Vita ya kunyamaziana kwenye mahusiano

Vita ya kunyamaziana kwenye mahusiano

Nampendamilele

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2024
Posts
387
Reaction score
547
Habari za usiku

Mimi napitia changamoto ya kimahusiano. Tumenyamaziana na mwanaume niliyekuwa na mahusiano hii ni week ya 4.

Kusema ukweli sina kosa lolote nililolifanya ila ni yeye ndio alikuwa na vitu alipaswa kuniambia (siwezi kuviweka hapa maana mhusika anaweza kuwa humu)

Nilijipa siku 3 za kujipendekeza kumtafuta kila siku ni mimi naanza nilivyomaliza hizo siku 3 nikauchuna; huwezi amini na yeye akakaa kimya ni ku-view status na ku-like. Hakuna kuongeleshana

Sihitaji kumtafuta.. na kama hatonitafuta nitafanya maisha yangu

Sasa nauliza; tumeshakaa mwezi hatuongeleshani - je naweza kuanzisha mahusiano mapya au bado mapema?
 
Kuna mdada mwingine kwenye confession page alisema aliachana na wanaume wa 3 tofauti, hawakugombana, ila tu ni ile silent treatment, mtu anajiona akimtafuta mwenzake atakuwa anajishusha, mwishowe uhusiano unakufa.

Mahusiano mengine mengi ya sasa, hamna anayetaka kuonekana mnyonge kwenye mahusiano, mnaweza mkawa wote moyoni mnapendana, ila kuonesha upendo ndo kipengele, mwishowe mahusiano yanakufa, mnabaki single.

Watu wengi wanataka kuoneshwa upendo, ila wao kuonesha upendo ni kipengele
 
Kuna mdada mwingine kwenye confession page alisema aliachana na wanaume wa 3 tofauti, hawakugombana, ila tu ni ile silent treatment, mtu anajiona akimtafuta mwenzake atakua anajishusha, mwishowe uhusiano unakufa..

Mahusiano mengine mengi ya sahivi, hamna anaetaka kuonekana mnyonge kwenye mahusiano, mnaeza mkawa wote moyoni mnapendana, ila kuonesha upendo ndo kipengele, mwishowe mahusiano yanakufa, mnabaki single.

Watu wengi wanataka kuoneshwa upendo, ila wao kuonesha upendo ni kipengele
Kuna kitu kilitokea mkuu then hajakisolve wala kusema chochote a naongea na mimi kama vile Hakuna kilichotokea

Mimi kumtafutaa ni kama kujipendekeza ni kama hanitaki tu
 
Back
Top Bottom