Vitu vinavyonikera ndani ya ndoa

duuu maduma ya hiv cjui yameshikiwa akl zao
 

Kama ilivyo kufunga ndoa ni hiari ya mtu pia kuachana ni uamuzi wa mtu binafsi. Huwa hatushauriwi kuachana ila yakifika kooni na yakikushinda unaachana mwenyewe bila hata kushirikisha watu. Huyu bado hajafikia stage ya kuachana ndio maana anaomba ushauri.

Hata kukaa bila kazi wala haikukeli kwa mwanaume ni kitimbi pia na ni aibu, kama ulikuwa hujui hakuna mwanamke anayetaka kuwa na mwanaume asiyejishughulika. Kuwa baba wa familia ni majukumu kwenye familia sio kuuza sura. Unatakiwa kuhakikisha familia inapata huduma zote. Kuendelea kumlea ni sawa sawa na kukumbatia bomu ambalo linaweza kulipuka wakati wowote. Lazima apate mrejesho ili akili iweze kufanya kazi.
 

Kuoa mwanamkeze msomi na mwenye kazi, ni kujitakia kufa haraka.

Huyo mwanaume angekua na hela afu akakufanyia ivo, hata usingekuja kumwanzishia thredi.
 
unamuona yuko hivyo sababu hana kazi alivyokua nayo hayo hayakuonekana,..nakushauri achana nae coz ni kero kwako.Endelea kuwalea watoto mwenyewe si unajimudu kwa sasa.
 
Umeonge kwa feeling sana asee....roho imeniuma sana.pole
 
Hakika wewe ni mdada wa tofauti sana coz unabusara pia unajitambua,..aliye kuoa amepata kitu cha thaman sana.Big up*1000
 
Mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba kwa mikono yake mwenyewe,...
 
Ndiyo ndoa za siku hizi usipoleta kitu home anakuhesabia siku!Mm ishafukuzwa mara 2 tena usiku wa manane baada ya kuishiwa ili hali wkt nina pesa walionyesha mapenzi ya kweli!!
Hayo hayakuwa mapenzi ya kweli gwa kukaja!...
 
Moja ya kitu tunakikosa kwenye ndoa/mahusiano ya mapenzi ni mawasiliano mazuri,tafuta angle nzuri mlizungumze hili,ila hilo la mtoto kulia usiku nadhani unahusika,suala la kutandika kitanda mwambie tu usiogope but kuwa makini utakavyoliadress
 

Uko sawa, lakini iwe kwa maneno mazuri, busara na upole. Wajua vitimbwi na kejeli ni sumu ya mapenzi; na bila mapenzi hawa watu hawataweza kwenda pamoja. Na hii ni miongoni mwa vyanzo vya watoto wa mitaani na panya road.

Ni kweli kuwa baba ni majukumu; lakini huwezi kubebesha majukumu kwenye kero. Mahali pengine mtu anaweza kuona bora kukaa peke yake kuliko kunyanyasika kisaikolojia. Upole ni muhimu zaidi kuliko maneno mengi.

Usidhani kuna 'mume' anayependa kukaa bila kazi. Kukosa kazi sio kitimbi; kazi zinapatikana kwa shida. Wangapi wana degree hadi masters mkononi leo hii na hawana kazi! Kama mambo ni rahisi hivyo, msaidie huyu dada kwa kumtafutia mumewe kazi; na kama akiikataa hiyo kazi turudi hapa jamvini kwa mjadala mwingine. Na hii pia itapunguza lawama kama si kuziondoa kabisa.

Unatarajia mrejesho wa aina gani mtu anaposhauriwa kuanzisha hizo mbwembwe? Utakavyomtenda mtu ndivyo atakavyokutenda. Basi, mpeni ushauri wa mapenzi na busara.
 
sijaona sehemu umesema uliongea nae then hajabadilika... haya ya kifamilia mamii yanaeleweka mweleze kwa upendo kama ni mwelewa ataelewa your concern, NOTE:- Dont you ever mention issue ya yeye kutokua na kazi wakat unamweleza.. but in a way shows helping each other and sharing of responsibilities, na pia msikilize na yeye with respect. ni hayo tuu.

sorry sijaolewa lakin, i dont knw if that will make sense to you.
 

Baby M, It makes a lot of sense; it is a real sense!
 
Kwa taarifa zako mwenyewe, mumeo amefukuzwa kazi, wewe ndiye unayehudumia nyumba kwa mahitaji ya kawaida ya nyumba, Unahudumia pia watoto wenu wawili. Kinyume chake ni kuwa mumeo alipaswa awe na kazi na alipaswa ahudumie nyumba yenu kama baba mwenye nyumba anavyopaswa kufanya, lakini hafanyi hivyo. Kwa kuwa hatimizi wajibu wa kutunza nyumba kama baba mwenye nyumba basi alipaswa akusaidie baadhi ya majukumu kwa kuwa kiukweli umezidiwa. Unafanya pia majukumu ya kiume, basi ingekuwa busara kwa kutambua hili mumeo angefanya pia baadhiya majukumu ya kike kwa kuwa ya kiume hayawezi. Lakini pia kama binadamu, kutokana na kufanya majukumu hata yasiokuhusu huwa unachoka. Ni kweli na ni jambo la kawaida kabisa.
Katika ndoa swala la kusaidiana sio ombi ni wajibu. Hoja ni usidie nini uache nini, usaidie wakati gani? Jukumu la kumtunza mke ni la mume kwa kufuata maandiko matakatifu, lakini kwa hali halisi ilivyo sasa katika familia yenu, wewe unajitunza mwenyewe, mumeo na watoto wenu. Ukidai utunzwe na mumeo wakati unaona mumeo hana kazi utakuwa unakosa hekma. Hali kadhalika jukumu la kutandika kitanda na kuandaa chakula ni la mke, lakini unapoona mke anakimbizana na muda kuwahi kazini au anachelewa kukupikia kutokana na kukamilisha kazi yenye ukomo wa muda( dead line) ni busara kumsaidia.
Ni vema pia kumsaidia mwenzi wako pasipo manung'uniko. Unapomsaidia huku ukinung'unika, msaada hugeuka masimango au manyanyaso, ladha ya msaada huu hugeuka na kuwa shubiri.
Kama unavyofanya wewe sasa hivi, unajaribu kuondoa ladha ya msaada wako kwa mumeo. Bora ungalimuomba msaada akusaidie kuliko kuja kumsema humu ndani jf. Mumeo ndiyo msiri wako wa kwanza hata kama kuna umbeya nadhani mbeya wa kwanza ni mumeo. Unapokuwa na mtu wa watatu kumsema mumeo, upendo unakuwa umekwisha au labda utarejea akipata kazi. Rafiki wa kweli hujulikana wakati wa shida. Kama leo mumeo ana shida huonyeshi upendo, upendo wako utakuwa sio wa kweli. Maandiko matakatifu yanatutaka hata kama tutakoseana, basi tuonyane kwa upendo. Sio upendo kumsema mumeo jf wakati unakaa naye kwenye kuta nne, unalala naye kuanako 6x6, unakula naye meza moja unashidwa kumueleza yanayo kusibu. Hakika hii ni zaidi ya unafiki
 
Mbona unazunguuka,..mwambie tu amwache ili mshahara wake usimuume.Yanini akonde bure?
 
bantulile, umeongea vyema sana mkuu. Ila naona kuna hoja moja haijakaa sawa; kuhusu majukumu ya kike na ya kiume.

Naona majukumu ya kike ni yale yanayomuhusu mwanamke kijinsia na ambayo mwanaume hayawezi kwa namna yoyote, kama mambo ya uzazi, kunyonyesha, kumpa mtoto mapenzi ya mama, na mengine kama hayo.

Majukumu ya kiume ni yale yanayofungamana na jinsia ya kiume, kuitunza familia kwa kadiri ya uwezo alio nao, kuipa familia mapenzi ya baba, na yanayohusiana na hayo.

Ama majukumu kama kufua, kupika, kutandika kitanda, kuosha vyombo, kumbeba mtoto na kucheza naye, usafi wa mazingira, nk, hayana jinsia. Husemwa kuwa ya kike kwa mazoea tu; haya yanaweza kufanywa na mume au mke; ni maafikiano ya watu wawili. Ndivyo ninavyoona.
 
Kwa sibhonike mkuu,...kama unaelekea kiwila kwa fasi ya ziwa nyasa!.....

Daaah inawezekana tunafahamiana mkuu!Sibonike ni maarufu sana na sidhani kama kuna mzawa wa Kyela hapafahamu!

Ukija Kyela japo kwa likizo alert me hommie tupate angalau tubia tuwili pamoja
 
Ndio maana ajira yake "iliisha"...
Vivu kama nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…