Vitambulisho 134 vya mpiga kura vyakamatwa na TAKUKURU mkoa wa Kagera

Chachu Ombara

Kuna kipindi niliaminishwa wenyeji wa Kagera ni watu wenye uelewa (wameelimika) kumbe mashipa tu tunayazidi hata sisi washoshang'ombe. Muache kula senene naona mnakoelekea mtauza hata watoto wenu.
 
Last edited by a moderator:
Mchezo wa kununua kadi ni mbinu ya siku nyingi ya chama tawala,bilashaka ndio wahusika wakuu

Zikisha nunuliwa zinafanywaje kwani?Mm huwa sielewe hii sanaa mana sioni km ni sayansi.Kadi ya mpga kuru itakaguliwa na kuhakikisha sura ıliyo kwenye kitambulısho na mpga kura mwenyewe.
 
Kama kweli ni hivi basi waacheni Watanzania waendelee kutawaliwa na ccm mpaka pale Yesu atakaporudi na kuwawezesha kujitambua. Kweli mtu mwenye akili timamu kwa hiari yako unauza kadi kwa 5,000/-!!!????? Kweli hii ni nchi ya misukule!
 
Zikisha nunuliwa zinafanywaje kwani?Mm huwa sielewe hii sanaa mana sioni km ni sayansi.Kadi ya mpga kuru itakaguliwa na kuhakikisha sura ıliyo kwenye kitambulısho na mpga kura mwenyewe.
Wanazinunua ili kupunguza kura za mpinzani make MTU akishauza kadi anakuwa ameuza haki take ya kupiga kura,ukichukulia hali ilivyo mbaya kwa maccm mkoa wa kagera,wanalazimika kupunguza kura za ukawa kwa mbinu I,watu wawe making hawa jamaa wanaosomba mania ya watu kwa malori wanaweza pia kununua watu
 
Hizi ni taarifa ambazo zimethibitishwa na naibu mkuu wa takukuru mkoa wa kagera John joseph
Kadi hizi zilikuwa zinanunuliwa kati ya sh 5000 hadi 10000,taarifa za kuwepo kwa njama zilitolewa na kijana mmoja ambaye hakuafiki kadi yake kununuliwa
Hivi hawa CCM wamelogwa nini, hawa ni mabingwa wa michezo yote michafu kuanzia rushwa, ufisadi na hata wizi wa kura kweny chaguzi mbalimbali, hivi huwa hawajisikii aibu chama chao kinapopigiwa kelele kwa mambo machafu wanayofanya? Hebu jirudini muwe waungwana tuendeshe za siasa kiustaarabu. Kwanini hamtaki kukubali kushindwa?
 
KUHUSU VITAMBULISHO VYA KUPIGIA KURA KUKAMATWA KAGERA

Vitambulisho 134 vya Kupigia kura, vimekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa –TAKUKURU- mkoani Kagera baada ya kukutwa vimenunuliwa na Kundi la watu kutoka kwa wapiga kura.

Taarifa ambazo zimethibitishwa na Naibu mkuu wa Takukuru mkoani Kagera, John Joseph vitambulisho hivyo vimekamatwa vikiwa tayari vimenunuliwa kutoka kwa wananchi kwa bei ya kati ya shilingi 5,000 hadi 10,000.

Amesema kuwa kukamatwa kwa Vitambulisho hivyo, kumetokana na baadhi ya Vijana walioshawishiwa kuuza kadi hizo na kundi la watu wanaopita, kutoafiki na kisha kulazimishwa kufanya hivyo.

View attachment 294967


Huku ndio kwa Miss yule wa Tegeta Escr...?
 
muvi wameitengeneza wenyewe

wamenunua wenyewe ili hao watu wasipige kura

jiulize vitaenda wapi baada ya hapo ?
 
Mwisho wa siku utasikia idadi ya waliopiga kura nchi nzima ni asilimia 30 na 70% haijulikani kwa nini hawakujitokeza kupiga kura kumbe kadi zao zimenunuliwa.
Inasemekana hata katika uchaguzi uliopita mgombea mmoja alinunua vitambulisho vya kupigia kura na baada ya kushinda akawapa wapambe wake wakavitupa pale stendi.
 
Hapo unapeleka mahakamani walionunua na hao wenye kadi hizo ndio itakuwa fundisho
 
Yaani umekesha usiku na mchana na hadi kuumwa na mbu kwenye kitua cha kuandikishia halafu unauza shahada kwa Tsh. 5,000/=, hii ni dhahiri ujinga na elimu ndogo na umasikini wa watanzania ndio mtaji mkubwa wa CCM na ndio maana hawako tayari ndani ya nchi hii elimu iwe bora na Wataznania tujukwamue kiuchumi ili waendelee kufanya ujinga kama huu.


Kwa ukweli kuna raia mizigo kweli kweli na kiuhalisia ni elimu ndogo ya darasani tu!
 
Zikisha nunuliwa zinafanywaje kwani?Mm huwa sielewe hii sanaa mana sioni km ni sayansi.Kadi ya mpga kuru itakaguliwa na kuhakikisha sura ıliyo kwenye kitambulısho na mpga kura mwenyewe.

Ikishanunuliwa inatupwa. Logic ni kwamba zinazonunuliwa ni zile ambazo wanunuaji wamejihakikishia kuwa ni wa upande mwingine. Kifupi ni kupunguza kura za upande pinzani.
 
Mbna huu mchezo ni wa kila baada ya miaka 5, mh.K undo mchezo wake ktk jimbo LA bukoba mjini.baada ya uchaguz kuisha hizo kadi utupwa mto kanon, hata 2005,2010 ccm walifanya hivyohivyo.
 
muvi wameitengeneza wenyewe

wamenunua wenyewe ili hao watu wasipige kura

jiulize vitaenda wapi baada ya hapo ?
Yupo Dada mmoja yuko rwamishenyi ndiye ananunua hizo kadi alishakamatwa na polisi halafu akaachiwa na akajitetea eti yeye anasajili line za simu kwahiyo wateja uziacha baadae uzirudia, wakati ni uongo, binachofahamu yeye amehakikishiwa usalama wake na mh.k eti kitakachotokea atasaidia
 
Maskini wa fikra huishi siku moja tu nayo ni leo!!!!!!!

Nawapa pole waliouza kadi zao kwa ajili ya leo!!!!!

Lakini alaaniwe yeye aliyewafanya hawa watanzania waishi leo bila kujali kama kuna kesho!!!

Ni mchezo mchafu usiofaa kuigwa hata mara moja kwani unadharilisha utume wa watu.
 
Tatizo watanzania 90% ni maskini wa kutupwa jamani chakula hawana, viatu hawana, nguo hawana, maji hawana, zaidi sana na elimu hawana n.k.
sasa mtu wa namna hiyo hata ukimpa 1000Tshs atakupa kadi yake. Hapa tunataka sasa tuione kazi ya tume ya uchaguzi NEC!
 
kweli elimu inahitajika sana unauza kadi kwa buku 5? yani yangu hata wangenipa laki moja siwezi kuuza haki yangu ........hivi chama gani kinafanya huu mchezo mchafu?
 
Back
Top Bottom