Vitabu vipya vya TIE na hatma ya Tanzania

Tatizo kubwa ni kwamba TIE wanapelekana kwa kujuana walimu wenye uwezo hawapewi nafasi watu ambao hawajawahi kufundisha kabiss eti ndo curriculum developer nchi hii tuna long way to go
 
Bado tunaaminishwa wanasiasa wajue kusoma na kuandika inatosha
 
Kama ilivyokuwa kwenye post yangu iliyotangulia kuhusu kitabu cha Taasisi ya Elimu: Najifunza Kusoma Darasa la Kwanza Kitabu cha Kwanza, ambacho ndio kimeandaliwa kusambazwa Tanzania nzima kama kitabu cha Kiada kwa ajili ya MAISHA ya wanafunzi na taifa, leo nitaendelea kubainisha makosa MACHACHE TU KATI YA MENGI ndani ya kitabu chao kingine: Najifunza Kuhesabu Kitabu cha Mwanafunzi Darasa la Pili, ambacho ISBN yake kwenye uk i ni 978-9976-61-537-7 lakini kwenye uk ii ni 978-9976-61-535-7.

Ni maombi yangu kuwa watatokea wahusika watakaoweza kufanya kinachopaswa maana, kimsingi, vitabu hivi VINALETA MASHAKA MAKUBWA kwa hatma ya nchi yetu. Siamini kuwa suluhisho ni kuanza kuvitetea vitabu hivi.

Yafuatayo ni hayo makosa MACHACHE TU kati ya mengi kwenye: Najifunza Kuhesabu Kitabu cha Mwanafunzi Darasa la Pili

1. Uk 8 pameandikwa: “Siku moja alinunua daftari nyingi …” ---- Je, wingi wa ‘daftari’ ni ‘daftari’? Kosa hili limerudiwa uk 23, 45, 64.
2. Uk 9 pameandikwa: “Angalia mchoro ufutao …”
3. Uk 19 pameandikwa: “Kujumlisha bila kubadili kwa wima” --- “kubadilini kwa wima” ndio kitu gani? Kilicho cha wima ni ‘kubadili’ au ni ‘kujumlisha’? Kosa hili limerudiwa uk 24, 40.
4. Uk 22 swali la 3 pameandikwa: “Wakaungana na wenzao 427 wa shule ya msingi mapambano.” --------- kwani japo ni Hesabu, ndio usizingatie matumizi sahihi ya herufi kubwa?
5. Uk 23 swali la 7 pameandikwa: “… mitihani yake ya darasa la kwanza na la pili?.” -------- sentensi inawezaje kuishia na alama ya kuuliza na nukta? Swali la 8 nalo hivyohivyo.
6. Uk 24 hatua ya kwanza inasema: “kuna makumi 1 …” lakini ya 2 inasema: “Jumlisha hiyo kumi 1…” -------- Kwa nini hapa useme “kumi 1”? Kosa hili limerudiwa uk 27, 40, 42, 43, 44.
7. Uk 26 kuna “Zoezi la 6” na wa 27 nako ni “Zoezi la 6”. Kosa la namna hii limerudiwa uk 28, 53, 66, 73, 74, 88, 93.
8. Uk 28 swali la 2 linaishia hivi: Shule hizo Jumla ya wanafunzi wangapi? --- wrong sentence.
9. Uk 29 wanasema: “Chati hii ina miraba ya ulalo na wima kama inavyooneshwa na mistari ya ulalo na wima” --- Hivyo, kuna miraba (square boxes) na mistari (arrows).

Mtu atajiuliza:

MOJA: Mraba kama mraba mmoja unawezaje kuwa wa ulalo au wa wima?

MBILI: Aya ya pili inasema: “Ukichunguza mstari wa kwanza wa ulalo una namba 101, 102, 103, 104 na 105.” ----- kwa kuwa hapo juu umetofautisha kati ya mraba (square) na mstari (arrow), je, namba ziko kwenye mstari (arrow) au ziko kwenye mraba (square)?
10. Uk 38 swali la 1 linasema: “Kaka alikuwa na mayai 649, Akauza mayai 415. Alibaki na mayai mangapi? ----- “Alibaki”???

Swali la 6 linasema: “… alikuwa na midoli 888 akauza midoli 573. Alibakiwa na midoli mingapi? --------- hongera kwa kusema “Alibakiwa”. Lakini neno “midoli” ni Kiswahili sanifu?
11. Uk 54 wameandika: “Tunashikana mikono na kufanya duara.” ------- duara huwa linafanywa???
12. Uk 63 Zoezi la 1 limeshatimia na maswali yake na fremu yake, kisha nje ndio unaweka picha za sarafu na kusema: “Chunguza michoro ya sarafu zifuatazo.” Huoni kuwa hizo sarafu ndio zilitakiwa zianze, ndipo useme “Jibu maswali yafuatayo”?
Mtu mmoja akajibu akaniambia kuwa “nyingi ya hizi ni typing errors tu”. Japo si kweli, lakini hata kama zingekuwa ni typing errors peke yake, basi ndio mnataka kutuambia hamna mpango wa kuzisahihisha? Au mnamaanisha kuwa zinakubalika? Na kama mna mpango wa kuzisahihisha, mnaona ni sawa tu kutumia mabilioni ya fedha kuchapa upya vitabu ambavyo tayari mmeingiza makosa lukuki na vimeshazamisha fedha nyingi? Je, na hivi mnavyosambaza au mlivyosambaza mtavirudisha na kuvitupa?

Tunaponya taifa au tunaliangamiza?
Uchambuzi mzuri
Tabu nyingine ipo vitabu hivyo hivyo kwa ngazi ya sekondari
Tatizo kubwa huko ni less contents
 
Wenye kazi zao wapo bize facebook.

Hii nchii ina Waziri wa Elimu.

Nikipata nauli nitahama hii nchi.

IMG_1494872993.231602.jpg
 
Sijui inakuwaje kitabu kinakuwa na error namna hiyo, maana mlolongo wa uandishi ni mkubwa,

Kuanzia kwa editor, reviewers ( on average wanakuwaga wa3) then publishing house nayo inakuwa na reviwer wake. after that mnunuzi wa kitabu (GoT) naye anakuwa na reviewer wake. mpaka kinachaguliwa kuwa kitabu cha kiada/ziada.

Pamoja na kuwa vitabu hivi vimechapishwa na serikali lakini mlolongo huo ulitakiwa ufuatiliwe, kwa kupenda cheap tumeingia gharama za bure za kuchapisha wakati zingeepukika kbs
 
Huo muhtasari wenyewe ni aibu tupu na umetiwa saini na waziri. Siku moja nilitaka kwenda wizarani kuonana na huyu mama lkn nilipofikiria ukiritimba wa nchi hii nikaona bora niache maana nitaonekana kichekesho cha kupigia mbuzi gitaa. Wallaj hatujajitambua bado. So pathetic
 
Watumishi wa taasisi hizo wamekuwa wakiteuliwa kwa kujuana,mtu anaetakiwa kuanda mtaala au kitabu lazma awe competent ,kwetu huku wanateuliwa kwa connection,kwanini huyu mtu ascopy na ku pest, tuna tatzo kubwa katika uteuzi wa wataalam
 
Sijui inakuwaje kitabu kinakuwa na error namna hiyo, maana mlolongo wa uandishi ni mkubwa,

Kuanzia kwa editor, reviewers ( on average wanakuwaga wa3) then publishing house nayo inakuwa na reviwer wake. after that mnunuzi wa kitabu (GoT) naye anakuwa na reviewer wake. mpaka kinachaguliwa kuwa kitabu cha kiada/ziada.

Pamoja na kuwa vitabu hivi vimechapishwa na serikali lakini mlolongo huo ulitakiwa ufuatiliwe, kwa kupenda cheap tumeingia gharama za bure za kuchapisha wakati zingeepukika kbs
Nadhani hii ni ishara wazi kwamba hawajafanya hayo hata kidogo.
 
Back
Top Bottom