Hivi vitambulisho watu walikuwa wanalipia 20,000/=, na uongozi wa mikoa, wilaya kata na vijiji waliamriwa waakikishe vitambulisho walivyopewa vinaisha. Hii ilikuwa ni biashara moja nzuri kwa waliobuni na ilikuwa ni kwa manufaa yao, maana wakiulizwa hizo fedha zilizopatikana zilifanya nini, majibu yatakuwa yana ukakasi tu. Vya NIDA havilipiwi, na ndiyo maana wanashindwa kuviwekea mkazo, japo kuna mbinu waliyokuwa wananaitumia kupitia mitandao ya simu ili kukusanya fedha