Vitambulisho vya utaifa vs sensa kipi kifanyike?

Mr.Mak

JF-Expert Member
Feb 23, 2011
2,841
1,102
Ndugu wana Jf
Naomba kuuliza huenda nyie mmepata kuelewa ili mnitoe sintofahamu niliyonayo. Kwenye vyombo vya habari kuna tangazo linalihamasisha wananchi kujiandikisha juu ya vitambulisho vya utaifa. na huku serikali inaandaa sensa,mie nashindwa kuelewa kwanini seriakali itenge mapesa mengi katika sehemu mbili tofauti kukusanya taarifa zinazofanana? kama lengo ni kujua pekee idadi ya watanzania ili iwarahisishie kupanga maendeleo basi sioni kama kulikuwa na sababu ya kufanyika mazoezi mawili at the same time ambayo yanafanana.

Kama ningeombwa ushauri: kama ningeombwa ushauri juu ya hili ningeishauri serikali iachane na sensa na isimamie zoezi la vitambulisho, at the end watakuwa wamepata takwimu sahihi wanazozihitaji ambazo hazina contradiction upande wowote. Mamlaka ya vitambulisho imetengewe fedha nyingi sana na huku tunalia kuwa hatuna fedha kisha wanatenga zingine za sensa za kukusanya information ambazo wangeweza kuzipa kupitia mamlaka ya vitambulisho.

NAOMBA KUWASILISHA.
 
Kweli naunga mkono hoja, kutatokea contradiction ya figures, badala yake wakite nguvu zaidi kwenye zoezi la utoaji vitambulisho kwa wananchi wote, zoezi liende haraka na kwa ufanisi ili mwisho wake tupate idadi ya watu angalau inayokaribia ukweli, na pia michanganuo kama age/gender/education/special needs etc. Maswala ya dini fulani wako wangapi hayana tija.
 
Back
Top Bottom