Seif al Islam
JF-Expert Member
- Nov 14, 2011
- 2,156
- 638
Wakati tukiendelea kushuhudia majina kadhaa ya watu maarufu na wasanii yakitajwa na kutakiwa kufika Kituoni kwa ajili ya Mahojiano, ningependa tujihoji maswali machache ili tuweze kupanua ufahamu wetu juu ya swala hili ambalo sasa limeteka vuchwa vya habari na likiwa limeingia katika “awamu ya pili” inayodaiwa kuwa itakuwa na “mawimbi makubwa”:
1. Kwanini “mapambano” haya dhidi ya dawa za kulevya hayaongozwi na taasisi husika kama vile Tume ya Uratibu na Udhibiti waDawa za kulevya, Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama?
2. Tatizo hili la Madawa ya Kulevya lipo Dar es Salaam peke yake?Kma ni kwa nchi nzima mbona Mikoani huko vita hii haiendelei?
3. Ni vigezo gani vinatumika kuandaa listi hizi za wanaoitwa kwenda Central?. Kama ni uchunguzi, ni taasisi gani inayofanya uchunguzi huo?
4. Kwanini watuhumiwa hawa wanaitwa Central Police wakati aliyeandaa List hahusiki na hana mamlaka yoyote kisheria pale Polisi Central?
5. Watauhumiwa hawa wanapofika Central nani anayewahoji?
6. Serikali iliyopita iliwahi kujinadi kuwa wanayo listi ya Wauzaji wa Dawa za Kulevya, je watuhumiwa hawa ni sehemu ya listi hizo? Kma jibu ni ndio kwanini listi haikukabidhiwa kwa vyombo husika?
7. Mwendeshaji wa “mpambano” haya akiacha kwa sababu yoyote iwayo, mapambano yatakuwa yamefikia tamati au yataendelea?
Nadhani haya ni baadhi ya maswali muhimu ya kujihoji katika wakati huu ili kuondoa miguno na sintofahamu zinazoweza kuibuka au kuibuliwa.
Nimeona ni vyema tujiulize haya