Vitambulisho vya wamachinga maarufu kama vitambulisho vya Rais Magufuli

Ulimbo

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
3,767
4,034
Kuna vitambulisho vya wamachinga vilivyo kuwa vinatolewa kwa gharama ya shilingi 20,000/=, ambavyo vilisemekana ni kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama wamachinga.

Kwa kweli watu ambao wamenufaika na vitambulisho hivi ni wafanya biashara wakubwa kwani waliamua kutoa bidhaa zao ndani kwenye maduka na kuuza barabarani hivyo kukwepa kodi ya serikali, leseni za biashara na pia kodi za mapango.

Sasa mwaka umeanza, je vitatatolewa vingine au watahuisha/renew hivi vitambulisho au ndo vya moja kwa moja?

Je kama watarenew, gharama zitabakia zilezile au zitabadilika?

1578495237971.png
 
Vitahuishwa kwa mara ya mwisho na baada ya uchaguzi vitafikia mwisho wa matumizi na jamaa watafurushwa mitaani. Sawa na itakavokuwa kwa wafanyakazi kuongezewa mshahara wa mwaka 2020/21 na baada ya hapo watarudi mwanzo.

Hata korosho na mazao mengine vitauzwa kwa bei ya juu. Na baada ya uchaguzi watatupwa.
 
Mbona vitambulisho hivyo vinafanikiwa
Ila vya NIDA vina feli????

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app

Hivi vitambulisho watu walikuwa wanalipia 20,000/=, na uongozi wa mikoa, wilaya kata na vijiji waliamriwa waakikishe vitambulisho walivyopewa vinaisha. Hii ilikuwa ni biashara moja nzuri kwa waliobuni na ilikuwa ni kwa manufaa yao, maana wakiulizwa hizo fedha zilizopatikana zilifanya nini, majibu yatakuwa yana ukakasi tu. Vya NIDA havilipiwi, na ndiyo maana wanashindwa kuviwekea mkazo, japo kuna mbinu waliyokuwa wanaitumia kupitia mitandao ya simu ili kukusanya fedha
 
Basi vya taifa wafanye hivyo
Maana mambo ya bure naona washashindwa
Bora wavitowe kwa fedha tu

Ova
Hivi vitambulisho watu walikuwa wanalipia 20,000/=, na uongozi wa mikoa, wilaya kata na vijiji waliamriwa waakikishe vitambulisho walivyopewa vinaisha. Hii ilikuwa ni biashara moja nzuri kwa waliobuni na ilikuwa ni kwa manufaa yao, maana wakiulizwa hizo fedha zilizopatikana zilifanya nini, majibu yatakuwa yana ukakasi tu. Vya NIDA havilipiwi, na ndiyo maana wanashindwa kuviwekea mkazo, japo kuna mbinu waliyokuwa wananaitumia kupitia mitandao ya simu ili kukusanya fedha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vitahuishwa kwa mara ya mwisho na baada ya uchaguzi vitafikia mwisho wa matumizi na jamaa watafurushwa mitaani. Sawa na itakavokuwa kwa wafanyakazi kuongezewa mshahara wa mwaka 2020/21 na baada ya hapo watarudi mwanzo.

Hata korosho na mazao mengine vitauzwa kwa bei ya juu. Na baada ya uchaguzi watatupwa.
Hakuna mfanyakazi ataongezewa mshahara kisa uchaguzi, hakuna unafuu wowote wa maisha utatokea hata kwa machinga kisa uchaguzi...serikali ya kijani haitahitaji ridhaa ya watanzania kuamua ibaki madarakani bali Tume ya uchaguzi na polis watafanya kazi hiyo. Nadhani Mungu atupe moyo wa uvimilivu taifa hili linapitia kugumu sana kuliko nyakati zote ambazo nimekuwepo hapa TZ.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom