Vita Ya Chadema Na CCM: Tafsiri Yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita Ya Chadema Na CCM: Tafsiri Yangu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Jun 9, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Jun 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  [FONT=&quot]Ndugu zangu,[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot]NIONAVYO, kuna upepo mgumu wa kisiasa unaovuma sasa kwenye nchi yetu. [/FONT][FONT=&quot]Ndio, upepo mwingine ni mgumu wenye kutingisha matawi ya miti na hata makoti tuyavaayo. Kamata-kamata hii ya sasa na matumizi ya nguvu ni ishara za upepo mgumu wa kisiasa unaovuma. [/FONT]
  [FONT=&quot]Hii ni nchi yetu. Tunaipenda nchi yetu tuliyozaliwa na ndio maana ya kuyaandika haya. Na naamini, kuwa msingi wa haya tunayoyaona ni mapambano ya vyama na makundi katika kuwania kushika mamlaka za dola. [/FONT]


  [FONT=&quot]Na katika upepo huu mgumu wa kisiasa uvumao sasa, ni vema tukaongozwa na busara badala ya kuruhusu kuongozwa na hisia zetu. Tufanye hivyo kama kweli tuna mapenzi ya dhati kwa nchi yetu tuliyozaliwa. Maana, tukionacho sasa ni kazi ifanywayo na baadhi ya wanasiasa ya kupandikiza chuki miongoni mwetu. [/FONT]


  [FONT=&quot] Na tusiombe chuki hii ikaachwa ikomae, maana, sote, kwa njia moja au nyingine, tutalipa gharama ya ujinga huu wa wanasiasa wa kutanguliza maslahi yao binafsi, ya vyama na makundi yao badala ya yale ya nchi yetu tuliyozaliwa.[/FONT]


  [FONT=&quot]Na katikati ya upepo huu mgumu wa kisiasa uvumao sasa tunauona mpambano mkali baina ya chama tawala – CCM na chama kikuu cha upinzani – Chadema. Siasa sasa inafanywa kuwa uhasama badala ya kuwa nyenzo ya kidemokrasia katika kuiendeleza nchi yetu. Katika nchi zetu hizi, na katika upepo huu wa mabadiliko, Serikali ya chama tawala Afrika haina maana ya Serikali inayoongozwa na watendaji wote walio wanachama au wafuasi wa chama tawala.[/FONT]


  [FONT=&quot]Hivyo basi, katika mpambano huu, tunaona, kuwa chama tawala, kwa namna moja au nyingine kinapotumia dola katika kuikabili Chadema kinaongeza nyufa za kiuongozi. Huu ni mkakati wa kimakosa na wa hatari sana. Na Mwana-CCM yule Fredrick Sumaye aliyesomea masuala ya Utawala kule Havard Marekani alipata kukitahadharisha chama chake, kuwa kisitumie Serikali kwa maana ya dola kujibu hoja za Chadema, badala yake, CCM ipambane na Chadema kwa hoja za kisiasa majukwaani. Sumaye alikuwa na hoja ya msingi, sina hakika kama wenzake kwenye CCM walimwelewa ipasavyo.[/FONT]


  [FONT=&quot]Ndio, tuko sasa kwenye mapambano ya kisiasa ya vyama yenye ushabiki mkubwa bila misingi ya hoja za kisiasa na kutanguliza maslahi ya nchi. Na Afrika ukikuta jogoo wawili wanagombana, basi, hapo hapakosi mashabiki. [/FONT][FONT=&quot]Na kila shabiki aliyesimama kutazama mpambano wa majogoo hao, ujue, kuwa ana jogoo wake anayemshabikia. Na jogoo anayemshabikia akishindwa pambano, shabiki ataondoka akisononeka. Kuna ambao watakosa hata hamu ya chakula siku hiyo. Kisa? Jogoo wake kagalagazwa![/FONT]
  [FONT=&quot]
  Na kama jogoo mmoja ni mnene na mwingine ni mwembamba, ujue, kuwa jogoo mwembamba ana mashabiki wengi. Lakini mie ni mmoja kati ya wachache, ambao, kwenye pambano kama hilo, hujitahidi kusimama katikati, hata kama ni kazi ngumu. Nawasilisha.[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]
  Maggid,[/FONT]
  [FONT=&quot]Dar es Salaam, Juni 9, 2011.
  MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
  [/FONT]
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Jun 9, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Enzi zetu tulikuwa tunaita "ushabiki maandazi."
   
 3. nyengo

  nyengo JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 433
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35

  Hii si vita ya CCM na CHADEMA hii ni uonevu wa nguvu za dola za CCM zidi ya wasio na dola(CHADEMA). Hii sio fair vita sababu CHADEMA wanatumia hoja na CCM wantumia nguvu za dola na sio hoja za kisiasa
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Maggid, nimeipenda hii sehemu ya mwisho!
   
 5. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Vita ipo wapi? Liambie jeshi la police lifanye kazi yake kwa mujibu wa katiba Kulinda usalama wa raia na malizake
  Polisi inapotumiwa na CCM yaana yake nini? kuna democrasia? Raia tumechoka ipo siku tutajibu mapigo ndio watuelewe
   
 6. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wenye masikio na akili tumekusikia na kukuelewa.


  Ishia hapo hapo....

  kama jogoo mdogo ana watu wengi, basi waliobaki lazima watakuwa upande wa jogoo mkubwa
   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Tatizo lako Maggid unapenda watu wasome mawazo yako tu humu lakini wewe hupendi kujifunza au kuchangia mawazo ya wenzako, na ndio maana sijawahi kukuona kwenye thread yoyote humu ukishiriki kwenye mijadala mizito, huo unaitwa ubinafsi.

  Hii ni changamoto tu nakupa, hii ni tafsiri yako lakini zipo tafsiri za watu wengine humu, soma thread ya William Malecela @New York, amelielezea vizuri sana hili leo hii.

  My opinion: Je serikali ya CCM iko serious kweli au ni kiini macho tu?
   
 8. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  I hope unamaanisha jogoo mwembamba ni chadema.
  Pia, Majidi
  Umelitumia neno chuki, ukimaanisha kwamba ccm wanapandikiza chuki
  dhidi ya chadema na chadema wanapandikiza chuki dhidi ya ccm na serikali yake.

  Toka mwaka 2007 wakati wanaanza operations sangara walidai
  msingi wa operations hizo ni kusambaza sumu ya chuki kwa wananchi dhidi
  ya ccm na serikali yake, wamefanikiwa sana katika hili, sasa wananchi
  wanaichukia ccm na serikali yake sana, wanawachukia wote, viongozi
  wa ccm na wale wa serikali, sababu wamejulishwa na chadema
  kwamba ni wao ndio chanzo cha umasikini wao wa kiuchumi, shida na
  mapungufu yote katika maisha yao ukilinganisha na hali ambayo
  walipaswa kuwa nayo kutokana na rasilimali tulizonazo.

  Nimetoka kwenye daladala moja masaa matatu yaliyopita,Konda
  kamuita mama mmoja abilia, mama akakataa kwamba daladala haina
  seat, konda akamuonyesha seat, mama akapanda, kavaa kanga za ccm,
  ameipata fresh kwenye daladala, konda alimuambia, hiyo kanga uliyovaa
  ndio chanzo cha matatizo niliyonayo mimi nabado nakuita kupanda
  daladala japo nipate pesa ya kula unaniletea malingo nimekukosea nini
  mama? Mama:Kivipi? Konda: we hiyo kanga si ndio ilikufanya ukawapigia
  ccm kura? mama:Kimya, Konda: sasa umetuweka wote kwenye dimbwi la
  umasikini, Abilia: Muambie muambie,

  Kama ni kweli CCM na serikali yake vinamikakati ya kupambana na
  Chadema basi ni kweli kabisa mwisho wao umefika, they are shooting
  to the wrong goal.
   
 9. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  siku zote tunajua uko upande wa jogoo anayejivimbisha(sio mnene) na usivyo na busara unaonyesha usivyoweza kuwa hakimu mzuri.
  jogoo mkubwa siku zote anataka mitetea wote waliopo duniani apande yeye na ukikuta ugomvi wowote kati ya jogoo wawili ujue yule mdogo alitaka kutimiza haki yake ya kimaumbile ya kupanda walau mara moja kwa siku,ila kwa sababu ya ubabe na tamaa hajui kama akiachiwa anawez kuchukuliwa na upepo.
  ccm kama mfano wako wa jogoo tumewaachia mitetea wote kwa miaka hamsini matokeo yake wamewaaambukiza ugonjwa usio na tiba wala kinga wa umsikini.
  sasa kwa upofu wako unaona kama chadema ni jogoo mwembamba.
  umekosea ni jogoo kijana.
  msubirie huyo jogoo mkubwa 2015 uone kama hata nyama yake hata fisi hawaitamani.
   
Loading...