Vitu siwezi kuja kufanya kwasababu ya mapenzi

Vitu siwezi kuja kufanya kwasababu ya mapenzi

Vitu ambavyo siwezi kuja kuvifanya hata nipende vipi. Vitu hivi vikitokea bora kla mtu aende upande wke tu na wala sitojiuliza mara mbili ni kuachana tu.

1. Kua against na familia yngu. Hta nipende vp km hakuna maelewano mazur kati ya familia yngu na mwanaume ninaempenda halafu tatzo likawashindwa kua solved naachana nae tu siwezi kuchagua mwanaume niliekutana nae tu hko juu ya familia yngu. Kwa mimi familia yngu ndio kla kitu hpa duniani na hakuna mtu yoyote anaweza kuwa juu ya familia yngu. Huelewani na familia yngu bora tuachane.

2. Mapenzi na kazi. Ati hv ninavohangaika na anatomy na physiology hta silali vizuri halafu mtu aje aniambie niache kazi kisa mapenzi tu. Ati nikae nyumbani tu 🙄 mwanaume wa hv naachana nae mara moja. Siwezi kuja kuchagua mapenzi juu ya kazi NEVERRRR

Kwangu vtu hv vina value kubwa kulko mapenzi. Km hv vitu hv havitokua sawa na mapenzi hakuna. Je wewe ni vtu gani vina value kubwa kwako kuliko mapenzi?

Ile miti vipi inakuwa vizuri?
 
Mume sio familia yako[emoji849], uko serious au unatania. Ila ukiishi na hii mentality utapata tabu sana ukija kuolewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu anasumbuliwa na kauli au malezi flani toka kwa mmojawapo ya wazazi wake, au wote wawili.
Hiyo akili ya kuongea hayo haijokea hewani tu toka kusikojulikana.

Basi kwa mawazo yake huyo baba yake asingekuwa sehemu ya famila yao kama mumewe hatakuwa familia yake.
 
Ndoa si drama mbele za watu nyomi, ndoa ni ule upendo uliobakia moyoni/

Ndoa ni ndoanoo
 
ki ukweli ujaeleweka una lengo gani kwenye post yako inaonyesha hujui nini maana ya familia likewise your under age ngoja ukue kwanza
 
Ukikua hata hiyo no.2 itakuja automatically.

God save us
 
Vitu ambavyo siwezi kuja kuvifanya hata nipende vipi. Vitu hivi vikitokea bora kla mtu aende upande wke tu na wala sitojiuliza mara mbili ni kuachana tu.

1. Kua against na familia yngu. Hta nipende vp km hakuna maelewano mazur kati ya familia yngu na mwanaume ninaempenda halafu tatzo likawashindwa kua solved naachana nae tu siwezi kuchagua mwanaume niliekutana nae tu hko juu ya familia yngu. Kwa mimi familia yngu ndio kla kitu hpa duniani na hakuna mtu yoyote anaweza kuwa juu ya familia yngu. Huelewani na familia yngu bora tuachane.

2. Mapenzi na kazi. Ati hv ninavohangaika na anatomy na physiology hta silali vizuri halafu mtu aje aniambie niache kazi kisa mapenzi tu. Ati nikae nyumbani tu [emoji849] mwanaume wa hv naachana nae mara moja. Siwezi kuja kuchagua mapenzi juu ya kazi NEVERRRR

Kwangu vtu hv vina value kubwa kulko mapenzi. Km hv vitu hv havitokua sawa na mapenzi hakuna. Je wewe ni vtu gani vina value kubwa kwako kuliko mapenzi?
Dah...mie nasubiri uzi wako mwingine siku za mbele huko.... utakao kuwa unalialia " Natafuta mwanaume yoyote anioe"

Sent using Beretta ARX 160
 
Kwa namba 2 ni sawa ila kwa namba 1 ndoa utaisikia kwa wenzako....
 
duuu kwa izo sifa subiri kuwa single mother wa zaidi ya watoto 3 na kuendelea. hivi ujiulizi kwanin wazazi wako wame dumu mpk leo na mpk waka kupata wewe. ndoa ni ya watu wawili tuu

SOMA HILI LILOMKUTA MWEZAKO KISA KUSIKILIZA WATU NA NDUGU


*MWANAMKE ALIYEACHIKA ANAANDIKA*
Ninaandika haya ili uelewe kwamba ni vizuri kuwatambua wenza wetu na mchango wao licha ya mapungufu yao. Nina umri wa miaka 32. Mimi na mume wangu tulikaa kwenye uchumba kwa miaka 6. Tulikuwa marafiki sana. Nilimsubiri mpaka alipomaliza masomo yake ya chuo na kuanza kazi.

Familia yangu na yake zilikutana, tukaoana na kupata mtoto ambaye kwa sasa ana miaka 7.

Wakati mwingine mume wangu alikuwa mwenye hasira za karibu lakini matatizo yetu yalianza pale nilipotaka kumfanya ajihisi kuwa hawezi kunidhibiti. Kila wakati tulipojibizana, nilifunga mabegi yangu kwenda kwetu na kuieleza familia yangu.

Dada zangu walikuwa wakimpigia simu mume wangu na kumfokea. Akinikatalia jambo au kunidhibiti nilikuwa nikimtishia kwamba kama anataka anipe talaka yangu. Sikuwa nataka talaka kweli, bali nilikuwa na kiburi na sikutaka nionekane kuwa ni mwanamke rahisi na dhaifu mbele yake.

Siku moja nilimsukuma sana kiasi kwamba alishindwa kuvumilia na kwa mara ya kwanza akanipiga na kunifungia nje. Nilienda kwa wazazi wangu. Ndugu zangu walimripoti polisi, kila mara nilijifanya kana kwamba nilikuwa nanyanyaswa. Lakini kwa kweli, mimi nilikuwa nikimnyanyasa mume wangu kiroho na kihisia.

Alikamatwa na kufungwa. Familia yake iliniomba nifute kesi. Nilihisi kwamba nilichofanya hakikuwa sahihi. Mume wangu hakuwa mtu mgomvi, alifanya aliyoyafanya kwa sababu nilimsukumia ukutani. Alipiga magoti na kuomba msamaha. Nilimsamehe, nikafuta kesi na tukasuluhishwa.

Baada ya miezi 3, nilifungasha mabegi yangu tena baada ya kutokea tatizo kidogo, nikaondoka akabaki peke yake. Siku mbili baadaye nilipokea simu kwamba alikuwa hospitali.

Ndugu zangu waliniambia kwamba sipaswi kwenda kumjulia hali kwa sababu ingeonekana kana kwamba najikomba kwake, na hata dada zangu waliamini kuwa hakuwa mgonjwa bali alikuwa akiongopa.

Muda wote huo, watu walinisikitikia kana kwamba mimi ndiye niliyekuwa nikinyanyaswa.

Alikaa wiki moja hospitalini, alipotoka nilipokea wito wa talaka.
Nilitaka kuikataa talaka, lakini kwa kuwa nilijihisi kiburi, nilitaka yeye ndio abadilishe nia na kuniomba tuendelee kuwa pamoja.

Nilimpigia na kumwambia anipe talaka yangu kwa sababu niliishi kana kwamba niko motoni.

Nilipoenda mahakamani, nilitaka kumfanya ajutie, niliiambia mahakama kuwa nataka tugawane mali zake.

Kwa mshangao aliiambia wazi mahakama kuwa mali ambazo mimi na yeye tulichuma pamoja nikabidhiwe zote, yeye anachotaka ni kuachana na mimi.
Tuliachana rasmi Julai 2009.

Kwa sasa mtalaka wangu ana mke mwingine, wakati mimi nikiwa hapa nimetelekezwa! Mwanangu pia anakosa upendo na usuhuba wa baba yake. Ndugu zangu wananisengenya na kunisema vibaya.

Maisha yangu yanategemea kile ambacho mwanangu anapewa na baba yake.
Najua niliichezea bure na kuipoteza ndoa yangu.

Niko hapa kuwaambia wanawake kwamba wanapaswa kuwa makini kuhusu ushauri wanaopewa na watu.

_*Usidanganyike, usiruhusu watu wakaingilia ndoa yako.*_
Hata dada zangu wadogo wanaheshimiwa kuliko mimi.
Wale waliokuwa wakinichochea niachike ndio ambao muda wote wananicheka na kunidharau.

Tafadhali dada zangu, shikamana na ndoa yako na uilinde vikali.
Ni rahisi mumeo kukuacha kama unaendelea kumvunjia heshima na kumkosea adabu. Atafanya hivyo bila kujali elimu yako, cheo chako na historia yako.
Niliona vyema niwashirikishe simulizi yangu ili mpate kuziokoa ndoa zenu.
Hakuna faida ya kuwa na kiburi kisichokuwa na manufaa.

*WAKATI MWINGINE HUWA SIO KOSA LA MWANAUME KABISA, BALI NI KIBURI CHAKO NA WALE WATU UNAOWARUHUSU KUKUSHAURI, HIVYO TUMIA HEKMA NA BUSARA KATIKA NDOA YAKO*.

 
Huyu alieandika huu uzi na wanaomuunga mkono hawajui chochote kuhusu ndoa Ilianzishwa na Mungu mwenyewe na akasema mtawaacha ndugu zenu wazazi wenu na mtakuwa mwili mmoja na kuishi pamoja kivyenu, ndoa ni zaidi ya haya aliyoandika, kama hajatendwa basi hizi ni hasira za kutendwa tuulize sisi tulio kweny ndoa zaidi ya miaka 12 tukuambie na mama ako akikuskia unasema hivi atalia sana
Mume sio familia yako[emoji849], uko serious au unatania. Ila ukiishi na hii mentality utapata tabu sana ukija kuolewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama unazungumzia hawara au bwana na sio mume hapo sawa maana kuna tofaut kubwa sana kati ya hao wengine niliotaja na mume
 
Back
Top Bottom