Vita sasa ni Mbowe na Slaa

Vita sasa ni Mbowe na Slaa

hii habari changanya hizi akili

'Kitendo cha Uhaini – Vince Flynn
Nilishauriwa kusoma riwaya maana zina mafunzo mengi sana. Huwa nasoma zaidi vitabu vya kitaaluma na kitafiti na mara chache sana huchukua riwaya. Mwaka huu nimezisoma nyingi mpaka sasa kuliko vitabu vingine. Katika vitabu Kumi na Tatu ambavyo nimesoma toka mwaka uanze, nane ni riwaya. Mwanzoni mwa mwezi huu nilisoma riwaya ya Act of Treason: Can he take out the enemy within? Iliyoandikwa na mwandishi maarufu Vince Flynn na kupigwa chapa na kampuni ya Simon and Schuster.
Mitch Rapp mpelelezi mahiri anapewa kazi ya kupeleleza tukio la kigaidi lililofanyika ndani ya Marekani na kumlenga Mgombea Urais wa nchi hiyo Josh Alexander. Shambulizi hilo lilimwua mke wa mgombea huyo. " juu juu shambulizi lilionekana ni kazi ya al-Qaeda". Zilikuwa zimebaki wiki mbili tu kabla ya uchaguzi mkuu wa Marekani shambulizi hili lilipotokea. Mgombea Alexander alishinda kwa kura za huruma. Uchunguzi ulipoendelea ulikuta ushahidi ambao ulishtusha. Ilibidi kukamilisha uchunguzi kabla ya Rais mpya kuapishwa.
Mgombea mwenza wa Alexander akiitwa Mark Ross alikuwa seneta na mtu mwenye nguvu sana. Alikuwa akipenda sana madaraka na uteuzi wake wa kuwa mgombea mwenza ulitokana na ushawishi mkubwa kwa mgombea kutoka kwa watu wenye nguvu waliobobea katika siasa za Washington. Ross alikuwa na mtandao mpana wa watu wakiwemo wenye rekodi za makosa ya kijinai. Mmoja wao Bwana Green alikuwa na makosa ya kutorosha fedha nje ya Marekani na alikamatwa na FBI na kukimbia hivyo kuhukumiwa akiwa nje. Bwana Green alitoa msaada mkubwa kwenye kampeni kupitia Ross ili apewe msamaha wa Rais. Kawaida nchini Marekani Rais anayemaliza muda wake hutoa msamaha kwa watu waliohukumiwa na mara kadhaa anayeingia hupendekeza majina yake kwa anayemaliza ili wapewe msamaha. Bwana Green ambaye sasa alikuwa anaishi nchini Uswiss alitegemea msamaha huu.
Siku ya shambulio mkuu wa kampeni za Urais Bwana Garret alimbadili mlinzi wa Makamu wa Rais na kumfanya kuwa mlinzi wa mke wa mgombea Urais. Pili alibadili mfuatano wa magari na kumtoa mke wa mgombea wa uRais katika gari la Rais na kumweka katika gari yake peke yake nyuma ya mgombea mwenza. Dakika tano baada ya msafara ule kuondoka bomu likalipuka. Mlinzi Mkuu wa mgombea Urais, mwanamama aliyekuwa anakua kwa kasi sana katika CIA akawekwa kwenye wakati mgumu sana na kuwa mwisho wa kazi yake. Kila uchunguzi ukionyesha kuwa Al Qaeda wamefanya kazi hiyo na Mlinzi bibi Rivera alizembea kazi.
CIA walipata picha za ngono zinazomwonyesha mke wa mgombea Urais bibi Jillian Alexander akifanya mapenzi na mmoja wa walinzi wa msafara wa kampeni. Wapinzani wao walizipata mapema lakini waliona sio vema kuzitumia katika kampeni. Hata hivyo picha hizo zilitumiwa na mpelelezi Mitch Rapp na kugundua haswa kiini cha shambulizi lile. Uchunguzi wake ulimfikisha nchini Cyprus na kumkamata mtu aliyelipua bomu lile na baada ya mapigano Mitch alimzidi nguvu na kumtia nguvuni Bwana Gazich. Uchunguzi wa nyaraka za kibenki ulimpeleka Mitch mpaka Uswiss na kuhusisha moja kwa moja Bwana Green aliyekuwa anaombewa msamaha na makamu wa Rais mteule.
Hatimaye CIA wakagundua kuwa shambulio lile lilifanywa na Makamu wa Rais mteule kwa msaada bwana Green aliyemkodi mlipuaji wa bomu. Katika kuhangaika ukweli usijulikane bwana Ross alianza kutumia vyombo vya habari kupaka matope CIA. Alitumia hususan gazeti la The NewYorkTimes, mhariri wake na mwandishi wake kumpa taarifa za ndani kuwa CIA wamemkata mtu asiyehusika katika shambulio lile. CIA hawakutetereka maana walikwisha kusanya ushahidi wote ikiwemo safari ya ghafla ya msaidizi wa Bwana Ross jijini Geneva katika kujaribu kuficha ukweli wa mambo.
Siku ya mwisho ya utawala wa Rais anayeondoka madarakani, Bwana Ross aliomba miadi ya kumwona Rais ili aweze kutoa msamaha kwa bwana Green. Mkurugenzi Mkuu wa CIA alichukua fursa hiyo kuweka sumu kwenye chai ya makamu wa Rais mteule na akafa pale pale Ikulu kwa kilichoitwa ugonjwa wa moyo. Mkurugenzi Mkuu wa CIA alinukuliwa akisema kumwua makamu wa Rais mteule ilikuwa ni kazi bora zaidi ya kizalendo aliyowahi kufanya katika maisha yake yote ndani ya taasisi hiyo.
Wakati wananchi wote wa Marekani waliaminishwa kuwa Al Qaeda ndio walishiriki shambulio lile, uchunguzi wa CIA uligundua ilikuwa kazi ya mtu wa ndani sana, namba mbili katika Serikali mpya iliyokuwa inaingia madarakani. Hakuna mtu mwenye akili ya wastani angeweza hata kuhisi kwamba mgombea umakamu wa Rais angepanga kumwua mke wa mgombea Urais wake. Act of Treason ni kitabu cha aina yake. Licha ya ukubwa wa wastani, nilitumia siku mbili kukimaliza. Sikukiweka chini mpaka nilipokimaliza. Mafundisho yake ni dhahiri.'
 
Ndege wanaofanana huruka pamoja, Aliyetoa post na wengi wao waliochangia Wanakubali Rushwa, Escrow, Dhuluma, umaskini ta tanzania, elimu ya kuokoteza, hawana jipya wanalotaka, SAME LEVEL OF THINKING CAN NOT MAKE CHANGES.....
 
Yaani Gazeti hili ukienda ukurasa wa tatu utakuta elimu ya unajimu,kisha jinsi ya kujiunga na Freemasons mwisho kwenye habari za michezo wanajadili taulo alilotundika kipa wa Simba siku ya Mechi ya Simba na Yanga

Bother Ben,
Hakuna namna Viongozi wa CHADEMA wanaweza kufungulia mashitaka gazeti hili?
Binafsi ninaona wamedhalilishwa kwa picha, uhalali au ukweli wa maneno ni jambo jingine.

Ni mawazo yangu.
 
yuko wapi sasa huyo nyerere wako??

alitukomesha sisi au alijikomesha yeye mwenyewe??

yule mchongameno nuksi saana

yeye alidhan dunian hapa angeish milele??

haya yuko wapi sasa??

kila mtu hapa dunian atakufa tuh utake usitake

TENA YEYE NYERERE NI KAFIRI HUKO ALIKO JEHANNAM INAMUUNGUZA VIZUR SANAA

NA IZID TUH KUMUUNGUZA.

NA WEWE UKIFA TUH INAKUSUBIR KAFIR MKUBWA WE..!!

Mkuu acha jazba! Itatoka haitoki?
 
Yaani Gazeti hili ukienda ukurasa wa tatu utakuta elimu ya unajimu,kisha jinsi ya kujiunga na Freemasons mwisho kwenye habari za michezo wanajadili taulo alilotundika kipa wa Simba siku ya Mechi ya Simba na Yanga
Daa, jamani mtuhurumie sisi tulio kwenye taaluma hiii!
 
Mbowe anataka kuchukuliwa fomu ya kugombea Urais na wazee wa Mwandiga Kigoma
 
Vita hii babu anaweza kuikimbia mapema kabisa sijui kama atamudu.
 
Slaa ataitwa msariti siku si nyingi huwezi kumpiga chini mkwe wa mwenye chama.
 
Propaganda nyingine hazina hata mashiko
Huku ni kujitia hasara kwa kumaliza wino kwenye hako kakampuni kenu uchwara tu
 
View attachment 235291

Sasa mambo ni hadharani. ILE vita ya Urais wa 2015 iliyokuwa ikipiganwa kati ya Viongozi Wakuu wa Vyama vya siasa nchini vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi, maarufu kwa jina la UKAWA, sasa imehamia kwa MAFAHALI wakuu wawili ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Mwenyekiti wa chama hicho , FREEMAN MBOWE anataka kugombea Urais wa 2015 kwa tiketi ya chama chake kwa udi na uvumba.

Uamuzi wa MBOWE na Wapambe wake kutaka kumuweka kando Dr. SLAA umejengwa katika misingi mitatu:

1. Ujana wa MBOWE ukilinganisha na Dr. SLAA
2. DHEHEBU lake la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT
3. Uzee na hali ya afya ya Dr. SLAA ambayo inaelezwa kudorora siku hadi siku kadri siku za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015 zinavyokaribia.

Tayari vyama viwili kati ya vinne vinavyounda UKAWA , CUF na NCCR-MAGEUZI vimekwisha kumtangaza mgombea wake wa Urais ambapo CUF wamemtangaza Prof. IBRAHIMU HARUNA LIPUMBA na NCCR-MAGEUZI wamemtangaza Dr. GEORGE KAHANGWA ambaye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Hadi sasa CHADEMA na NLD bado hawajawatangaza wagombea wao tayari kuingia kwenye KAPU la UKAWA na wale wa CUF na NCCR ili kumpata mgombea mmoja atakayeshindana na mgombea wa CCM.

Taarifa zaidi zinasema shinikizo la kumtaka Mbowe agombee kupitia MBOWE linatoka katika makundi makuu mawili ambayo ni

1. Waumini wa KKKT
2.Wafanyabiashara wanaotoka Ukanda wa Kaskazini wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Kwa kawaida jamii ya Mkoa wa Kilimanjaro imekuwa ikiishi katika matabaka mawili yenye misimamo isiyoingiliana kuanzia kwenye mila , desturi na tamaduni zao.

Kwa mjibu wa Mbunge mmoja wa Chadema, matabaka hayo ni ya wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro wanaoishi Ukanda wa kaskazini kwa upande mmoja ambao unatamabulika zaidi kwa jina la CHAGALAND, na wananchi wanaoishi ukanda wa chini au wa kusini , ambao ni jamii ya WAPARE.

IMEELEZWA kwamba wafuasi wengi wa Chadema katika Ukanda huo wa kaskazini , ambao wengi wao ni waumini wenza wa MBOWE katika dhehebu la KKKT , wangependa kuona safari hii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitokana na Kanisa hilo.

Kundi la pili la Wafanyabiashara walioko nyuma ya Urais wa Mbowe , ambao wana asili ya Ukanda wa Kasakzini mwa Mkoa wa Kilimanjaro inasemekana wamekuwa ni chachu ya Nguvu ya ksiasa iliyonayo CHADEMA kwa sasa kutokana na michango ya ufadhili wa hali na mali kitoka katika jamii hiyo.

Hivyo wafanyabiashara hao wa kutokea ukanda wa Kaskazini mwa Mkoa wa Kiliamnjaro wangependa kuona Juhudi zao za kukifhadhili chama zinazaa matunda kwa kumuwezesha Mh. MBOWE kuwa mgombea urais hasa ukizingatia kuwa ni mtu kutokakatika UKANDA ambao wanatokea.

Chanzo: TAZAMA Tanzania.

Haya magazeti mengine vioja kweli. Hvi yana mhariri kweli au mwandishi wake na mhariri ni Nape?
 
Umekurupuka wewe!!!!,unatuonyesha pic ya TAZAMA ,then baadae eti chanzo ni TANZANIA DAIMA,una udini wakati huu sio wakati wa kujadili udini!!,KAMA HATUJUI KUSOMA Hata picha hatuoni kweeeli?
 
Back
Top Bottom