Vitabu vipya vya TIE na hatma ya Tanzania

Teleskopu

JF-Expert Member
May 5, 2017
702
765
Kama ilivyokuwa kwenye post yangu iliyotangulia kuhusu kitabu cha Taasisi ya Elimu: Najifunza Kusoma Darasa la Kwanza Kitabu cha Kwanza, ambacho ndio kimeandaliwa kusambazwa Tanzania nzima kama kitabu cha Kiada kwa ajili ya MAISHA ya wanafunzi na taifa, leo nitaendelea kubainisha makosa MACHACHE TU KATI YA MENGI ndani ya kitabu chao kingine: Najifunza Kuhesabu Kitabu cha Mwanafunzi Darasa la Pili, ambacho ISBN yake kwenye uk i ni 978-9976-61-537-7 lakini kwenye uk ii ni 978-9976-61-535-7.

Ni maombi yangu kuwa watatokea wahusika watakaoweza kufanya kinachopaswa maana, kimsingi, vitabu hivi VINALETA MASHAKA MAKUBWA kwa hatma ya nchi yetu. Siamini kuwa suluhisho ni kuanza kuvitetea vitabu hivi.

Yafuatayo ni hayo makosa MACHACHE TU kati ya mengi kwenye: Najifunza Kuhesabu Kitabu cha Mwanafunzi Darasa la Pili

1. Uk 8 pameandikwa: “Siku moja alinunua daftari nyingi …” ---- Je, wingi wa ‘daftari’ ni ‘daftari’? Kosa hili limerudiwa uk 23, 45, 64.
upload_2017-5-11_12-58-27.png
2. Uk 9 pameandikwa: “Angalia mchoro ufutao …”
upload_2017-5-11_12-58-44.png
3. Uk 19 pameandikwa: “Kujumlisha bila kubadili kwa wima” --- “kubadilini kwa wima” ndio kitu gani? Kilicho cha wima ni ‘kubadili’ au ni ‘kujumlisha’? Kosa hili limerudiwa uk 24, 40.
upload_2017-5-11_12-59-6.png
4. Uk 22 swali la 3 pameandikwa: “Wakaungana na wenzao 427 wa shule ya msingi mapambano.” --------- kwani japo ni Hesabu, ndio usizingatie matumizi sahihi ya herufi kubwa?
upload_2017-5-11_12-59-25.png
5. Uk 23 swali la 7 pameandikwa: “… mitihani yake ya darasa la kwanza na la pili?.” -------- sentensi inawezaje kuishia na alama ya kuuliza na nukta? Swali la 8 nalo hivyohivyo.
upload_2017-5-11_12-59-40.png
6. Uk 24 hatua ya kwanza inasema: “kuna makumi 1 …” lakini ya 2 inasema: “Jumlisha hiyo kumi 1…” -------- Kwa nini hapa useme “kumi 1”? Kosa hili limerudiwa uk 27, 40, 42, 43, 44.
upload_2017-5-11_13-0-1.png
7. Uk 26 kuna “Zoezi la 6” na wa 27 nako ni “Zoezi la 6”. Kosa la namna hii limerudiwa uk 28, 53, 66, 73, 74, 88, 93.
upload_2017-5-11_13-0-19.png
8. Uk 28 swali la 2 linaishia hivi: Shule hizo Jumla ya wanafunzi wangapi? --- wrong sentence.
upload_2017-5-11_13-0-37.png
9. Uk 29 wanasema: “Chati hii ina miraba ya ulalo na wima kama inavyooneshwa na mistari ya ulalo na wima” --- Hivyo, kuna miraba (square boxes) na mistari (arrows).

Mtu atajiuliza:

MOJA: Mraba kama mraba mmoja unawezaje kuwa wa ulalo au wa wima?

MBILI: Aya ya pili inasema: “Ukichunguza mstari wa kwanza wa ulalo una namba 101, 102, 103, 104 na 105.” ----- kwa kuwa hapo juu umetofautisha kati ya mraba (square) na mstari (arrow), je, namba ziko kwenye mstari (arrow) au ziko kwenye mraba (square)?
upload_2017-5-11_13-1-9.png
10. Uk 38 swali la 1 linasema: “Kaka alikuwa na mayai 649, Akauza mayai 415. Alibaki na mayai mangapi? ----- “Alibaki”???

Swali la 6 linasema: “… alikuwa na midoli 888 akauza midoli 573. Alibakiwa na midoli mingapi? --------- hongera kwa kusema “Alibakiwa”. Lakini neno “midoli” ni Kiswahili sanifu?
upload_2017-5-11_13-1-29.png
11. Uk 54 wameandika: “Tunashikana mikono na kufanya duara.” ------- duara huwa linafanywa???
upload_2017-5-11_13-1-47.png
12. Uk 63 Zoezi la 1 limeshatimia na maswali yake na fremu yake, kisha nje ndio unaweka picha za sarafu na kusema: “Chunguza michoro ya sarafu zifuatazo.” Huoni kuwa hizo sarafu ndio zilitakiwa zianze, ndipo useme “Jibu maswali yafuatayo”?
upload_2017-5-11_13-2-4.png
Mtu mmoja akajibu akaniambia kuwa “nyingi ya hizi ni typing errors tu”. Japo si kweli, lakini hata kama zingekuwa ni typing errors peke yake, basi ndio mnataka kutuambia hamna mpango wa kuzisahihisha? Au mnamaanisha kuwa zinakubalika? Na kama mna mpango wa kuzisahihisha, mnaona ni sawa tu kutumia mabilioni ya fedha kuchapa upya vitabu ambavyo tayari mmeingiza makosa lukuki na vimeshazamisha fedha nyingi? Je, na hivi mnavyosambaza au mlivyosambaza mtavirudisha na kuvitupa?

Tunaponya taifa au tunaliangamiza?
 
Nimefedheheka sana, Mkuu huenda ndio matokeo ya watendaji wenye vyeti feki. Nashauri bandiko lako pia ungelituma kwenye barua pepe ya Taasisi husika ili waone kasoro hizo. Hongera kwa uchambuzi na ufuatiliaji kamanda.
Asante mheshimiwa Mteule kwa ushauri wako.
 
Sidhani kama boss wa taasisi ile ana muda wa kupita humu jf zaidi ya kwenye biblia yake anayoambatana nayo kila mahali.
Itoshe kusema TIE itumie walimu wenye weledi mpana katika masomo na utunzi wa vitabu na waepuke kuwakusanya wasiokuwa walimu kuandika vitabu.
Typing error karibu kitabu chote! Hapana. Bwana Kalonzo Yohana mteule mkuu wa taasisi japo nasikia umebadili jina angani badili aina hii ya uandishi wa vitabu kabla hujavisambaza kwa walaji.
 
Sidhani kama boss wa taasisi ile ana muda wa kupita humu jf zaidi ya kwenye biblia yake anayoambatana nayo kila mahali.
Itoshe kusema TIE itumie walimu wenye weledi mpana katika masomo na utunzi wa vitabu na waepuke kuwakusanya wasiokuwa walimu kuandika vitabu.
Typing error karibu kitabu chote! Hapana. Bwana Kalonzo Yohana mteule mkuu wa taasisi japo nasikia umebadili jina angani badili aina hii ya uandishi wa vitabu kabla hujavisambaza kwa walaji.
Nina uhakika TIE wametumia walimu katika uandaaji wa vitabu hivi Mnasihi. Lakini kuwa mwalimu sio synonymous na kuwa mwandishi hata kidogo; maana kwenye kozi za ualimu hakuna somo la uandishi wa vitabu. Ni kwamba tu its impractical kusema kuwa TIE ndio pekee wanaotakiwa kuandika vitabu vya Kiada. It simply won't work. It's destined for failure.
 
Back
Top Bottom