Vita ya Malaria inapoendeshwa kibiashara zaidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita ya Malaria inapoendeshwa kibiashara zaidi

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Njaare, Oct 9, 2010.

 1. N

  Njaare JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Thursday, 07 October 2010 09:10 0diggsdigg


  [​IMG] Dismas Lyassa

  Na Dismas Lyassa
  KUNA msemo wa kiswahili usemao ‘katika safari ya mamba na kenge huwamo’...ikiwa na maana isiyo rasmi kuwa katika safari fulani, wakati mwingine hata wasiohusika nao huweza kuwemo.

  Ndicho kinachoonekana wazi, kwamba katika safari ya kupambana na malaria Tanzania, kuna wengi wanaifanya kibiashara zaidi. Wanaendesha kampeni hii ya malaria katika hali ya kutia kichefuchefu, kwamba hawana hata tone la haya dhidi ya mawazo yao machafu ya kuendesha biashara kupitia malaria, badala ya kusaidia jamii.
  Ukisikiliza redio au kuangalia televisheni na hata kwenye magazeti, matangazo dhidi ya malaria ni mengi, lakini kama ni mtu mwenye kutathmini vizuri, nafikiri utakubaliana na mimi kwamba kinachoendeshwa ni biashara zaidi, wala si wengi wenye huruma ya dhati ya kupambana na ugonjwa huo.

  Heri yetu mnaofanya haya mabaya, kumbukeni ya kwamba duniani tunapita, fedha na mali tutaziacha. Ni muhimu katika kufanya kazi kwetu, wakati mwingine tuwe na hofu ya Mungu, hasa ikizingatiwa kuwa wengi wetu tunajiita watu wa dini fulani, ambazo kwa ujumla zote zinakataza mambo machafu.
  Nafahamu katika makala haya watasoma wale ambao wanahusika na mikakati ya kibiashara ya kupambana na malaria, na wataisoma wale ambao kweli wana uchungu na nchi, lakini kwa vyovyote itakavyokuwa, unaruhusiwa kuichukuliwa kwa namna unavyotaka.
  Msingi wa Tanzania iliyo imara, pamoja na mambo mengine inatutegemea Watanzania wenyewe kusemana ukweli bila woga, kwani hata katika vitabu vitakatifu tunaelezwa ya kwamba woga ni dhambi. Kwa bahati nzuri hata katiba pia inaruhusu watu kusema yale wanayohisi si ya kukiuka katiba hiyo.

  Kuwaambia watu watumie vyandarua wakati hawana fedha ni sawa na kuwatukana, kwani nani anapenda kulala huku anaumwa na mbu? Naamini tatizo la Watanzania sio kwamba hawajui uzuri wa kutumia vyandarua, bali wengi hawana fedha.
  Kuendesha kampeni kwamba watu watumie vyandarua, ni jambo ambalo sio baya, lakini sio busara sana kama kuwasaidia Watanzania kwa kuua mbu.
  Kampeni ya sasa dhidi ya malaria, imekaa kibiashara zaidi, nafikiri kwa walio wengi watakubaliana na mimi dhidi ya hili. Kama kweli wanataka tuondokane na malaria, kipaumbele kingekuwa namna ya kupambana na mazalia ya mbu.
  Katika baadhi ya nchi duniani, hawajui mbu anafafanaje zaidi ya kuona kwenye televisheni au vitabu, je kwanini Tanzania tusiwaze jambo kama hili? Yote yanawezekana, shida kubwa ninayoiona ni kwamba hatuko katika kusaidia, tunawaza kuendesha mambo kibiashara zaidi.

  Tunaambiwa kwamba kuna vyandarua vina dawa inayodumu miaka mitano, sina la kusema, kwa wale wanaotumia vyandarua wana majibu sahihi juu ya hili.
  Tayari baadhi ya watu wameanza kulalamika hivyo vyandarua vinavyoelezwa kuwa vina dawa inayodumu kwa zaidi ya miaka mitano, wakisema mbu wanatua na kuwauma kama kawaida. Tufanyeje? Ni swali lisilo la jibu.
  Mwananchi mmoja alinukuliwa na gazeti moja akisema “Ni uongo mtupu! vyandarua vile havina dawa! Dawa gani inawekwa halafu mbu wanatua, hawafi na wanatuuma? Wasitudanganye bwana! Hii ni danganya toto!”.
  Binafsi ninaposikia matangazo ya kupambana na malaria, huwa natamani kuzima radio au televisheni kwa sababu kwa namna ninavyoona roho inauma, ni biashara zaidi kwa mtazamo wangu, ingawa kwa mwingine anaweza kuona ni tofauti kwa sababu zake binafsi.

  Miongoni mwa vyandarua vinavyolalamikiwa ni pamoja na vile vinavyotolewa na serikali chini ya mpango wa hati punguzo, na kutolewa kwa wananchi kwa bei ya Sh500 kwa kinamama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.

  Ndio nasema ni vizuri, serikali na watu wengine kwa ujumla tukatafakari kwa makini vita dhidi ya malaria, kwani kwa hali ilivyofikia sasa, wengi wanaona ujanja ni mwingi kuliko vita halisi.

  Ofisa Mawasiliano wa Kitengo cha Vyandarua katika Mpango wa Taifa wa Kupambana na Malaria (NMCP), Susan Omari anasema vyandarua hivyo huua mbu aina ya Anopheles ambaye ni wa malaria lakini wa cullex hawafi kwa sababu tayari wamejijengea usugu ingawa awali walikuwa wanakufa.

  Kama hilo ndilo jibu, kwanini baadhi ya watu wanalalamikia kuwa na malaria licha ya kutumia hivyo vyandarua...ni mambo ambayo nafikiri Watanzania tunapaswa kuyaangalia kwa makini.
  Takwimu za malaria zilizotolewa na NMCP zinaonyesha kwamba watu kati ya 10 milioni hadi 12 milioni, sawa na robo ya Watanzania wote huugua malaria kila mwaka na kati yao, 60,000 hadi 80,000 hufariki, wengi wao wakiwa ni kinamama wajawazito na watoto walio na umri chini ya miaka mitano.

  Mikoa inayoongoza nchini kwa kuenea malaria nchini ni Kagera, Lindi, Mtwara, Mwanza, Mara, Shinyanga, Ruvuma na Pwani.
  Je ni sahihi katika uzito kama huo kampeni dhidi ya malaria kuendeshwa kwa mchezo? Jibu ni hapana. Ni lazima tuwe na mikakati dhabiti ya kuhakikisha yeyote ambaye yuko kwenye vita hivi, anafanya jambo ambalo kweli linakuwa na msaada kwa ustawi wa jamii.

  Badala ya watu kushindwa kufanya kazi, badala ya watu kuumwa kwa malaria nk, ni vizuri serikali na asasi au mashirika yenye kuhusika katika vita hii, wakaifanya kwa ustadi ili tuweze kuwa na taifa ambalo litatumia nguvu na akili nyingi katika kufanya mambo mengine ya maana hasa katika suala zima la kuinua uchumi.
  Ndugu zangu haya ni madai, kwa maana hiyo ni vizuri tukayafanyia utafiti hasa kwa wale ambao wanalalamikiwa kuendesha vita hivi vya malaria kibiashara, kama wataona kuna ukweli aidha kwa bahati mbaya au kusudi, ni vizuri wakaangalia namna ya kuachana na tabia hii, badala yake mikakati ilenge kuondoa tatizo hili ambalo kwa hakika lina athari kubwa kwa uchumi wa tanzania.
  Dismas Lyassa ni mwandishi wa makala gazeti la Mwananchi, globalsourcewatch@gmail.com

  Source: Mwananchi 7th Oct. 2010  Naona makala hii imekaa vizuri. Wenye uwezo waache kuchezea afya za watu na amani yao. Hela inayotumika kwenye matangazo na matamasha itumike kuharibu mazalia ya mbu.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Ndefu kweli hii lakini safi
   
 3. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mpaka tusubiri hisani ya watu wamarekani tumebakiza kunanihii tu na ...................wke nako watuwekee mabango yao nnfyuuuuuuu
   
 4. minda

  minda JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  ni kweli maelezo yanayotolewa kuhusu hizo neti ni tofauti kabisa;

  • mbu wananigonga kama mwanzo licha ya kuambiwa wanakufa
  • mbu anaishi ndani ya neti (kwa majaribio!!!) muda wowote utakaoamua mpaka umuue!!!
   
 5. minda

  minda JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  ikumbukwe vita hivi vilianza kwa sugu kuporwa dili na hao jamaa wanaozoea kupata tenda za jengo kuu, kama walivyofanya jana usiku kwenye bd ya mkuu wa jengo kuu
   
 6. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kuna athari ya hali za Wananchi wengi zikawa ngumu zaidi miaka ijayo ikiwa kama mwenendo wa utendaji kazi wa wajasirimali na wafanya biashara, ni udanganyifu, dhuluma na Hiyana. Mundo na Chauro walivodokeza, ingawa naona watu wa nje (misaada) hawatoweza kutengeza bila wananchi wenyewe kuwa mbele. Hiyo misaada imekua ikishuka toka enzi za Nyerere, hali ndio inazidi kuwa mbaya. Ukipata nafasi soma hii nakala Foreign aid is fuelling poverty « JamiiForums|TMF Blogs . Wakati mungine najiuliza, je Na hao wanaotoa misaada, mbona hua hawaangalii real situation,. Inawezekana wote wezi. Kwa sababu ubadhirifu na wizi wa mali ya uma uko sehem zote duniani. Ila kuna serikali ambazo zimedhibiti kiasi kukubwa.

  Mnaoaje kwa mfano, Iwepo sheria kua, Project yoyote ambayo inahusisha mali ya uma, lazima iwe audited katika na mwisho wa project. Na comitee ya kuoditi iwemo watu katika Jamii. Nadhani itasaidia kurudisha uamifu kati ya serikali na jamii.
   
Loading...