Unaifahamu vema tafsiri ya upotoshaji?
Ukipata hakika rejea
Nakumbuka mwaka 2009 wakati nilipokwenda kumtembelea kaka yangu Mbeya (anafanyakazi almashauri pale mjini)....Kuna siku tulikwenda kulamba povu pendelevu (beer) kwenye bar karibu na pale almashauri. Kabla ya kufika pale kuna vinjia vya uchochoroni vya hajabu, yaani njia za mkato mpaka unafika pale bar. Nakumbuka ilikuwa kama saa mbili kasoro hivi, tukapita pale uchochoroni tukakuta pochi imejaa imetuna, nikashindwa kuikota kwa sababu nilishasikiaga habari za tego la kichawi juu ya Mbeya. Yaani mtu anakutegea kitu kama hela chini, ukiinama kuichukua unageuka kuwa mbuzi ama kuku, kisha unachukuliwa msukule kwenda kuuzwa Congo DR ama Zambia. Nikamtonya kaka, akasema ngoja aikote yeye.....kuhesabu zile pesa kukawa na laki 6 cash, na hapa tulikuwa njiani kwenda bar na shilling elfu 20 tu, hivyo tukawa na laki 6 za ziada. Ile kufika mbele tu, si chini ya mita 20 karibu na kijipori hivi, akatokezea jamaa yuko uchi huku kashika boxer mkononi anavaa akipiga kelele kaangusha pochi yake. Kusimama kumwangalia anakokwenda, akatokea demu kule kule porini alikokuwa yule jamaa, kutuona sie akashangaa na kuganda kwa mshangao huku akisema shemeji Samahani usimwambie mwenzio....tutaongea kesho, yaani yeye alikuwa mke wa rafiki wa kaka yangu alikuwa analiwa kule porini na yule jamaa. Kwa kifupi, tulichukua zile hela ila pochi tuliitupa mbele ya safari ili aione na kuiokota kwani kulikuwa na vitambulisho vyake mle.
Wasioyaweza wa Mjini....! Hawa majamaa wanayaweza!
Majamaa ni wajasiriamali wa kutoka moyoni na sio UDBS!
Na hapa ndipo wanapopikwa first class specialist doctors na senior Economists!
Na wana uwezo mkubwa wa ile tunaita PROBLEM SOLVING TECHNIQUES!
Mkoani si sawa na vijijini wajameni ...
1. Hakuna sehemu watu wamestaarabika kama mikoani maana ni mara chache kukuta vitu vya watu waliokosa kazi kama vigodoro mara sijui kuchambana..simply ustaarabu
2.hakuna sehemu zenye natural view poa na hali ya hewa nzuri kama mikoani.hivyo ukihitaji sehemu ya kupunguza stress then mkoani ni sehemu poa .
3. Chakula na bidhaa nyinginezo ukizitoa za viwandani ..hupatikana kwa bei nafuuu na maisha huku hayasubiri foleni ..hivyo kwa kiasi fulani ni stress free zone...
4.Magonjwa ya ajabu ajabu kama kipindupindu au upungufu wa nguvu fulani ni nadra kuyasikia pia kutokana na nature ya maisha...
5.huku ndo kuna wataalamu wa asiliambao watu wajanja huja kuogeshwa uchi huku wakililia masuala fulani ..sasa sijui mjanja anaekalishwa na mshamba nimuiteje
6.. huku ndipo wanapotokea waendeshaji wa dar maana wenyeji wameshakimbia na waliokulia huko wengi hawana ustahimilivu na maisha ndo maana wengi wamekuwa wateja badala ya wauzaji...
7. Watu waliopo karibu na mipaka ya nchi ni kawaida kusomesha watoto na kufanya shopping nchi jirani kwa mfano wana kagera wengi wanaijua kampala na kona zake kuliko hata dar na hata bidhaa za madukani kama nguo kwa kanda hii hutokea Uganda...
8. Vituko vya huku ni vituko kweli na kama ni ushirikina bhasi sio ule soft kama ulojo na kama matukio ya shoka ni shoka kweli la kiume...
All in all dar ni sehemu ya biashara hivyo pesa ni rahisi kiasi lakini mikoani ni sehemu ya kuishi vyema..nasubiri treni la magu lije ili nione watu wangapi watalala mikoani na kufanya biashara dsm ...
Aisee kwenye iisue ya Tanga kuongoza kwa waganga na wajanja wanaojifanya waganga ni pasua kichwa. Hasa kabila la wasambaa na wazigua. Nakumbuka enzi zile za giza kabla hata mambo ya kurikodi sauti hayajaenea kwa wengi kuna mshenzi mmoja msambaa kwa kabila aliwapukutisha watu wa uchagani kweli kweli. Huyo mshezi alikuwa na kibuyu chake kilichukuwa ''kinaongea'' kama mtoto mdogo anayejifunza kuongea kwa sauti ya kijini-jini hivi. Ukifika tu unaelezea shida yako halafu kibiyu kinaanza ''kufoka'' povu kama la bia lakini jeusi halafu kinakuagualia kwa kukueleza m'baya wako. Kama ni Mshana kinasema ''tio... tio.. ni shana... shana... loga loga'' (kikiwa na maana ya ndiyo ndiyo ni Mshana amekuloga.) Basi huyo mshenzi alikula vichwa vya wachaga wengi sana kwa hicho ''klijini'' chake. Baada ya mimi kukua na kutafakari ndio nikagundua kumbe alikuwa anaweka spika ndogo ndani ya kibuyu na kuunganisha waya wa kisiri siri kwa chini mpka kwenye chumba kingine karibu ambapo alikaa mwongeaji.