Vita kati ya Mtemi Milambo na Wafipa

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
946
Mara baada ya Mtemi Mirambo kuvamia Wanyaturu na Wakimbu, mtemi Mirambo aliamua kuwavamia Wafipa. Historia inasema kuwa, kulikuwa na baadhi ya wafanyabishara kutoka katika ardhi ya Ufipa, waliokuwa wanakuja kufanya bishara na Wanyamwezi katika ardhi ya Urambo. Biashara yao ilikuwa ya kubadilishana mbuzi kwa pembe za ndovu.

Katika kufanya biashara na Wafipa, wafipa kabla ya kuondoka waliamua kumtorosha binti wa Mtemi Mirambo. Na mara baada ya Mtemi Mirambo kusikia habari hizi, kuwa Wafipa wamemtorosha binti yake (Mwanangwa). Mtemi Mirambo alikasirishwa sana na kitendo kile.

Na ndipo Mtemi Mirambo alipotao amri kwa wanajeshi wake kuwa, wawafuate hao wafipa na kuwapora mali zote na kumrudisha binti yake (Mwanangwa). Ukweli ni kwamba wanajeshi wa Mtemi Mirambo walifanikiwa kuwakamata wafipa hao na kuwapiga sana na kunyang’anya mali zote na kisha kumchukua binti wa Mtemi Mirambo. Na mara baada ya wanajeshi kurejea Urambo, ndipo Mtemi Mirambo aliposema kuwa, “Wafipa wamenikosea sana, na Hivyo nitaenda kuwavamia na kuwapiga”.

Na mara baada ya kusema hayo, Mtemi Mirambo hakutaka kuchelewa, alichukua jeshi lake na kwenda kuvamia Ufipa. Ukweli ni kwamba kulikuwa na umbali mkubwa kutoka Urambo hadi Ufipani, na kulikuwa na milima mikali sana. lakini ilikuwa ni kazi nyepesi sana kwa wanajeshi wa Mirambo. Kwani wao suala la vita lilikuwa ni la kawaida sana. Na zaidi ya hapo maisha yao yalijengwa kikakamavu sana. Kwa hiyo suala la umbali na milima halikuwa tatizo kwa wanajeshi wa Mtemi Mirambo.

walitumia siku kumi hadi kumi na mbili kusafiri kutoka Urambo mpaka Ufipa. Kulikuwa na milima, mabonde, mito na maporomoko lakini mwisho wa siku wanajeshi wa Mirambo wakiwa na Mtemi Mirambo mwenyewe walifanikiwa kufika katika ardhi ya Ufipa. Ilikuwa nyakati za asubuhi wananchi wa Ufipa walikuwa wakiamka kutoka usingizini. Mara wakasikia milio ya risasi. Milio ya risasi ilihashilia uvamizi katika ardhi ya Wafipa. Na ndipo wanajeshi wa Ufipa waliamua kukuchua mishale, mikuki na pinde na kuanza kuwashambulia wanajeshi wa Mtemi Mirambo. Ukweli ni kwamba vita kati ya Wafipa na Wanyamwezi ilikuwa kali sana. Takribani kwa saa tatu hivi, Wafipa walijitahidi kupambana na wanajeshi wa Mtemi Mirambo.

Lakini mbele ya wanajeshi wa Mirambo, Wafipa walionekana kushindwa, kwani wanajeshi wa Mtemi Mirambo walikuwa tayari walishavuta bangi. Na ilifikia wakati Wafipa waliishiwa mishale na kuamua kukata miti(mbiligi zya milungamba) na hata kutumia mawe ya moto yalikuwa yakitumika katika masuala ya uyeyushaji wa vyuma. Lakini hiyo nayo pia haikusimamisha vita kati ya wanajeshi wa Mtemi Mirambo. Mtemi Mirambo alikuwa akifurahishwa na wanajeshi wake walivyokuwa wakifuata amri zake.

kwa hakika vita ilikuwa kali, japo Wafipa walikuwa wakitumia vimbo( mbiligi zya milungamba), wanajeshi wa Mirambo walionekana kushambuliwa wakiwa na silaa zao. Wanajeshi wengi walichapwa na fimbo za Wafipa na kufa papo hapo. Wapo walikuwa wakichapwa na kuzimia hapo hapo na wengine walichapwa na kuapata kichaa cha mbwa. Hata mwangalizi wa Ikulu ya Mtemi Mirambo alishambuliwa kwa fimbo na kuanguka chini. Hakika vita ilikuwa ngumu kwa pande zote.

Ukweli ni kwamba vita kati ya Mtemi Mirambo na Wafipa ilikuwa kali sana. Na mara baada ya wanajeshi wa Mtemi Mirambo kuona kuwa vita imekuwa kali. Waliamua kupanda juu ya nyumba na kuingia ndani na kukamata Wafipa walikuwepo ndani. Wafipa waliokamatwa walifanywa kuwa wafungwa na kupelekwa mpaka kwa Mtemi Mirambo huku wakiimba nyimbo.

Wafungwa au mateka hao walikuwa wake kwa waume, na walipelekwa wakiwa kwenye mstari mpaka kwa Mtemi Mirambo akiwa na wanajeshi wake wenye sura za kutisha. Na mara baada ya wafungwa hao kufikishwa mbele ya Mtemi Mirambo, wanajeshi wa Mtemi Mirambo waliamua kuua wanawake wote waliokuwa wajawazito. Kwa wale wanawake walikuwa na watoto, walibebeshwa mizigo na hata wale watoto wapo walibebeshwa mizigo.

Na wapo baadhi ya wanaweke walibeba mizigo mizito huku walkiwa wamebeba watoto mgongoni. Na kwa wale watoto wenye umri wa kati walinyongwa kwa kuning’inizwa kwenye mtu ili ndege waje kula nyama za watu. Hakika kulikuwa na mauaji ya kutisha yaliyokuwa yakifanywa na wanajeshi wa Mtemi Mirambo. Na mara baada ya kufanya unyama huo, wanajeshi wa Mirambo waliamua kurudi Ulyanhulu wakiwa na rundo la mateka wake kwa waume. Hakika wanajeshi wa Mtemi Mirambo walifanikiwa kufika Ulyanhuru wakiwa na mateka wao na mali nyingi kutoka katika ardhi ya Ufipa.

Lakini kulikuwa na maswali juu ya ki vipi wanajeshi wa Mtemi Mirambo walifika Ufipa licha ya kuwa na milima mikali?. Wapo waliodhani kuwa, wanajeshi hao walifika Ufipa kupitia njia ya Mpanda. Kwani kutoka Mpanda ilikuwa lahisi kufika katika ardhi ya Ufipa. Jambo la kusisitiza ni kwamba, vita hivi vilikuwa kama njia moja wapo ya Mtemi Mirambo kufanikiwa kutawala maeneo kama Karema na ziwa Tanganyika. Hakika maisha ya Mtemi Mirambo yalijaa vita na mapambano. Ndio maana wazungu wa mwanzo walimwita “Napoleone Bonapate wa Afrika” maana alikuwa na maisha ya ajabu sana..

SATURDAY NJEMA
 
... nachopendea watemi (wafalme) wa zamani hususan Afrika huku jukumu lao la msingi ni kupiganisha vita na cha kuvutia zaidi wanakuwa front line kuongoza mapambano. Leo watawala wanalindwa tena wanafichwa mbali huko! Ha ha ha!

Ila asikwambie mtu, vita za enzi hizo ukatili ulikuwa kutisha. Imagine wanawake wajawazito wanatobolewa matumbo wakiachwa wajifie; watoto wa umri wa kati wananing'inizwa kwa mti kuchomekwa shingoni n.k. Of course ilikuwa ni njia mojawapo ya kumtisha mpinzani wako "usirudie tena" ila ubinadamu ulikosekana kabisa.
 
Kama ukisoma historia hizi utagundua kuwa Waafrika hatukuwa na upendo wa dhati wa aina yoyote ile,tulikuwa tumejawa na hali za kuchukiana wenyewe kwa wenyewe na ukatili wa hali ya juu, hivyo yanayoendelea sasa ni muendelezo wa iliyokuwa tabia ya muafrika wa kale ambayo kwa sasa inaendelea katika ulimwengu wa kiteknolojia.
 
Kama ukisoma historia hizi utagundua kuwa Waafrika hatukuwa na upendo wa dhati wa aina yoyote ile,tulikuwa tumejawa na hali za kuchukiana wenyewe kwa wenyewe na ukatili wa hali ya juu,hivyo yanayoendelea sasa ni muendelezo wa iliyokuwa tabia ya muafrika wa kale ambayo kwa sasa inaendelea katika ulimwengu wa kiteknolojia.
Sikweli

Hivi kuna bara lililopigana vita vya wenyewe kwa wenyewe kushinda Europe?

Hizo falme zilikuwa katika stage ya state formation hivyo hiyo expansionism ilikuwa ni lazima na hauwezi kuingia kwenye utemi wa mtu mwingine bila resistance.

Ulaya wamepigana vita toka Utawala wa ugiriki mpaka vita vya pili vya dunia hebu jaribu kupima hicho kipindi na waafrika.
 
Sikweli

Hivi kuna bara lililopigana vita vya wenyewe kwa wenyewe kushinda Europe ?

Hizo falme zilikuwa katika stage ya state formation hivyo hiyo expansionism ilikuwa ni lazima na hauwezi kuingia kwenye utemi wa mtu mwingine bila resistance.

Ulaya wamepigana vita toka Utawala wa ugiriki mpaka vita vya pili vya dunia hebu jaribu kupima hicho kipindi na waafrika.
Kama si kweli vipi tuaminishane waafrika walikuwa watu wazuri wakati hapo katika vita walikuwa wakiua hata wasiokuwa na hatia tena wakati a,mbao tayari walikuwa wamewakamata kama mateka,kama ingetokea wamekufa wakati wa mashambulizi basi tungesema vita havina macho,lakini inafikia hatua ya kubebesha hadi watoto mizigo halafu tuseme huo ulikuwa ni ubinadamu.

Ukitazama chanzo cha hiyo vita ilikuwa ni upande mmoja kumchukua binjti wa watu bila kufuata taratibu ambazo zinatakiwa katika jamii ya kiafrika,na kama wazee wa zamani tena watemi ambao ndo walikuwa wasimamizi wakubwa wa mambo ya mila na tamaduni walishindwa katika hili,ni vipi tuaminishwe kuwa Afrika ilikuwa bara salama.

Hapo ni katika kutazama ubora wa muafrika na wala si Yuropa wala kwingine.
 
Kama ukisoma historia hizi utagundua kuwa Waafrika hatukuwa na upendo wa dhati wa aina yoyote ile,tulikuwa tumejawa na hali za kuchukiana wenyewe kwa wenyewe na ukatili wa hali ya juu,hivyo yanayoendelea sasa ni muendelezo wa iliyokuwa tabia ya muafrika wa kale ambayo kwa sasa inaendelea katika ulimwengu wa kiteknolojia.
Umewahi kuona jamii za nyani zikipendana? "Joking"
 
... nachopendea watemi (wafalme) wa zamani hususan Afrika huku jukumu lao la msingi ni kupiganisha vita na cha kuvutia zaidi wanakuwa front line kuongoza mapambano. Leo watawala wanalindwa tena wanafichwa mbali huko! Ha ha ha!

Ila asikwambie mtu, vita za enzi hizo ukatili ulikuwa kutisha. Imagine wanawake wajawazito wanatobolewa matumbo wakiachwa wajifie; watoto wa umri wa kati wananing'inizwa kwa mti kuchomekwa shingoni n.k. Of course ilikuwa ni njia mojawapo ya kumtisha mpinzani wako "usirudie tena" ila ubinadamu ulikosekana kabisa.
Enzi hizo watu waliishi kama wanyama na kulikua hakuna ubinadamu.

Hata sasa wapo binadamu wachache wenye tabia kama za wanyama waliopo hifadhini.
 
Jamaa anasimulia utadhani anasimulia ile ndoto ya kutisha sana, mara nikabanwa na tumbo la kuhara ndotoni, thanks God, kikatokea ghafla choo kizuri cha dhahabu safi, ile nimemaliza, nataka tu kuflash usingizi ukakata
 
Hawa machifu wa enzi hizo walikuwa ni wanyama sana na ndio maana koo zao zote ni kama zimesambaratika kwa sababu ya laana ya matendo yao ya kinyama waliokuwa wakiwafanyia wenzao.
 
Kama ukisoma historia hizi utagundua kuwa Waafrika hatukuwa na upendo wa dhati wa aina yoyote ile,tulikuwa tumejawa na hali za kuchukiana wenyewe kwa wenyewe na ukatili wa hali ya juu,hivyo yanayoendelea sasa ni muendelezo wa iliyokuwa tabia ya muafrika wa kale ambayo kwa sasa inaendelea katika ulimwengu wa kiteknolojia.
Historia ya Ulaya umeisoma? Paper 2 of World History.
 
Back
Top Bottom