minziminzi
Member
- Nov 25, 2014
- 11
- 3
Hadithi-inayokuja,-ni-ya-Sungura-sikia,
Hadithi-uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia,-Sungura-nakuambia
Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura-akayapenda,-mtini akasogea,
Mtini akasogea,-Sungura-nakuambia.
-Sungura-karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka,-nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua-Sungura-nakuambia.
Mtazame hapo juu-Sungura-amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia,-Sungura-nakuambia.
Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho wake akachoka,-kachoka hata mkia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea,-Sungura-nakuambia.
Sizitaki mbichi hizi-Sungura-akagumia,
Naona nafanya kazi, bila faida kujua,
Yakamtoka machozi-matunda akalilia,
Matunda akalilia,-Sungura-nakuambia.
Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia,-Sungura-nakuambia.
Hadithi-nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda-Sungura, utapata mbivu hizi.
Hadithi-uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia,-Sungura-nakuambia
Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura-akayapenda,-mtini akasogea,
Mtini akasogea,-Sungura-nakuambia.
-Sungura-karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka,-nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua-Sungura-nakuambia.
Mtazame hapo juu-Sungura-amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia,-Sungura-nakuambia.
Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho wake akachoka,-kachoka hata mkia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea,-Sungura-nakuambia.
Sizitaki mbichi hizi-Sungura-akagumia,
Naona nafanya kazi, bila faida kujua,
Yakamtoka machozi-matunda akalilia,
Matunda akalilia,-Sungura-nakuambia.
Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia,-Sungura-nakuambia.
Hadithi-nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda-Sungura, utapata mbivu hizi.