Betting kwenye kitu gani ?
Kwenye mpira / casino na mchezeshaji yoyote ambaye ni Bookmaker Betting ni Probability inayomu-favor mchezeshaji.. Thus in the long run utapoteza / utaliwa... tu Ngoja nikupe mfano....
Tuseme tunajua kabisa kwamba Timu A kwa nguvu zake ana uwezo wa kuzifunga timu zote bila shida yoyote ila kutokana na happenstance kwa kawaida huwa anadraw mechi moja au kufungwa katika msimu (sio zaidi ya mechi moja); Labda msimu una mechi 100; kwahio mimi mchezeshaji nikikupa Odds za 1.2 ; hapo ni kwamba ukiweka dau la Tshs 1/= mara mia utakuwa umetumia Tshs 100/= na kama Timu A ikishinda mechi zote kama ambavyo inategemewa on average utakuwa umepata Tshs 120 yaani faida Tshs. 20/= na sababu najua hilo kwamba kuna game moja itapotea kwahio utashinda Tshs 19/=
Kwa kufahamu hilo badala ya kukupa odds za 1.2 Takupa odds za 1.01 Yaani kwenye mechi 100 ukishinda zote utapata faida ya Tshs. 1 lakini sababu najua kuna atleast game moja Timu A itapoteza utakuwa umepoteza Tshs. 1 kwenye hio game hence mwisho wa siku utajikuta wewe ndio umepoteza
Moral of the Story: The House Eventually Always Wins