IshaLubuva
JF-Expert Member
- Dec 4, 2008
- 250
- 11
Imeshakuwa ni muda sasa tangu ilipoamuliwa kuwapatia wanawake upendeleo wa kuwa na nafasi za Udiwani na Ubunge zijulikanazo kama Viti Maalum. Oktoba mwaka huu wa 2010 tunaendaq kufanya uchaguzi wa madiwani, wabunge na Rais. Ningependa wana JF tujadiliane kuhusu nani hasa anayenufaika na nafasi hizi za viti maalum? Je, ni kweli kuwa wanawake wa Kitanzania wananufaika kwa namna yoyote? Mbona nafasi hizi zimeendelea, kwa kiasi kikubwa, kugawanywa miongoni mwa wake za wakubwa tu?. Je, kuna haja ya kuendelea kuwa na nafasi hizi?