Vita kati ya Seif na Hamad Rashid yaibukia Manzese

KING COBRA

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
2,782
864
Leo saa tatu Hamad Rashid anafungua tawi jipya la Cuf Manzese karibu na mtaa wa Kosovo.

Seif katoa order kwa Mtatiro kuzuia. (STF) watatumwa hapo

UPDATED 12, Dec 2011:

MAMBO si shwari ndani ya Chama cha Wananchi (CUF), baada ya mabounsa wa chama hicho kuvamia mkutano wa Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed, kufanya vurugu na kumwondoa mbunge huyo kwa nguvu.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Hamad Rashid mwenyewe, zinaeleza kuwa tukio hilo lililotokea jana kwenye ofisi ya CUF Kata ya Manzese jijini Dar es Salaam.Vurugu hizo zimekuja kipindi ambacho mbio za kuwania nafasi ya Katibu Mkuu wa chama hicho zikiwa zimeshika kasi.

Hamad Rashid

Akizungumzia vurugu hizo ambazo zilitokea saa 4:00 asubuhi, Hamad Rashid alisema yeye alifika katika eneo hilo baada ya kupata mualiko kutoka Ofisi za CUF Wilaya ya Kinondoni."Mimi nilikuja kufuatwa nyumbani na viongozi wa wilaya ili niende kutoa msaada wa viti na meza kutokana na kuwepo upungufu wa vifaa hivyo katika ofisi za eneo hilo," alisema Rashid.

Alisema kabla ya kumaliza kuzungumza na wanachama wa Kata ya Manzese, walitokea vijana wasiojulikana na kuanza kufanya vurugu zilizomlazimu aondoke katika eneo hilo.

Mbunge huyo ambaye aliwahi kuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni katika bunge la Tisa, alisema msaada huo ni moja ya nia yake ya kutaka kutangaza nia ya kugombea nafasi ya Katibu Mkuu wa CUF.

Akawataka wanachama kuwa makini katika kipindi hiki alichoeleza kuwa chama hicho cha upinzani kimeanza kudhoofika na kinaonekana kupoteza nia ya kushika dola.

"Chama (CUF) kwa sasa kimekuwa hakina meno kutokana na kufifia kwa vuguvugu. Siasa za sasa ni ujasiri, nataka kugombea uongozi ili nionyeshe ujasiri wangu katika kukiokoa chama chetu kitoke hapa kilipo," alisema Rashid.

Alisema chama hicho kwa sasa kimekosa mvuto wa kisiasa kutokana na mfumo wa uongozi uliopo baada ya Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad kuonekana anafanya zaidi shughuli za kiserikali badala ya chama.

"Tunahitaji kufanya mabadiliko ya katiba ndani ya chama. Haiwezekani katibu mkuu ambaye ni mtendaji mkuu wa chama awe na madaraka makubwa ambayo yanamfanya ashindwe kufanya kazi ipasavyo ndani ya chama," alisema Rashid.

Aliwataka wanachama kukataa chama kufanya kazi za kinafiki kwani uamuzi unaonekana kutolewa na watu wachache na sio wanachama wote.

Mtatiro

Alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro alisema ofisi yake haikuwa na taarifa na mwaliko wa Mbunge huyo anaenda kutoa msaada katika kata ya Manzese na kama amefanya hivyo, sio ratiba ya chama ni ratiba yake binafsi.

"Hiyo taarifa ya Hamad Rashid alikuwa Manzese ndiyo kwanza naipata kwako, japokuwa hatuna utaratibu kama huo kiongozi mkubwa kama yeye atembelee kata bila taarifa. Niseme tu alichokifanya ni kinyume na taratibu za chama chetu," alisema Mtatiro.

Alisema utaratibu wa chama hicho ni kiongozi kutoa taarifa kama anaenda kutembelea sehemu fulani ili aweze kuandaliwa ulinzi katika eneo husika.

Mtatiro alisema watu waliofanya vurugu eneo la Manzese hawajatoka makao mkuu, kwani hajaona ratiba yoyote inayoonyesha kamati ya ulinzi ya CUF kama ilikuwa Manzese jana.

Alisema chama hicho kina ulinzi mpaka ngazi ya matawi, hivyo inawezeka vijana hao wakatoka katika kata husika. Walifanya hivyo baada ya kutokuwa na taarifa ya ziara yake na kugundua ameenda kinyume na utaratibu wa chama.

Lakini alipotakiwa kuzungumzia kuhusu suala la kutoa taarifa makao makuu, Hamad alisema "sio lazima kila kitu makao makuu wajue, kwani jukumu la kupeleka taarifa ya ujio wake lilikuwa ni la ngazi ya wilaya iliyomwalika.

"Sio kila kitu ninachokifanya wapate taarifa makao makuu. Mpaka sasa hivi nimeshafanya shughuli nyingi za kichama bila taarifa tatizo lao wanapenda kuyafanya mambo madogo madogo kuwa makubwa uongozi wenyewe sasa hivi haujielewi," alisema Rashid.

Awali, Kaimu Katibu wa Kata ya Manzese wa CUF Hamdani Ngurangwa alisema anashangazwa na vurugu hizo, kwani taarifa ya ujio wa kiongozi huyo katika kata yake kwa ajili ya kukabidhi viti na meza, zilifika ofisini kwake wiki moja kabla na alizipeleka katika ofisi ya mkoa.

"Taarifa hizi za Mheshimiwa Hamad Rashid alizileta mapema na tulizipeleka katika ofisi za CUF wilaya, lakini jibu tulilolipata lilitushangaza kidogo," alisema Ngurangwa.

Alisema taarifa ya kiongozi wa wilaya ilidai kuwa kutokana na agizo la makao makuu, viongozi hao hawatakiwi kushirikiana Hamad kwa jambo lolote katika ujio wake.

"Nilishindwa kutii agizo hilo kutokana na kutokuwa na barua ya maandishi kutoka makao makuu. Ndio maana nilimwalika mbunge huyo kuendelea na shughuli zake,"alisema Ngurangwa.

Hivi karibuni kumekuwepo mvutano wa chini kwa chini wa viongozi ndani ya chama hicho, ukihusishwa na kuwania nafasi ya ukatibu mkuu na uenyekiti wa chama hicho.

Baadha ya wanachama wanadai kuwa Maalim Seif na Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa ibrahim Lipumba ambaye hivi sasa yupo nje ya nchi kikazi wamekifanya chama hicho kukosa mvuto hususna Tanzania bara.

Maalim Seif baada ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa aliteuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Hata hivyo, mabadiliko ndani ya chama hicho yanazuia na viongozi hao wa juu wakidai kuwa wanaotaka mageuzi ya uongozi wanavunja katiba ya chama.

Vuguvugu la kutaka mabadiliko ya uongozi ndani ya CUF ulipamba moto baada ya kumalizika kwa uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Igunga ambako mgombea wa chama hicho, Leonald Mahona aliambulia nafasi ya tatu, wakati katika uchaguzi mkuu uliopita alishika nafasi ya pili.

Katika uchaguzi huo chama hicho akilitumia nguvu kubwa ya fedha aikiwamo kutumia Helkopta katika kampeni zake na magari natimu kubwa ya viongozi wa juu wa chama.

Chanzo: Mwananchi
 
Hamis Hasan anatajwa kuongoza Blue-Guard kwenda kumvuruga Hamad Rashid leo.
 
Hawa ndugu wa mke wana visa sana!!!
CCM watajuta kukioa hiki chama!!
 
Kweli kuishi kwingi kuona mengi! ila hawa wote wana kauroho flan ka madaraka, maana kama nakumbukumbu nzuri huyu Hamad ndo alishinikiza bunge litambue minority ili na yeye aambulie madaraka kambi ya upinzani
 
Hawa wapemba vipi? Si ndio hawa hawa kila siku wanapiga makelele Zanzibar ijitenge? Wapi na wapi kufungua matawi Manzese? Si wakafungue huko Kibanda Maiti na Mchamba Wima? Maugomvi yao ya ndani wasituletee hapa! Kweli Tanganyika tamu nimeamini.
 
Hebu dadavua;

Hhamad Rashid anafungua tawi la CUF au lake? Maana sioni mantiki ya katibu wao kupinga - wote wazanzibari, wapemba, wanaume, majina yao Hamadi; kulikoni watu hawa fujo ughaibuni?
 
Hebu dadavua;

Hhamad Rashid anafungua tawi la CUF au lake? Maana sioni mantiki ya katibu wao kupinga - wote wazanzibari, wapemba, wanaume, majina yao Hamadi; kulikoni watu hawa fujo ughaibuni?
Au tumuombe kanali kikwete awakamate foreigners awa kwa fujo ughaibuni?
 
Sababu hasa ya ugomvi wao nini?
Halafu ni kwa nini Seif anazuia kufunguliwa kwa Tawi ilhali ni jambo la Heri kwa CUF?
 
Back
Top Bottom