toka kwako anayeendesha atumie vyakula vyepesi bites zaidi nyama kavu za kutafuna
12.Akili yako muda wote iwe barabarani na sio unakokwenda au unakotoka
13.Jitahidi njiani si kila mtu ajue unaenda wapi
14.Hakikisha upepo uko sahihi wakati wote
15.Hizi mvua kuwa makini ukiona inazidi tafuta mahali salama paki subiri ipungue kisha uendelee
16.Hakikisha hakuna gari lolote nyuma linakufuata kwa muda mrefu bila sababu,chukua namba kisha mpishe aende

. ASANTE KWA KUSOMA UJUMBE NA KUUELEWA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom