VITA VILIVOCHUKUA MUDA MFUPI DUNIANI

yussufhajj

Member
Mar 24, 2016
27
8
Vita hivi vilipiganwa mwaka 1896 kati ya Utawala wa kifalme wa visiwa vya Uengereza na Utawala wa kifame wa visiwa vya Zanzibar.

Sababu kuu ya vita hivi ni mgogoro wa madaraka uliotokea Zanzibar 25/Agosti/1896 baada ya kufariki kwa sultan hamad bin thuwayn ambapo khalid bin barghash na hamoud bin Mohammed walianza kugombaniana ufalme .
Utawala wa visiwa vya Uengereza ulikua ukimpendelea bwana hamoud bin Mohammed awe mrithi wa kiti hicho cha ufalme .
lakn bwana khalid bin barghash aliuchukua ufalme kwa nguvu hali iliofanya Uengereza kutangaza vita na Zanzibar na kutuma kikosi chake cha maji (royal navy).

Ilipofika Asubuhi ya tarehe 26 Agosti 1896 saa tatu vikosi vya Uengereza vilianza kushambulia na bwana khalid bin barghash akakimbilia ofisi ya ubaloz wa ujerumani.

Vita hivi vilidumu kwa dakika 45 na vimeingizwa katika kitabu cha world gueness book
 
sasa kama imeingizwa kwenye world records za guiness kwa nini umeileta kama tetesi?
 
Kuna mambo sijaelewa moja zanzibar wakati huo ilikua chini ya colon la nani?

Ujerumani ilikua na ubalozi wake zanzibar?

Vita vilianza 25/08 na kuisha 26/08 yet unasema vilidumu dakika 45????
 
Zanzibar na omani zilikua na sultan mmoja,aliekuwa na makao yake zanzibar kama sikosei
 
Kuna mambo sijaelewa moja zanzibar wakati huo ilikua chini ya colon la nani?

Ujerumani ilikua na ubalozi wake zanzibar?

Vita vilianza 25/08 na kuisha 26/08 yet unasema vilidumu dakika 45????


trhe 25 ni kifo cha mfalme na trhe 26 ndio vita vyenyewe .
zanzibar hadi wakati huo haikua imetawaliwa ila ilikua ina maeneo ilio tawala . uengereza,marekani na ujerumani zote zilikua na ofisi za ubalozi zanzibar . ikulu ya zanzibar ya sasa ni jengo la ilokua ofisi ya balozi ya uengereza.zanzibar ilianza kuwa koloni la uengereza wakati wa sultan ally
 
Back
Top Bottom