Dah!!!! Pole sana aisee wanaume wa tabia hii wanatufanya wanaume wote tuonekane hamnazo. Nani Aliyekwambia kwamba huwezi kubembeleza mtoto mpaka uwe na maziwa? Mkomalie abadilike ili akupe msaada nyumbani kama habadiliki basi itisha kikao cha wazazi au wakubwa wa pande zote mbili wakusaidie kumuelewesha umuhimu wa yeye kukupa msaada hapo maskani kwenu.
Tatizo hapo ni kuwa umeolewa. Ingekuwa mmeoana kusingetokea tatizo kama hilo.
Tatizo lingine, ni pale mume anapokuwa mwizi akiwa kazini, akiachishwa kazi maisha yanakuwa magumu X 3.
Ukiona mwanamme mvivu namna hiyo ujuwe ni mvivu kazini pia na mvivu bedroom. Kwa situation kama hiyo usitegemee kama kuna ufumbuzi wowote utapatikana, hicho ndio kichocheo kikubwa cha wewe kutembea nje ya ndoa kama bado hujaanza mpaka leo.
Yaani hapo unamvuruga huyu dada na kumuharibia ndoa yake. Unaposema 'akipata kazi' kwani hakuwahi kuwa na kazi? Makucha gani hayo yaliyofichwa kwa zaidi ya miaka mitano?
Haya ni baadhi ya matatizo na madhara ya kuleta post mahali pasipostahili. Ushauri mwingine hewa kabisa!
Aroo!!!!! Mkuu naona tumeanza kusemana hapa sasa kama huna la kuchangia bora ukae kimya ? Sio lazima This is too far. nitakupiga mkuki ?
Sikutegemea na ushungi wako mkubwa ungekuwa na mawazo finyu kama hayo, kwahiyo hukuona suluhu zaidi ya kutembea nje ya ndoa, kweli unaipenda ndoa ya mwenzako wewe? Kweli mlio wengi walimu wenu vipofu, umetoa ushauri finyu sana kwa kweli. Kesi ya usaliti huwa haiishi na inafunika kesi zote, ukirudishwa kwenu utajibu mme wangu alikuwa mvivu ndio maana nikaamua kutoka nje ya ndoa, kweli?
hujawahi kupata stress wewe. Yaani unaamka huna hata energy ya kutoka kitandani. Ukijilazimisha kuoga ndo imetoka hiyo.
Stress ni mbaya sana. Na zaidi mwanaume anaweza kuwa anajisikia nikifanya kazi nitaonekana ni kwa sababu sina hela. Hata hiyo kuomba kikombe cha kahawa, anataka kumkumbusha kuwa mimi ni mumeo
wakati mwenza anapitia hali ngumu anahitaji support ya hali ya juu. Kuna hausigelo, wasaidiane kazi za nyimbani. Period!
so ushamshauri hiyo gesi yako??????
kama wewe ni me utakuwa wa ajabu sana, mke akulishe, akuvishe na kila kitu akufanyie, pengine hata peteol ya kupuyangia anakupa, unashindwa kumsaidia hata kumtuliza mtoto wenu huku mama akifanya shughuli nyingine za ndani, eti kisa kuna wengine wanatafuta kuolewa hawapati wa kuwaoa. Wanaume tuache tabia chafu kama hizi unazojaribu kuonesha hapa. Lakini kama wewe ni ke, bado hujitambui hata kidogo
wanaume tulio wengi wa aina hiyo, tukiwa ulaya tunafua mpaka pichu za waajiri wetu. Teh he heeeekweli ndugu yangu wewe umenena
Huyu mwanamama alichokosea hapo ni vile tu alivyosema mmewe yuko home akitafuta kazi ,Sioni kama kaonyesha dalili za kumchoka mwenzi wakeila anaamini mmewe angeweza kumpa tafu ya mambo madogo madogo kama kukoroga chai yake mwenyewe wakati yeye akiwa busy na mambo mengi,au kusaidia kumbembeleza mwanae..
Bado kasema analazimika kufanya kazi na mtoto mgongoni wakati mmewe yuko busy na remote
Pia Kutandika kitanda ina maana mkewe akiumwa au kwa namna moja au nyingine hayupo nyumbani net inaweza kukaa kitandani mwezi mzima haijafuliwa ,haijatolewa kitandani na mashuka hayajabadilishwa ?
Huyu mama sijaona anasema anaomba mmewe aoshe vyombe ,adeki ,au apike ila amesema hata Chai kweli hawezi kujitengenezea?
Duh harafu naona wanaume wengi wanatetea
Msinimeze naomba kujua ina maana asili ya mwanaume ni Uchafu???
Please !!@Matola @Aspin RR Kaizer Mtambuzi ..na wengineo wengi comment zenu
Naamini, na ndivyo ilivyo, chochote unachadhani ni kibaya na hakifai kuanikwa hadharani maana yake usikifanye kabisa. Uvivu wa mtu sio siri ya mtu kuisema iwe ametoa siri ya ndani. Mnapenda sana kuexaggerate mambo, hata yasiyo siri ya ndani mnaita siri ya ndani. Mtaishia kunyanyaswa tu kama hamtajitambua hata tuwatetee vipi huko kwenye jamiipole sana dada ni dhahiri tabia za mumeo baada ya kukosa kazi zinakukwaza mno....hii tabia yakuanika mambo ya chumbani humu kwa kweli siipendiiii kabsa....
huyo mumeo naye akija kusema mapungufu yako itakuwaje aanze kusema mke wangu mara hiv mara vile nawe uje ugundue utafil ajee..? au huyo mumeo asome hizi habari zako aone unavyo mnanga patakalika..?
naamini hukulazimshwa kuolewa naye ulimpenda vile alivyo... maisha kunakupanda nakushuka bhanaa......mweleze kwa upole na deko aone namna gani unahitaji msaada wake mpaka mwenyewe afil guilty...hata kama amekosa usianze kumnunia wanaume wanadekezwa bibie ni kama watoto wadogo atiiiii
Hili ni tatizo la kuokota wanawake barabarani kitu kidogo yuko tayar kupoteza ndoa yakee..... wenzako kibao wanakazi nzuri na mishahara minono lakini kila siku wanachezea mangumi waume wao walevi, wana michepuko hatarii na mke anajua ametulia tuli anamuomba mola wake ambalishe mume wake....wewe kufua hizo boxer na kahawa umenuna wiki nzima....pu.mbavu sanaaa
Dina ukisema habari kamili hiyo ya net ni siyo sababu yenyewe hasa inayomsumbua dada huyu bali sababu yenyewe ni kuwa Mama akiwa kazini jamaa kakaa tu home na akirudi toka kutafuta rizki inayofanya ndiyo wale jamaa bado hajafanya kazi yyt ile home ikiwemo kumtunza mtoto!
Swali Je wakati jamaa ana kazi alikuwa anatandika kitanda?Kama hajawahi fanya kazi hizo kwa nn leo aonekane kituko?
Inawezekana sijapitia post zote, lakini jibu la mleta mada limekuwa lipi kuwa 'bwan' shemeji' alikuwa akifanya hayo kabla? Kama alikuwa akifanya, basi swali lije kuwa kulikoni? Na kama amesimama, basi yaweza kuwa kuna sababu, msongo ikiwa mojawapo. Kama hakuwa akifanya kabla, basi iweje leo aanze tu? Kwa mfumo wetu ulivyo lazima itaonekana anafanya au anaulizwa afanye kwa kuwa hana kazi! Na ninavyoelewa mie kwenye ndoa vitu vingine vinaonekana vidogo lakini kiuhalisia viko sensitive haswa...
Mimi swali langu linabaki pale pale bro, hatujagombana, tuna vicheko kede kede ndani ya nyumba na furaha tele, shughuli/kazi pia wote tunazo...kuna ugumu wa kunyanyua ka-neti ukarushia juu?