Vitambulisho vya Taifa vyakamilika! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vitambulisho vya Taifa vyakamilika!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Michael Amon, Apr 28, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Apr 28, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imesema awamu ya kwanza ya Vitambulisho vya Taifa imekamilika na vitaanza kutolewa mapema mwezi ujao (May).

  Imesema kuwa uzinduzi wa kutoa vitambulisho hivyo ulikuwa ufanyike jana katika maadhimisho ya sherehe za miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lakini ilishindikana kutokana na shughuli nyingi na ukubwa wa tukio hilo.

  Ofisa Habari wa NIDA, Rose Mdami alisema uzinduzi huo unatarajiwa kufanywa na Rais Jakaya Kikwete ambapo wiki ijayo watazungumza na waandishi wa habari na kuelezea utaratibu mzima utakavyokuwa.

  Katika utekelezaji wa mradi huo, Mamlaka itatoa vitambulisho katika makundi matatu; Watanzania, wageni wakazi na wakimbizi.

  Alisema baada ya wafanyakazi wa Serikali, watafuatiwa wanafunzi, wafanyabiashara na hatimaye Watanzania wote watafikiwa na huduma hiyo muhimu kwa Taifa bila gharama yoyote.

  Hata hivyo, imeelezwa kuwa, pamoja na kuwa huduma hiyo ni bure, lakini mwananchi atakayepoteza kitambulisho chake atalazimika kukilipia.
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Apr 28, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Hivi itakuwa ni lazima kuwa na hivyo vitambulisho?
   
 3. mwitaz

  mwitaz JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 314
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tatizo itachuku muda mrefu kwa kila Mtanzania kukipata!
   
 4. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #4
  Apr 28, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Ni kweli itachukua mda sana mkuu na hiyo inatokana na wingi wa watu.
   
 5. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #5
  Apr 28, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli sina uhakika kama kuna ulazima au la.
   
 6. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2012
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  China wanavyo hivi.. nakumbuka nilikuwa train station! polisi anakuwa pale anapita randomly ku scan .. kina info zako zote!!! kama ni wanted man imekula kwako... kama haunacho ule muda imekula kwako... sijui hivi navyo itakuwa hivo... !
   
 7. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #7
  Apr 28, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Duh! Lets hope itakuwa hivyo.
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Apr 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Young_Master kwa siye tupo nje je vitatufikia kwa njia ipi?tutavipata hivyo vitambulisho?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #9
  Apr 28, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli mkuu sidhani kama kuna njia ya nyie mlioko nje kuvipata hivi vitambulisho labda mje huku bongo.
   
 10. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Lakini Mi ningependa sana kila Mtanzania angekuwa nayo kwn ingependeza sana!
   
 11. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #11
  Apr 28, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Kila mtanzania atakuwa nacho ila vitatolewa kwa awamu. haviwezi kutolewa vyote kwa wakati mmoja.
   
 12. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #12
  Apr 28, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,462
  Trophy Points: 280
  kweli mkuu wenzetu zambia wanavyo tokea zamani wakati huo sisi tunatumia vya ccm vilikua vinatolewa na wenyeviti wa vijiji kama sikosei.!
   
 13. Mtanzanika

  Mtanzanika JF-Expert Member

  #13
  Apr 28, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 2,210
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  kwa kua kuna balozi za Tz huko,nina imani vitawfikia kirahisi tu.
   
 14. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #14
  Apr 28, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Kama ndio hivyo basi sisi tumepitwa na wakati.
   
 15. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #15
  Apr 28, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Unadhani serikali ya Tanzania itawakumbuka hao walioko nje?
   
 16. Mtanzanika

  Mtanzanika JF-Expert Member

  #16
  Apr 28, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 2,210
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  ni lazima.
  kila huduma by that time itakuhitaji kuwa na Kitanbulisho,,,kama Wakenya wameanza kitambo sana na mambo haya.
   
 17. Peter Dafi

  Peter Dafi JF-Expert Member

  #17
  Apr 28, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 355
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 60
  Dah, sasa me nikajua nivizuri zaidi, mbona inaonekana sio Digitally hivi nikama vya wagambo au vya kupigia Kura, ndo nini sasa mpaka Wanyasa wanavyo.
   
 18. Mtanzanika

  Mtanzanika JF-Expert Member

  #18
  Apr 28, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 2,210
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  kwa kuwa ni waTz na nyumbani kwao ni hapa Serikali isipowakumbuka wao wataikumbusha.
   
 19. Mtanzanika

  Mtanzanika JF-Expert Member

  #19
  Apr 28, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 2,210
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hivi si kama vya Kura, hivi vina Chip kama vile ATM ambayo itakua na info zako zote.
   
 20. s

  shosti JF-Expert Member

  #20
  Apr 28, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  mie nabeba kinachonipa mkate hivi vya kwenu ym...hongereni hatimaye mmefanikiwa
   
Loading...