NGAYANIMO
Member
- Feb 17, 2026
- 36
- 55
VITA BARANI AFRIKA..
Nchi ya kwanza kujitawala upya katika Afrika ni nchi za Afrika ya Kusini zilizojiunga na kujiendesha wao wenyewe katika mwaka 1910. Misri, katika mwaka wa 1922 walikuwa wanajiendesha wenyewe, na Tangier katika mwaka wa 1925.
Madola mengi ya Afrika yalianza kupigania uhuru katika miaka ya baina ya 1950 na 1960, na Wazungu wakasalimu amri na kuanza kutoa uhuru. Libya wakajinyakulia uhuru katika mwaka wa 1951, Eritrea katika mwaka 1952 ikiwa imejiunga na Ethiopia, Morocco katika mwaka wa 1956, na wakarudishiwa Tangier.
Katika mwaka huu wa 1956, Sudan na Tunisia vile vile walipata uhuru wao, na Ghana katika mwaka wa 1957, Guinea katika mwaka wa 1958, na vile vile Morocco wakarudishiwa Spanish Morocco.
Katika mwaka wa 1960 Ufaransa ukatoa uhuru kwa Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Congo (Brazzaville), Cote d'Ivoire, Dahomey (Benin), Gabon, Madagascar, Mali, Mauritania, Niger, Senegal na Volta ya Juu (Burkina Faso).
Vile vile, katika mwaka huohuo wa 1960 Congo (Kinshasa), Nigeria, Somalia, na Togo zikapata uhuru, na katika mwaka wa 1961 Sierra Leone na Tanganyika zikapata uhuru, na Afrika ya Kusini ikawa Jamhuri.
Katika mwaka wa 1962 Algeria, Burundi, Rwanda, na Uganda zikawa huru, na 1963 zikafuatia Zanzibar, Gambia na Kenya, na katika mwaka wa 1964 Malawi (Nyasaland), na Zambia (Rhodesia ya Kaskazini) zikapata uhuru.
Baada ya miaka miwili, katika mwaka wa 1966 Botswana (Bechuanaland) na Lesotho (Basutoland) zikajinyakulia uhuru. Mauritius na Swaziland katika mwaka wa 1968 na vile vile Guinea ya Ikweta. Hispania ikairudisha Ifni katika mwaka wa 1969 katika mamlaka ya Morocco.
Aidha, katika mwaka wa 1974 Guinea ya Kireno (Guinea-Bissau) ikapata uhuru wake, na katika mwaka wa 1975 Angola, Cape Verde, Mozambique, Sao Tome na Principe zikapata uhuru. Hispania vilevile ikaitoa Sahara ya Magharibi kwa Morocco na Mauritania katika mwaka wa 1976, lakini wananchi wakakataa kuwa chini ya nchi mbili hizi, kukazuka vita. Mauritania ukaitoa sehemu yake na kuipa Morocco katika mwaka wa 1979, tatizo ambalo mpaka sasa linaendelea baina ya Morocco na Sahara ya Magharibi, na Umoja wa Mataifa unajaribu kutatua tatizo hili. Waingereza wakawapa uhuru Shelisheli katika mwaka wa 1976, na Ufaransa ukatoa uhuru kwa visiwa vya Ngazija (Comoro).
Katika mwaka wa 1977 Jibuti (Nchi ya Afars na Issas) iliyokuwa ikitawaliwa na Wafaransa ikarudi kwa wenyewe. Rhodesia (Zimbabwe) ikapata uhuru halisi mwaka wa 1980, na South West Africa, iliyokuwa ikitawaliwa na Afrika ya Kusini ikapata uhuru katika mwaka 1990 na kuitwa Namibia.
Uingereza umebaki na visiwa vya Saint Helena na Ascension, na Ufaransa unaendelea kutawala Mayotte na Reunion. Hispania vilevile unaendelea kutawala visiwa vya Canarias pamoja na Ceuta na Melilla na visiwa viwili vingine vilivyoko karibu na Morocco.
KWANZA UNIT - SO WHY
Verse..1.( chief Ramsone)
"Mlii wa parabanda yowe la vita wahutu nchini Rwanda/
Ebu.! Tunukuu juhuzu za O.A.U/
Umoja Afrika /
Yote Tuombe Toba /
Ebusha Viumbe na mabomu Aridhini Angola 🇦🇴 /
Eeh..! Mola
Eeh..! Mola
Mashood Abiola haki yake wapi, kwame nkuluma, Steve biko Tuunganishe Hip Hop/
Wanasiasa wanaangamiza swala hili natatiza/
Dunia yote inajiuliza/
So why..?
Hivi Kwanini..?
Wasio na hatia wanapoteza uhai..
Chorus..
"Afrika , Afrika wewe
So why ..?
Afrika, Afika yowe
So why ...? "
Verse..2.( D.Rob)
"Hivi kwanini..?
Usiniulize mimi/
Jiulize wewe/
Hivi Kwanini..?
Tumwange Damu yetu si wenyewe /
Nasikitisha/
Natatanisha/
Yoh..!!
Kama maisha yenyewe ndio hivi Afrika Tutafika /
Mwisho wa safari Bara hili kuelimisha/
Sasa tupatane/
Tupendane/
Yoh..!!
Kwanini..?
Tupigane sababu ya wachache/
Kama Amani basi aache/
Amani iwe juu na siraha nazo ziachwe /
Tutuze Bara hili Afrika tufaidike/
Vita na maovu tuebuke/
Walokufa tukumbuke/
Milio ya risasi na mabomu isisikike/
Waasi wafichuke/
Na macho ya wa Afirika yafunguke/
Amani imepanuke Afrika yote/
Viongozi tukutane Tuongee swala kwa wote/
Damu imemwangika yakutosha/
Mizinga iliporushwa /
Watu wakafa njaa/
wengine kukosa jamaa/
Wakimbizi wamezangaa/
Hakuna pakukimbilia/
Watoto wanalia/
Wasio na hatia/
Wana Ang'amia /
Mungu atasaidia/
kama tutaonyesha njia/
Onyesha njia/
So why...!!"
Chorus..
"Afrika , Afrika wewe
So why ..?
Afrika, Afika yowe
So why ...? "
Verse "Chief Ramsone "
Afya ...!!
Maisha marefu Nyerere, mzee Mandela/
Nipo ndani ya istemela Naelekea kuzulu narudi carryall nakuamulu F.I.S
weka chini mtutu watoto wadogo vitani marufu
Verse "D rob"
"Amani na Upendo vionyeshwe kwa matendo/
Afrika itatulia ..
Hivi kwanini...?
JIulize Mara mbili/
Tena kwa makini/
Afrika nini..?
Nani..? jenzi Taifa teule /
Kama si mimi , wewe au Yule/
Udungu umetoeka/
Jamii inateseka/
Ona hali hii inavyojionyesha/
Wakimbizi wanatoeka
Hawana Urundi kwa makundi .."
Verse. "Chief Ramsone "
A.F.I , I.S.A Kama sikosei wote ndugu tokea Eeh.. Nuhu /
Abidjan kusini kwa 🇸🇩 sudani , Somalia 🇸🇴 upendo sabaya hadi Liberia 🇱🇷 /
Hivi kwanini...?
Wasio na hatia wanapoteza uhai
Chorus..
"Afrika , Afrika wewe
So why ..?
Afrika, Afika yowe
So why ...? "
Ukwaju wa kitambo
0767 542 202